Nawezaje kutumia Zantel kwenye Huawei E160? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawezaje kutumia Zantel kwenye Huawei E160?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Jaluo_Nyeupe, Jan 12, 2011.

 1. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Wataalam,
  Nina modem yangu ya Huawei E160x (model K3565-rev2) unlocked. Nimejiunga na Zantel Highlife sasa nataka kutumia kwenye hiyo modem yangu lkn tatizo nashindwa kununua bundle ya 2GB kwa kuwa kuna sehemu nikifika inanidai number ya modem na kutoa mf. 0775x xxxxxx. Nimejaribu kuingiza number ya hiyo line lakini imegoma, naomba msaada tafadhali kama jambo hili linawezekana.
   
 2. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  huduma ya highlif hiyo ipo kwenye CDMA,ili uweze kutumia huduma hiyo lazima uwe na modem ya Zantel, sasa sijuwi umejiunga vp! Au sijakuelewa?
   
 3. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Sio kweli mkuu, sio lazima uwe na modem ya zantel ndio uweze kujiunga na huduma ya highlife. Kwani kuna faida nyingine hata wakati wa kupiga simu unapokuwa umejiunga na Highlife. Mimi nilijiunga kwa kutumia simu yangu ya mkononi tu na wakanijulisha kuwa nimejiunga na Highlife pamoja na kunikata sh !1000.
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sina utaalamu sana na mambo yamodem lakini trough kusoma kuna teknolojia mbili CDMA( Kwa jina lingine EVDO) na GSM. kwa hiyo modem uliyonayo itakuwa imetengenzwa a ku accomodate technology moja either iwe GSM au CDMA.

  Inakuja Issue nyingi inabidi ujue ISP or provider wako anatoa huduma yake ya Internye kutumia Teknolojia gani. Mfano kama Voda wana provide internet kwa Teknolojia ya GSM basi ukiwa na modem ya CDMA hata ikiwa unlocked huwzi kuitumia. Hivyo Hivyo kama TTCL wanatumia Teknolojia ya EVDO pekee basi hata ukiwa na modem ya GSM huwezi kuitumia kwa huduma za TTCL

  Ni sawa uwe na computer kali ya MAC lakini una software kali za Windows.. Huwezi kuistall application zako za windows kwenye kompyuta ya MAC.

  So usidhani modem ikiwa unlocked utaweza kuhama hama freely tu .Yote itategema na aina ya modem ya Aina ya teknologya Service provider anatumia.

  Home work yako

   
 5. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ndio maana nilikuuliza kama nilikuelewa!, ulipo oengelea highlife 2gb bundle weekly subscribtion hii mkuu lazima uwe na modem ya Zantel, elewa zantel anatoa huduma ya internet kwa (gsm) na (cdma) highlife internet hii lazima uwe na cdma modem. Ama highlife kwa ajili ya kupiga simu labda uwe unapiga simu za nje ndio utafaidika. Mimi mwemyewe nimejiunga hihlife na natumia modem ya zantel.
   
 6. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Asante mkuu kwa ushauri. Umenifumbua macho sasa.
   
Loading...