Nawezaje kupata kibali kutoka SUMATRA kuhusu Biashara ya usafilishaji?

Youngstunna

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
261
295
Habari wakuu,

Poleni na majukumu na pia niwatakieni kheri ya mwaka mpya. Shida yangu ni moja naomba anaye jua utaratibu wa kupata kibali kutoka kwa SUMATRA kupata ruti ya kusafirisha abiria toka eneo moja kwenda jingine upoje, nina gari Toyota hiace nataka ipige route za Dar - Chalinze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dar - Chalinze itakulipa kweli kwa gari aina ya Toyota Hiace! Maana hiyo barabara imejaa gari nyingi zenye nafasi ndani mfano Coaster za Dar Msata, Dar Moro, nk.

Ungeitafutia route za ndani ndani mfano Mbezi Mwisho - Mloganzila Hospital, nk ingekuletea hesabu nzuri bila shaka. Ila Dar Chalinze! Hiyo ina ushindani sana kwa mtazamo wangu.
 
Tate Mkuu, Umempa ushauri mzuri na wa kweli.
Na huko chalinze hata Mimi huwa naendaga Kuna gari nyingi Sana yaani mtu anayekwenda chalinze gari za morogoro atapanda,za msata atapanda,za miono atapanda,na Bado Kuna Noah nyingi tu nazo zinapiga mzigo kwa hiyo ujazaji wao ni wa foleni pale mbezi mwisho ukienda unakutana na coaster karibu kumi na kila coaster moja ili ijaze ni karibu masaa 2 ndio iondoke.
Kuna ruti mpya Kama za Ubungo mloganzila,Makumbusho-Goba-Mbezi.
Ukikosa hizo hata Makumbusho-Bunju Ina abiria muda wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Youngstunna,
Hongera sana kwa kuanza na wazo chanja mwaka 2020. Nakushauri iwapo una nafasi ama msimamizi mzuri, nenda morogoro Sumatra ukate route ya Ifakara - Malinyi ina biashara nzuri kwa hiace
 
Back
Top Bottom