Nawezaje kupokea hela kutoka nje ya nchi bila kuwa na akaunti ya Benki?

Baby Nimah

JF-Expert Member
Oct 31, 2018
700
745
Hey guys ! I hope mko powa,mm sipo pow sana afya yangu inamgogoro kidogo God is good all the time nitakaa sawa

Nina rafiki yangu yupo UK alikuwa anataka kunitumia pesa kidogo akaniuliza una account ya bank nikamwambia sina,akaniuliza kama kuna namna nyingine ya kutuma,

Jf kuna wa somi wengi na wajuzi wa mambo naombeni msaada wenu,natanguliza shukrani karibuni

😍Nikiipata hiyo hela nitawakumbuka jamani🤗
 
Western Union money transfer atumie. Ama muombe mtu akaunti unayemuamini atume kwa akaunti yake,
Pia Kuna namna Fulani kwa mpesa unapokea hela. Mie Kuna mdada ameshanitumiaga Kama tumilioni kadhaa kwa simu ikaja kwa mpesa tokea USA mkuu. So fight bana upate hizo hela
 
Kwa

Kwa TIGO pesa inawezekana?
Maana yy mwenyew mshamba kama mm
 
Hey guys ! I hope mko powa,mm sipo pow sana afya yangu inamgogoro kidogo God is good all the time nitakaa sawa

Nina rafiki yangu yupo UK alikuwa anataka kunitumia pesa kidogo akaniuliza una account ya bank nikamwambia sina,akaniuliza kama kuna namna nyingine ya kutuma,

Jf kuna wa somi wengi na wajuzi wa mambo naombeni msaada wenu,natanguliza shukrani karibuni
Tumia Western Union.

Hakikisha una kitambulisho kinachotambulika na unampa majina yako kama yalivyo kwenye kitambulisho. Na yeye akishatuma pesa atakutumia namba ya siri na swali na jibu.
 
Naona now mobile inafanya vizuri I recommend M-PESA
Tanzania kwa uzoefu wangu naona WU imekaa vizuri
 
Tumia Western Union.

Hakikisha una kitambulisho kinachotambulika na unampa majina yako kama yalivyo kwenye kitambulisho. Na yeye akishatuma pesa atakutumia namba ya siri na swali na jibu.
Si lazima swali na jibu ila kama ulivyosema ahakiki jina lake ni sahihi kwenye ID na MTCN
 
Hapana navyojua ni mpesa pia kumbuka wao voda wametangulia kwanza. Afu wewe uko dar Nini Mana dar mwapenda Sana tigo.
Njia ya fasta tu aende Western Union yaani akituma tu unaenda kwa ofisi zao inachukua popote hapa tz. Ila awe na document za kumtambulisha. Mana mie wkaati natuma tokea rashia kuja mza lazima kitambulisho wanakuomba. Pia swali utakalo jibu Kama paswedi akiweka pound zake kadhaa wewe huku unapokea Tzs jamani. Changamkia update hela hiyo la sivyo ataweza ahairisha ama akapata dharura akaifanyia kazi wewe ukabaki kusubiria wakati mwingine
 
Mwambie a-download app ya WorldRermit. Humo anaweza kukutumia fedha kwenye mtandao wowote wa simu hapo Tanzania.
 
Tigo pesa kwa WorldRemit ni faster unapokea dakika tu
Ila mpe namba na wewe hakikisha una kitambulisho chako
 
Western Union money transfer atumie. Ama muombe mtu akaunti unayemuamini atume kwa akaunti yake,
Pia Kuna namna Fulani kwa mpesa unapokea hela. Mie Kuna mdada ameshanitumiaga Kama tumilioni kadhaa kwa simu ikaja kwa mpesa tokea USA mkuu. So fight bana upate hizo hela
Akishazipata, usisahau kunijlisha
 
Naomba niboreshe kuhusu Western Union.

Jamaa wa UK atatuma pesa kwa kujaza fomu ambayo itaonesha majina ya mtumiwaji.

Pia, atajaza neno la siri, mfano "favoutite colour" "Green". Hili neno la siri atamtumia mtumiwaji kwa njia anayoona inafaa yenye usiri.

Mtumiwaji ataenda kwenye tawi la wetern union (mara nyingi nayaona kwenye Benki ya Posta), atajaza fomu ambayo ina vipengele mfano jina la mtumiwaji, na neno la siri ambalo jamaa alimtumia.

Mhudumu atalinganisha taarifa anazoziona kwenye kompyuta, bila kusahau taarifa za kitambulisho mfano NIDA, mpiga kura nk. Kama zinafanana anapata hela yake.
 
Back
Top Bottom