Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Rapa Nay wa Mitego baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Shika Adabu Yako’, Jumatatu ijayo anatarajia kuachia ngoma mpya na kali iitwao ‘Saka Hela’.
Akizungumza hivi karibuni, Nay amesema mara nyingi amekuwa akionesha mali zake pamoja na pesa ili kuwatia machugu vijana ya kutafuta pesa.
“Tarehe 9 ya mwezi huu, i mean Jumatatu ijayo nitaachia rasmi video yangu mpya ya wimbo ‘SakaHela’ , kaa tayari kwenye runinga yako. Saka Hela ni wimbo ambao unatoa majibu kwanini mara nyingi nimekuwa nikionesha mali zangu, kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula kuona kigongo kingine,” alisema Nay.
Nay ni mmoja kati ya wasanii ambao wanaweza kucheza na hisia za mashabiki wake kutokana namna ya utunzi wa mashairi yake ambayo huwashika mashabiki.
Source: Bongo 5