Nawezaje kushusha hatari ya kupata ujauzito wenye matatizo au Mtoto Njiti?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Unastahili matunzo, mapenzi na uangalizi sawa na ya mtoto wako tarajiwa. Huduma hizi zitakusaidia kudhibiti matatizo ya afya unayoweza kuwa nayo na kukukinga dhidi ya kisukari cha ujauzito pamoja na shinikizo la damu la juu. Kadri utakavyokuwa na afya njema ndivyo atakavyokuwa na mwanao.

Usije ukapuuzia miadi na madaktari wengine kama una tatizo la kitabibu la kudumu kama kisukari au au shinikizo la damu la juu. Kamwe usisahau ratiba ya miadi ya magonjwa yako ya kudumu. Kumbuka kushughulikia magonjwa yako ya kudumu kabla ya kupata ujauzito kutasaidia kukuweka wewe na mwanao katika siha njema na kuepuka maudhi yanayowaandama wajawazito wengi.

Kumbuka kumtembelea dakatri wako wa meno kwa ajili ya uchunguzi
Kuwa meno na fizi zenye afya hupunguza uwezekano wa kujifungua kabla ya wakati pia hupunguza uwezekano wa kupata watoto njiti.

Dumisha lishe bora na iliyo na uwiano mzuri
Kula vyakula vya aina tofauti tofauti kutakusaidia kupata virutubisho vyote unavyohitaji. Kila siku tumia mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali, nafaka kamili (unga usiokobolewa, n.k.), maharage, pamoja na maziwa machundu ikiwa ni pamoja na vayakula vingine vilivyo na ukwasi mwingi wa madini ya kalisi (calcium). Kwa njia hiyo utaweza kudumisha afya ya meno na mifupa yako mwenyewe na kumsaidia mwanao kuendelea kukua kwa afya njema.

Pia usisahau kujumuisha vyakula kama vile mboga za majani, maharage makavu, maini na baadhi ya matunda ya jamii ya sitrusi kama vile machungwa, ndimu na n.k. kwani hivi vina kiwango kizuri cha madini ya foliki.

Kuwa na kiwango cha uzito kinachotakiwa
Ongea na daktari wako kujua ni kiasi cha gani cha uzito kinachohitajika katika kipindi hiki cha ujauzito. Wanawake wenye BMI ya kawaida wanatakiwa kuongeza uzito wa kilogramu 1 mpaka 15. Kama tayari ulikuwa na uzito mkubwa kabla ya kuwa mjamzito daktari wako anaweza kupendekeza uongeze kati ya kilogramu 6 na 11. Kuwa na uzito muafaka kutakusaidia kupunguza uwezekano wa kupata mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati. Pia utapunguza hatari ya kupata kisukari katika kipindi cha ujauzito au shinikizo la damu la juu la kipindi cha ujauzito.

Fanya mazoezi ya mara kwa mara
Mazoezi ya mara kwa mara yatakusaidia kuwa na uzito muafaka katika kipindi hiki cha ujauzito. Kufanya mazoezi huku kutakupatia nguvu na kukuepusha na msongo. Kumbuka wewe na daktari wako katika kipindi hiki mnaweza kupitia upya programu yako ya mazoezi. Kuna uwezekano mkubwa unaweza ukaendelea mazoezi mengi tu kama unatakavyoshauriwa na daktari. Daktari wako atakusaidia ni mazoezi gani utaendelea nayo na mazoezi gani unahitaji kupunguza, n.k.

Sitisha kuvuta sigara au kutumia kileo
Hutakiwi kuvuta sigara au kutumia kileo katika kipindi chote cha ujauzito. Matumizi ya pombe yatamuweka mwanao katika hatari ya kupata hitilafu katika akili na katika viungo vya mwili. Uvutaji wa sigara nao huongeza uwezekano wa kujifungua mtoto mwenye uzito pungufu ambalo ni tatizo linalowakumba zaidi wajawazito watu wazima (miaka 35 na zaid). Kutokuvuta sigara kunasaidia kukukinga na prieklampsia (hali inayopelekea kupata kifafa cha mimba).

Muulize daktari wako kuhusu dawa unazohitaji kutumia wakati wa ujauzito iwapo ulikuwa unavuta sigara kabla ya ujauzito. Muulize dakatari wako kuhusu ni dawa gani zilizo salama kutumia ukiwa unanyonyesha ili kumjengea mtoto wako kinga. Mweleze daktari historia ya dawa ulizotumia ulizoandikiwa na daktarai na hata zile unazotumia bila ya kuandikiwa na dakatari, virutubisho na dawa za miti shamba. Ajue namna ya kukusaidia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom