Nawezaje kutumia akili iliyonipa matokeo darasani kutoka kimaisha?

Malingumu

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
616
429
Nawasalimu ndugu wapendwa tunaopendana kupitia JF yetu.

Binafsi huwa najiuliza na kuona kuwa kuna utofauti kati ya akili ya darasani na akili ya maisha. Najichukulia mfano: darasani nilikuwa smart sana yani wakati fulani nilikuwa natatua mafumbo ya walimu hata mi mwenyewe nilikuwa nashangaa na nilipokuwa najilinganisha na watu wengine ambao walikuwa wanafeli kile ambacho mi nilikuwa nafaulu nilikuwa nakosa majibu.

Ila kwa sasa nimeingia mtaani na naona kama akili ya kule darasani na ya huku kuna utofauti. Yani namna ambayo unaweza kupenya kifedha na kufanikiwa kimaisha kwa ujumla. Sijajua labda huenda sijakaa karibu na pipe za mafanikio ila huwa najiuliza kuwa nawezaje kutumia akili ya darasani kufanikiwa kimaisha? Nikafikiria labda huenda waliotutangulia (developed Countries) watakuwa wamegundua kijifaa cha ku-convert (Converter ya akili). hahaa may be!!!

Bado najaribu kuwaza nawezaje kutumia akili yangu ambayo ilinipa matokeo mazuri shuleni kufanikiwa kimaisha.

Any idea..!!??
 
ni ngumu sana kua na akili ya mtaani maana vitu vya kijinga jinga ndo vinavyowatoa watu, mtu mwenye akili ya darSani hawezi fanya vitu vya kijinga jinga....mwwnye akili za darasani hua anawwza kua mfanyakazi mzuri sana maana yeye hu avoid kukosea vitu...
 
Akili za darasani ni kwaajili ya kumuandaa mtu kutumiwa na mwenye akili ya mtaani nishida sana ukachomoka kimaisha kwa kutumia akili za darasani
 
Back
Top Bottom