Nawezaje kuwa na furaha na amani ya roho?

Quetzal

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
6,331
10,751
Nimekuwa myonge na nafsi Yangu inasononeko.

Sikosi chakula wala pakulala...Ila nakosa furaha moyoni, naona uzito rohoni mwangu, nakosa furaha kabisa.

Naona mambo yangu nashindwa yabeba.

Najitahidi kusali na kukumbuka maandiko ya Mungu, napata afueni kwa muda.

Japo najipa moyo kuwa kwenye uzito Kuna wepesi...Naamini nothing last forever not even our troubles.

Kuna muda nikitembea barabarani nikiona watu wanacheka nahisi wananicheka Mimi.

Huu Uzi hauhusu mahusiano ya kimapenzi kabisa.

Sinywi pombe, sivuti Bangi wala sigara.

Nifanyaje kupunguza Hali ya sononeko moyoni mwangu.
 
Una kazi? Umri wako? Unaishi kwako (umepanga) au bado uko nyumbani? Nijibu nitakushauri Jambo
 
Ukiwa kwenye hali hiyo usiruhusu mawazo mabaya/negative kutawala. Jaribu kukumbuka moments nzuri ulizowahi pitia na kukupa furaha hakika itakufanya nafsi yako kusuuzika
 
Hali hii imeakuanza lini? Ni mara yako ya kwanza au huwa inakutokea mara kwa mara? Je, kuna tukio lo lote baya (mf. kufiwa na mzazi au mpendwa wako) ambalo limetokea au lilitokea kipindi hiki? Afya yako ikoje? Umeongezeka (sana) uzito au kukonda ghafla? Kazini kuna misukosuko? Maisha yako kimapenzi yamekaaje? Kuna mabadiliko yo yote hasi kiuchumi? Ulikuwa mfuasi wa CHADEMA katika uchaguzi uliopita? Kiroho umesimama imara?

Majibu ya maswali hayo juu (na mengineyo) yaweza kutoa fununu lakini pia yawezekana ni msongo wa mawazo (depression) umekuanza. Kama ni hivyo utahitaji msaada wa kitaalamu kutoka kwa daktari wako au watoa nasaha. Au yawezekana ni mvurugano tu wa homoni na makemikali mwilini na hali hiyo yaweza kujirekebisha yenyewe tu.

Kwa sasa jaribu kuwa karibu na watu wakupendao. Kama kuna mmoja unayemwamini mwambie unavyojisikia. Unahitaji faraja na watu wanaojali. Kama ni muumini yawezekana pia ikawa ni vita vya kiroho. Mbali na wewe mwenyewe kupambana katika maombi, jaribu kumshirikisha kiongozi wako wa kiroho. Kama upo katika kikundi cha maombi au jumuia waombe wawashe moto wa maombi kwa ajili yako. Epuka kuwaza mawazo hasi na jitahidi sana kufanya mambo uyapendayo na hasa hasa kusaidia wenye shida. Badala tu ya kujifungia ndani, kama unaweza, nenda hata hospitalini huko ukasalimie wagonjwa siku za wikiendi au wakati wo wote unapokuwa na muda. Saidia watoto katika vituo vya mayatima huko na matendo mengine madogo madogo ya wema. Naamini baada ya muda msukosuko huu utapita, moyo wako utatanzuka na furaha yako itarejea.

Na kumbuka tu kwamba "you are fearfully and wonderfully made. Mungu Akubariki.

20201112_092610.jpg
 
Tafuta movie/ drama za kikorea ambazo hazijatafsiriwa, hutojuta ushauri huu.

Mimi nikitoka kazini fasta home, napita sokoni, napitia maziwa. Nikifika ni movie na kula, kunywa, kuchungulia JF. Hayo ndio maisha yangu.

Hii ndo njia pekee ya kupunguza stress, kuna kipindi nilikuwa kama wewe sasa hivi nimezoea.

Wengine watakushauri utoke out. Ila najua sio rahisi utoke out, kufanya nini?

Wengine watakwambia utoke na marafiki. Marafiki wapi? Wakati mmetoka kazini mkaenda home utoke kwa lipi? Mkifika huko mfanye nini wakati umeshiba?

Poole dia hiyo hali naijua huwa haielezeki.
 
Tafuta movie/ drama za kikorea ambazo hazijatafisiliwa,hutojuta ushauri huu.

Mm nikitoka kazini fasta home, napita sokoni , napitia maziwa. Nikifika ni movie na kula, kunywa, kuchungulia jf.hayo ndo maisha yangu.

Hii ndo njia pekee ya kupunguza stress.kuna kipindi nilikuwa kama wewe sasa hivi nimezoea.

Wengine watakushauri utoke out. Ila najua sio rahisi utoke out kufanya nini?

Wengine watakwambia utoke na marafiki. Marafiki wapi? Wakati mmetoka kazini mkaenda home utoke kwa lipi? Mkifika huko mfanye nini wakati umeshiba?

Poole dia hiyo hali naijua huwa haielezeki.
Naomba hizo movie basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuexperience kwako hii hali hujajua tu bado unaweza ikawa inasababishwa na nini?
 
Inabidi ujue chanzo cha tatizo lako,(underlying cause) then ndo utafute suluhisho. Jiulize mwenyewe hio hali imeanza lini, unaweza Pata chanzo cha tatizo lako.
Pia unaweza waona psychologist au viongozi wa kiimani wakakusaidia.
Asante.
 
Nimekuwa myonge na nafsi Yangu inasononeko.

Sikosi chakula walapakulala...Ila nakosa furaha moyoni, naona uzito rohoni mwangu, nakosa furaha kabisa.

Naona mambo Yangu nashindwa yabeba.
Najitahidi kusali na kukumbuka maandiko ya Mungu, napata afueni kwa muda.

Japo najipa moyo kuwa kwenye uzito Kuna wepesi...Naamini nothing last forever not even our troubles.

Kuna muda nikitembea barabarani nikiona Watu wanacheka nahisi wananicheka Mimi...

Huu Uzi hauhusu mahusiano ya kimapenzi kabisa.

Sinywi pombe,sivuti Bangi Wala sigara.

Nifanyaje kupunguza Hali ya sononeko moyoni mwangu.
Nishakuelewa ugonjwa wako.
Hata mimi nilikuwa na ugonjwa kama huo.
Huwa ugonjwa unasababishwa na loneliness/antisocial behaviour.
Inawezekana mazingira uliyolelewa ulikuwa hupati nafasi ya kujichanganya na watu ambayo hiyo hali imeendeleza upweke ambao ndio unakusumbua hadi leo.

Dawa ya huo ugonjwa ni kujichanganya na watu mbalimbali kwa mfano hata kama hunywi pombe sio mbaya mara moja moja kujichanganya na marafiki kwenda sehemu za kurelax inaweza kuwa beach au pub au kwenye mahotel.

Mimi hiyo hali huwa inaondoka nikitoka nyumbani na kujichanganya na watu pamoja na kusafiri sehemu mbalimbali.
Chukua hatua
 
Back
Top Bottom