Nawezaje Kusafirisha vitu vya ndani mkoa kwa mkoa

simon2016

JF-Expert Member
Oct 19, 2020
593
1,669
Kwa wale mlioweza kusafirisha vitu kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine naomba ushauri mliwezaje?

Kama kuna kampuni unaijua au inajishugulisha na kusafirisha vitu(furniture kitanda,sofa,kabati show case n.k) vya ndani kwa bei nafuu kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine tuwasiliane njoo inbox tuyajenge.

Nataka kutoa vitu dodoma kwenda iringa mjini.
 
Vitu vya ndani? Maini, figo, firigisi nk ... Ok

Natania tu mkuu, kuna makampuni unaweza kuwapa hiyo kazi ndo mishe zao hizo
 
Kwa wale mlioweza kusafirisha vitu kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine naomba ushauri mliwezaje?

Kama kuna kampuni unaijua au inajishugulisha na kusafirisha vitu vya ndani kwa bei nafuu kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine tuwasiliane njoo inbox tuyajenge.

Nataka kutoa vitu dodoma kwenda iringa mjini.
Nenda pale iringa road uwe una simamisha malori ongea nao lakini hakikisha mizigo yako ipo tayari.
 
Kwa wale mlioweza kusafirisha vitu kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine naomba ushauri mliwezaje?

Kama kuna kampuni unaijua au inajishugulisha na kusafirisha vitu vya ndani kwa bei nafuu kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine tuwasiliane njoo inbox tuyajenge.

Nataka kutoa vitu dodoma kwenda iringa mjini.
Mkuu Dodoma kuja Iringa Kuna magari mengi Sana. Kuna magari yanatoka kupeleka mbao mikoani, Kuna magari yanafuata mkaa wa mawe n.k yanakuja tupu.
Ukifikisha mzigo wako pale maghorofani unapata usafiri hata usiku.
 
Makampuni yatakupiga kama upo Dodoma we nenda pale nje ya uwanja wa mpira Jamuhuri ulizia gari inayoenda Iringa ongea na dereva maana utasafirisha kwa bei ndogo huwezi amini
 
Kama una vitu vilivyotengenezwa kwa mbao (Mazao ya misitu),Usidhubutu kukutana na wale jamaa wa misitu,
Bora uuze ukanunue iringa tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom