Nawezaje kuwa Raia wa Tanzania?

Maelezo yako ni mazuri sana.

Hata hivyo Naomba niweke maelezo ya nyongeza kama ifuatavyo:-

1. Mwombaji wa uraia lazima awe anaishi nchini kihalali. Naamanisha awe anaishi kwa kibali (residence Permti) halali kilichotolewa na Uhamiaji.
Vibali vipo vya aina nne :-

(i) Residence Permit Class A
(ii) Residence Permit Class B
(iii) Residence Permit Class C
(iv) Dependant Pass

2.Sheria ya Uraia kwa sasa inanukuliwa hivi:-

"Sheria ya Uraia Sura ya 357, rejeo la mwaka 2002.

Naomba kuwasilisha.

Wahusika wa Idara ya Uhamaiji kama watapitia hapa wanaweza kuja kusahihisha pale kwenye makosa au kutoa ufafanuzi zaidi wa Kitaalamu.
Shukrani mkuu
 
Wasalaam, naomba kuuliza endapo mimi ni raia wa nchi nyingine, lakini kutokana na mapenzi yangu kwa nchi ya Tanzania na watu wake, nikatamani au kutaka kua raia wa tanzania na kuridhia kuukana uraia wa nchi nilimotoka.

Je, ni hatua zipi yapaswa nifanye kuweza kukamilisha hilo? Ni njia ipi rahisi ambayo itaniwezesha kuupata uraia mapema pengine bila kusubiri au kuishi miaka mitano. Inashangaza kusikia ama kuona kuna Watanzania hawaipendi nchi yao wanakuambia bora wakawe mbwa ulaya, na ilihali kuna wengine nchi zingine wanatamani kua raia wa tanzania, wanaipenda tanzania, wanatamani kuishi tanzania, wanapenda lifestyle ya watanzania, wanapenda wadada / wakaka wa kitanzania, wanatamani kuoa/kuolewa na mtanzania.

Anyway, msaada wa swali hapo juu.
Ni kweli kuna watu wa nchi za kigeni wangependa waje wawe angalau Maumbwa nchini Tanzania
 
URAIA WA TANZANIA



UTANGULIZI

Masuala ya uraia nchini Tanzania yanasimamiwa na sheria ya Uraia Na. 6 ya 1995, pamoja na Kanuni zake za mwaka 1997. Kwa mujibu wa sheria hiyo, zipo aina tatu za uraia nchini Tanzania ambazo ni;

i. Uraia wa Tanzania kwa kuzaliwa

ii. Uraia wa Tanzania kwa kurithi

iii. Uraia wa Tanzania kwa Tajnisi
Uraia wa Tanzania kwa Kuzaliwa.

Kwa mujibu wa Sheria ya Uraia ya Na. 6 ya Mwaka 1995, mtu yeyote anayefuzu kuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa ni yule aliyezaliwa nchini Tanzania na ambaye wakati wa kuzaliwa kwake mmoja wa mzazi wake alikuwa raia wa Tanzania.
Uraia wa Tanzania kwa Kurithi

Mtu yeyote aliyezaliwa nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Muungano au baada ya Muungano anahesabika kuwa raia wa Tanzania kwa kurithi kuanzia tarehe ya kuzaliwa kwake kama siku ya kuzaliwa kwake mama au baba yake ni raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzaliwa au tajnisi. Hii ina maana kuwa kama wazazi wake walikuwa ni raia wa Tanzania kwa kurithi wakati wa kuzaliwa kwake mtu huyo hawezi kuwa raia wa Tanzania kwa kurithi.
Uraia wa Tanzania kwa Tajinisi:

Mtu yeyote ambaye siyo raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzaliwa au kurithi anaweza kuomba uraia wa Tanzania kwa tajnisi kwa mujibu wa vifungu Na.8 na 9(1) vya Sheria ya Uraia ya 1995. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, Mhe. Waziri mwenye dhamana ya kusimamia masuala ya uraia nchini (kwa sasa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi) ndiye mwenye mamlaka ya mwisho kutoa au kutotoa uraia wa Tanzania kwa wageni walioomba uraia.
Sifa za Kuomba uraia wa Tajnisi:

Mgeni anayetaka kuomba uraia wa Tanzania anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:-

i. Mwombaji awe na umri wa miaka 18 au zaidi na awe na uwezo wa kufanya maamuzi yanayokubalika kwa mujibu wa sheria za nchi

ii. Awe ameishi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muda wa miezi 12 mfululizo kabla ya kutuma maombi

iii. Katika muda wa miaka kumi kabla ya miezi kumi na mbili hiyo awe ameishi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muda usiopungua miaka saba

iv. Awe anaelewa vizuri lugha ya Kiswahili au Kiingereza

v. Awe na tabia nzuri

vi. Awe alichangia na ataendelea kuchangia katika ukuzaji wa uchumi, Sayansi na teknolojia na utamaduni wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

vii. Awe anakusudia kuishi moja kwa moja ndani ya Jamhuri ya Muungano ikiwa ombi lake la uraia litakubaliwa

Taratibu za kuomba uraia wa Tajnisi

Zifuatazo ni taratibu za kuomba uraia wa tajnisi kwa mgeni ambaye ana umri wa miaka 18 na kuendelea:-

i. Mwombaji anatakiwa kujaza fomu za maombi ya uraia ambazo zinapatikana katika ofisi zote za Uhamiaji za Wilaya, Mikoa na Makao Makuu

ii. Mwombaji anatakiwa kutoa matangazo ya nia yake yakuomba Uraiya mara mbili mfululizo kwenye gazeti lililosajiliwa Tanzania
Tanzania Bara na Zanzibar.

Mchakato wa kushughulikia maombi ya uraia

Ili kuhakikisha kuwa wageni wanaopewa uraia ni wale wenye manufaa kwa Taifa, maombi yote yanapaswa kupitia na kujadiliwa katika vikao vya Kamati za Ulinzi na Usalama vya:-
Ngazi ya Kata au Shehia (kwa upande wa Zanzibar)

Katika ngazi ya Kata au Shehia anayoishi mwombaji atahojiwa na maombi yake kujadiliwa na kikao hicho na hatimaye ombi kupelelekwa kwa Mkuu wa Wilaya kwa hatua zaidi.
Ngazi ya Wilaya

Kikao cha Ulinzi na Usalama cha Wilaya hujadili maombi ya uraia na hatimaye kutoa maoni na mapendekezo yake
Ngazi ya Mkoa

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa hujadili maombi yaliyowasilishwa na kutoa maoni na mapendekezo yake kuhusiana na ombi husika na hatimaye hutumwa kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji au kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, ambaye naye hutoa ushauri na mapendekezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Waziri wa Mambo ya Ndani ndiye mwenye mamlaka kisheria kutoa Uraia wa Tanzania kwa Tajinisi.
whyme mambo yote yako hapa.
Kama una swali la nyongeza uliza wajuzi kama hawa.
Acha kujibizana na hao wapambe wa thread.
 
Back
Top Bottom