Nayapenda makabila yanayoenzi matambiko ya kimila kwani matambiko sio ushirikina

kwa uelewa wangu imani yeyote ambayo haimuhusishi Mungu aliye hai ni ushirikina... kufanya matambiko ni ushirikina pia hauna tofauti na uchawi
Dini na zenyewe zinafanya matambiko, au hujui kuwa kuhiji ni tambiko? Au kwavile hayo mahekalu hayapo Afrika?
 
Anaesema matambiko ni ushirikina basi kwa wakristu ile altare wanayozunguka kwa mishumaa ni ushirikina tena wa kizungu . Zingatia tambiko lako la kiafrika
Mwafrika ni mpuuzi tu ndo mana anaambiwa yeye ni nyani na still anakubali sasa mtu anashindwa ata kufatilia vizazi vyake vitano vya nyuma na kujua vilikuwa vinaishije na yeye improve vipi ndo kwanza anaona ni takataka Hawa wazungu na waarabu kweli wametukamata pabaya jitu linanua maji ya baraka eti linywe ukiliambia rudi nyumbani kila mwaka Kawaenzi babu zako walau kwa Kuchinja na Kula litakuambia ni ushirikina apo linaombewa kutwa linapewa mafuta sijui maji ya baraka simple tu mtu anaamini na kupigwa hela
 
Siyo mimi tuu nimeacha,na familia yangu na jamaa zangu na wachagga wengine wengi sana wameachana na huu ushetani na kuamua kuambatana na Yesu anayeokoa na kukomboa na kufungua vifungo.Wewe acha ushamba nenda makanisani uone jinsi wachagga tunavyomtumikia Mungu,utaona wivu na kujuta ulikua wapi siku zote.
Jamaa wewe ni mwehu kabisa, Yesu ana asili yoyote na wewe, unajivisha ujinga tu au nyie ndio wayahudi weusi na mibendera juu ya israel mmeweka makwenu
 
Hata shetani naye anaenda kanisani,haujasoma kwenye kitabu cha Ayubu kuwa wana wa Mungu walipokusanyika Shetani naye alijihudhurisha?
Ayubu ni nani babu zako walitumia hilo jina?? Hamna ata majina ya asili huko.kwenu au nayo ni ujinga? Ndio mana mnahangaika na magonjwa tu kwa ujinga huu endelea kukemewa mapepo mtumwa wa fikra wewe
 
Waafrika tunazidi kuwa watumwa kutopenda mila zetu

Binafsi napenda makabila yanayoendeleza matambiko ya kimila

matambiko sio ushirikina nachukia ushirikina na uchawi wa kwenda wa waganga sana nakataa hayo mambo.

Ila matambiko ya kimila ni ibada nzuri sana kwa sababu haihusishi ushirikina wala kumtoa mtu kafara

Hizi ibada za matambiko hazijaanza leo toka enzi za ibrahimu alipotaka kumtoa isacka

Ndo maana jamii nyingi duniani nenda mpaka kwa wajapan, wachina mpaka wazungu matambiko yapo

Moja ya faida ya matambiko ni kuwa mungu anajibu haraka mnoo kupitia matambiko

Mtakesha sana misikitini na makanisani mkiomba mathalani mvua lakini wanaotambika wataomba mvua na itanyesha

Kama matambiko ni mabaya kwanini wengi wamuombao mungu kupitia matambiko hupata majibu haraka??

Kama ni mgonjwa hupona
kama ni balaa huondoka
kama ni laana huisha
kama ni mvua zitanyesha
kama ni njaa neema zitakuja

Naunga mkono matambiko ya kimila na makabila yote yanayoendelea matambiko nayasupport kwa 100%

Tatizo Mwafrika hana Imani na cho chote kilicho chake ukisha ona mtu anajaribu mpaka kubadilisha mwonekano wake kwa kudhani sio mzuri (haupendezi), kutukuza utamaduni wa mtu mwingine basi ujue tatizo ni kubwa sana. Lakini kwa kifupi dini zote zimetokea kwenye matambiko alichokifanya Myahudi Abraham anasemekana kuwa ndio baba wa Imani kwenye kitabu cha historia kiitwacho Biblia, angekifanya Msukuma au Mnyakyusa leo Waafrika tungesema uchawi. Mambo kama al badri kwenye Imani za Kiislamu zina tofauti gani na ushirikina..?!! Wajapani na wengine wa Mashariki wana Imani zao tofauti kabisa na Ukristo au Uislamu na wanaendelea vizuri na wanakula neema hapa hapa duniani. Kipimo gani tunatumia kusema hizi Imani za ku import na nyingine tulifundishwa kwa nguvu eti ndio Imani za kweli?? Tatizo liko kwetu na usikute msoto huu unaonatupata Waafrika ukawa unatokana na kuacha Imani zetu na kuwatelekeza mababu zetu. Leo hatuna mbele wala nyuma shida, mateso na kudharaulika imekuwa ndio kitambulisho na Mwafrika na mtu mweusi popote pale alipo kwenye sayari hii. Hebu tusiwe wa haraka kupayuka kabla ya kufakari kwa kina bila uwogo tujiulize tatizo nini..!!
 
Mkuu umeongea point sana sana, Unajua sisi kila chetu hakifai, leo mtu anamuenzi Abraham au Mohamed na kusasau kuwa babu zake wala hawakumjua kabisa Mkuu kuna takataka kibao zinafanyiika huko misikitini na makanisani io albadiri ni mfano mdogo sana ila mtu huona ni baraka ila chake ni laana, mfano mzuri pia huo uliotoa wa ngozi
 
Ndugu mbona umekuwa mkali mno?

Jaribu kuwaeleza kawaida watakuelewa mkuu tu.
Jamaa ni zaidi ya Malimbukeni kama umefata dini fulani huo ni uhuru hukatazwi ila sio kuita babu zako wamelaaniwa je bila wao kulea vizuri generation kwa kile unachoona sasa ni Kibaya je ungezaliwa leo hii?? Na kumjua uyo Yesu ama mtume unae muona wa maana sanaaa
 
Mimi linapokuja swala la matambiko actual sipuuzi hata kidogo ninachowasihi tu ni kuwa matambiko hayo yasi athiri uhai au kuchukiza wengine ila yafanyike na ninajitahdi kukaa na wazee kila nirudipo kijijini kufahamu machache juu ya utamaduni na vitu vya nyumbani Natoa mchango mkubwa sana kuhakikisha izo mambo zinafanikiwa nina miaka sijakanyaga msikitini wala kanisani, Maisha ni safiii tu
 
Jamaa ni zaidi ya Malimbukeni kama umefata dini fulani huo ni uhuru hukatazwi ila sio kuita babu zako wamelaaniwa je bila wao kulea vizuri generation kwa kile unachoona sasa ni Kibaya je ungezaliwa leo hii?? Na kumjua uyo Yesu ama mtume unae muona wa maana sanaaa

Kabisa.

Usemacho kina maana na ni jambo rahisi kulielewa isipokuwa kueleweka kwa walimwengu waliotekwa akili na ukoloni wa kiimani itakuwa ngumu sana kwakuwa fikra na mawazo yao yametekwa na nguvu ya kutawaliwa na ukoloni.
 
Tunasafari ndefu sana mkuu, Hata haya matatizo mengi ya sisi africans kuna muda unawaza tu sijui ni huu Ujinga wa kusahau kabisa vizazi vyetu vya nyuma hata kuvienzi tu, leo tunawasoma ni ceaser,Da vinci, Jesus wa miaka mingi mno ambapo ata wazo la hizi dini mpya halikuwepo huku kwetu na babu zetu still walimudu maisha
 
Waafrika tunazidi kuwa watumwa kutopenda mila zetu

Binafsi napenda makabila yanayoendeleza matambiko ya kimila

matambiko sio ushirikina nachukia ushirikina na uchawi wa kwenda wa waganga sana nakataa hayo mambo.

Ila matambiko ya kimila ni ibada nzuri sana kwa sababu haihusishi ushirikina wala kumtoa mtu kafara

Hizi ibada za matambiko hazijaanza leo toka enzi za ibrahimu alipotaka kumtoa isacka

Ndo maana jamii nyingi duniani nenda mpaka kwa wajapan, wachina mpaka wazungu matambiko yapo

Moja ya faida ya matambiko ni kuwa mungu anajibu haraka mnoo kupitia matambiko

Mtakesha sana misikitini na makanisani mkiomba mathalani mvua lakini wanaotambika wataomba mvua na itanyesha

Kama matambiko ni mabaya kwanini wengi wamuombao mungu kupitia matambiko hupata majibu haraka??

Kama ni mgonjwa hupona
kama ni balaa huondoka
kama ni laana huisha
kama ni mvua zitanyesha
kama ni njaa neema zitakuja

Naunga mkono matambiko ya kimila na makabila yote yanayoendelea matambiko nayasupport kwa 100%

Binafsi mi sipendi misikiti wala makanisa kwa sababu hayana maana kwetu, tumeletewa tu ili tusahau mila zetu tuendekeze mila za watu. Nawashukuru wazazi wangu kutufundisha hii mila na I'm so proud of it kwani naona jinsi Mungu anavyotusaidia kiukoo.
 
Keep it up mkuu, mimi nitajifunza na kutumia tech zao hata lugha pia but swala la imani ni too sensitive siwezi kuwafata niliwahi andamwa na majanga mpaka nkarudi bush huko nkakaa na wazee na Nikatoa kidogo tukafanya kama kuwakumbuka babu, Nashukuru mambo yameninyookea je ningesema sijui ni okoke nipigwe hela na muda wangu na hawa Manabii uchwara si mpaka leo ningekuwa kiguu na njia na makanisa yote ningemaliza lakini kijijini huko najua ni mara moja kwa mwaka kama sina nafasi nanua Ni mbuzi ngombe nawapa mambo yananyooka.
Sitaki kusikia habari za kanisani wala msikitini, Sijui yesu sijui mtume sijui wokovu, Yani sina akili kabisa niende macca kuhiji sijui kwenye kaburi la Mohammed au israel.sijui eden ile hali makaburi ya babu zangu yanapotea hata kuyajengea mtu unashindwa huo ni zaidi ya Ujinga, Ujinga sio tusi bali ni sifa
 
Keep it up mkuu, mimi nitajifunza na kutumia tech zao hata lugha pia but swala la imani to sensitive siwezi kuwafata niliwahi andamwa na majanga mpaka nkarudi bush huko nkakaa na wazee na Nikatoa kidogo tukafanya kama kuwakumbuka babu, Nashukuru mambo yameninyookea je ningesema sijui ni okoke nipigwe hela na muda wangu na hawa Manabii uchwara si mpaka leo ningekuwa kiguu na njia na makanisa yote ningemaliza lakini kijijini huko najua ni mara moja kwa mwaka kama sina nafasi nanua Ni mbuzi ngombe nawapa mambo yananyooka.

Nakuambia waarab na wazungu ndiyo waliotupa laana hizi tulizonazo sasa, mabalaa ya njaa, na majanga kibao yote hiyo ni kwa sababu mizimu yetu imekasirika kwanini tuwasuse wao tuwafuate watu wa nje na imani zao zisizo tuhusu na kuzifanya kuwa zetu?
 
Mkuu kutoka kwenye huo utumwa ni kazi ngumu mno watu wametopea uko Kabisa, Na niwana andanwa kweli.kweli na mabalaa wanabaki kuhama hana mara leo kanisa hili mara kesho lile, Hakuna namna watu wataacha huo ujinga
 
Inasikitisha sana kuwa watumwa wa dini na imani za watu mpaka tunachezewa akili. Kuna yule nabii wa Afrika Kusini anayewaambia waumini wake wapige punyeto kwanza kabla ya kusali na wanafanya hivyo tena mbele ya watoto wao. Yaani dini zinatumiwa kutufanya sie waafrika wajinga, yaani basi tu.
 
Back
Top Bottom