Nazidi kujikita Ughaibuni

Mkuu hongera sana. Upo pande zipi hapo Uswid. Stockholm ana Umeå? Gothernburg Anna Linköping? I hope muda huu una enjoy joto la summer na kimvua cha hapa na pale. Hongera pia kwa kupata Scholarship. I hope unamega 10,000 SEK @ month sawa na 2.7M za kibongo.

Kumbuka kufanya savings. Tuma pesa kidogo home ila usisahau kufanya savings. Kwenye ile bank account unakuwa na account mbili ile ya kawaida na ile ya savings. Uwe unaweka pesa za matumizi kwenye account ya kawaida na savings kwenye account yake.


Kwakuwa ushapata personal number maana yake unaweza pia kufanya vibarua vya hapa na pale huku ukiwa unasoma. Ukisema unapatikana mji gani mie nitakushauri kibarua gani kitakuwa rahisi kuendana na masomo. Kila la kheri.!
Gottsunda, uppsala mkuu...!!
 
Wakuu baada ya kukimbia joto la jiwe Bongo land kufuatia shuruba nzito zilizokuwa zikifanywa wakati wa utawala wa mwendazake na wafuasi wake.

Niliamua kukaa hapa Sweden kwa miaka 2 mpaka sasa kwa visa ya matembezi huku nikiishi kwa hisani ya vibibi vya kizungu hatimae kupata ajira ya muda mfupi kufuatia maelewano yangu mazuri na vibibi hivi.

Mpaka nilipo amua kubadili gia na kuomba scholarship ya shule na hatimae kupata kibari cha kuishi Kama mwanafunzi hivyo kuzidi KUJIKITA zaidi huku ughaibuni na Sina wazo la kurudi bongo ya mama Samia suluhu kwa Sasa.

Msalimieni sana mama mwambieni Nina Imani nae.

View attachment 1830842
Kumbe maneno yetu makali yalisaidia. Ungelegea urudi sasa hivi na wewe ungekuwa unasubiri ajira za manati!
 
Back
Top Bottom