Nawezaje Kusupply Vitabu vyangu Vya English Grammar?

Jojo123

JF-Expert Member
Jan 31, 2013
432
694
Waandishi wa Vitabu naombeni Mnielekeze

Nimeandika kitabu cha English Grammar kwa kushirikiana na Maprofessor wa will wa lugha hapo UDSM na Phd holder flan wa chuo cha Havard ambaye nilimuomba akipitie kukiboresha zaidi alipo kifanyia marekebisho duh..ata mm ikabidi nijifunze upya. So kitabu kipo kwenye softcopy.. Nimesha tafuta Kiwanda cha kukiprint

Ila naombeni waandishi wanipe ABC ya mchakato je Naanzia wapi kusupply? na je njia bora zaidi ya kumake follow up ili mapato yake yasivuje huwa mnafanyaje?

Vipi kihusu copyright?

Je, bei ya soko kwa sasa kwa kitabu cha A5 chenye page 56-60 kina kuwa kinauzika kwa bei gani na printing yake inachezea bei gani.

Je, supply point zinakuwa na Makubaliano gani? je mnasupply bookshop kwa mali kauli au mna wauzia kwa prepaid?

Naombeni Ujuzi wote muhimu kwa wanao jua.. nategema kukichapisha Kabla ya mwezi wa3 kuisha kiwe sokoni.

Nimetafuta Amazon wakaniambi ni weke Copyrigt page, Kuwe na ISBN code, kuwe na Tittle Page.. hivyo nikabaki najiuliza napataje hivi vitu ili Amazon wakubali kuniuzia uko duniani.

Mwenye anajua pakupata hivi vitu ajisaidie ujuzi na maelekezo.

Asanteni
 
Hongera kwa kuandika kitabu; ^umejitoa nje mmoja^ (^you've singled out yourself^) kuwa miongoni mwa wachache wanaothubutu haswa.
 
Hongera kwa kuandika kitabu; ^umejitoa nje mmoja^ (^you've singled out yourself^) kuwa miongoni mwa wachache wanaothubutu haswa.
Asante sana Bro.. Ila ni ngumu sana but i hope na mm nitaacha footprint kwa vizazi kunafaika na elimu yangu
 
vitabu vya mafunzo mara nyingi hua vinachapishwa ma taasisi ya elimu, kama unataka kukifanya kiwe cha biashara inabidi uonane na wachapishaji binafsi mf : Mkuki n.k. Wachapishaji ndio husambaza vitabu kwa hapa kwetu, wao ndio wanajua masoko yalipo.
 
Asante kwa jibu bro! Je hao mkuki na nyota ni private company au nao ni Taasisi ya Kielimu?

Je kwa uzoefu wako.. makubaliano yao yanakuwaje kati yao na mwandishi ili nijue najipangaje wasije nizidi akili wakani lalia kwa mgawanyo.. asante
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom