Nawezaje kuirudisha meseji nilitotuma kwenye yahoo messenger !! ndoa iko hatarini!

green29

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
311
41
wazee nimetuma message ya nyumba ndogo kwa wife kwa bahati mbaya. Nilikuwa nachati nao wote kupitia yahoo messenger sasa nikajikuta namtumia msg wife badala ya nyumba ndogo. wife alisha log out nahisi bado hajaisoma , nataka kujua kama naweza kuivuta ili asiikute.

bahati mbaya nilikuwa namkumbusha nyumba ndogo good time tuliyokuwa nayo wakati wa mwaka mpya huko zanzibar wakati wife anajua nilikuwa kigoma kikazi.

nisaidieni tuokoe hii ndoa changa washikaji
 
Kazi unayo.

Unanikumbusha tamthiliya moja ya Kiswahili shule ya sekondari, nafikiri ilikuwa inaitwa "Halahala" jamaa alituma barua ya mke kwa nyumba ndogo na vice versa.

Kimaadili hata kama kungekuwa na njia ya kukusaidia waungwana wangejisikia uzito.Lakini kwa jinsi ninavyofahamu, ukiondoa kuingia katika messenger yake kwa password yake na kuifuta sijui kama kuna njia.

Zaidi ya hapo nachoweza hapo ni kuleta uzushi wa kisaikolojia na kujifanya kama Shaggy katika "It wasn't me". Kwamba kuna kidudumtu kaingia kwenye messenger yako anataka kuwaharibia mambo.

Lakini mimi ningekushauri umuangukie na uachane na mambo ya nyumba ndogo, ukweli ndiyo dawa ya yote.

Ona

http://answers.yahoo.com/question/index?qid=20070602232858AAcagtd
 
Pole Green29,

Hizi ndo thawabu za nyumba ya pembeni- ina maana mama hatoshelezi? Au amennenepa na manyama ya mwili mengi sana nini?
 
Kana-ka-Sungu sijui yuko wapi leo... naona angepata suluhisho... ha ha.

The bottom line ni kuwa: siku za mwizi ni arobaini. Pole kwa yatakayo kusibu bwana Green29.

Pundit, hata Shaggy ana admit mwishoni mwa wimbo kuwa kufanya hivyo si vyema, 'it wan't me' inasaidia lakini siyo dawa. Kama ulivyosema, pengine ukweli utakuwa wa maana... ilaaa... mmmmh, sijui kwa kweli, demu mwenyewe kama anakuwa anajua mambo ya internet kisawasawa, sidhani kama ataweza kuongopewa..

oooh, kuna kitu kimenijia kichwani, subiri ni ku pm... it's evil though.. lol

Ule wimbo wa Messenger kaleta balaa, unafaa kweli kupigwa hivi sasa, nimeutafuta kwenye youtube siuuoni..... lol
 
heheheeee unalo hilo muzeee!!1haya sasa tafuta namna ya kumwangukia mkeo hata nakwa mshenga wako na kila kitu muzee as wanawake wa sas...mwee ngumi mkononi...mie natanguliza pole zangu
 
Patamu hapo, ila pole mkuu,
Ila naamini Mungu kaamua kukupiga kofi kwa tabia unayo mfanyia mwenzio! tena ndoa yenyewe changa?? mkuu tafadhali...
 
Pole sana bosi.
Shida moja ni kwamba meseji ikishaondoka katika Pc yako hiyo siyo yako tena.
Naungana na wachangiaji wengine kwamba muombe mkeo radhi kwa uzinzi huo.
Kila la kheri!
 
GREEN 29, kudadadeki!!!Akha!! Kumbe wanaume ndivyo munavyotuchezea akina mama. Yaani unachati na kimada na wakati huo huo wachati na mkeo!!! Yaani ningekuwa na namba ya simu ya mkeo ningempigia muda huu na kumpa breef ya haya yote na kumjaza upepo kinoma halafu namshawishi aende kwenye internet akasome na kuprint hiyo message. Vile vile ningemshauri akunyime UNYUMBA mpaka hapo mafisadi wa BOT au Balali atapokamatwa!!! Ushauri wanngu wa bure, GRRN 29 acha vimada utakufa, kuna UKIMWI na Liyumba katembea na karibu dogo dogo zote zinazowavutia nyie mabraza men. Mungu akubariki!
 
Mwambie mkeo kuwa uliiacha simu mezani na kuna mtu aliichukua kwa muda bila wewe kujua akaitumia kutaka kukuvunjia nyumba yako.Mwabie si unajua tena watu hawapendi maendeleo ya mtu bwana? Halafu leo uongeze ufundi zaidi utakapokuwa nae faragha basi utakuwa umemmaliza.

Lakini bwana acha haya mambo.Sisi bado tunakuhitaji nadani ya Jamboforum.Tutakusahau sasa hivi usiendekeze haya mambo.Yaliyopita yamepita thamini ulichonacho ndani.Mkeo simjui lakini naamini ni mzuri kuliko huyo uliyempelekea meseji na ndio maana mawazo yamekuelekeza mesaji iende kwake badala ya huyo hawara.MUNGU NI MKUBWA si umeona amebadilisha mawazo na meseji ikaenda kwa mwandani wako?
 
Pole sana mkuu!

Acha uasherati, Mungu hapendi kabisaaa...

Kabala hata mkeo hafungua email na kuisoma,mpigie simu umuombe msamaha, ila hiyo tabia uache ndoa yenyewe bado changa GREEN 29 unakuwaje wewe?
 
Ningeweza kukufundisha Uongoa ila utakuwaa ujinga nafikiri mawazo ya wandewa yanajitosheleza sana. Sio mbaya ukimuangukia na kuomba msaamaha.
 
Pole ndugu green29, ila kwa ushauri wangu jaribu yafuatayo; mwambie wife kuna jamaa yako ulimpa email yako na yake(wife) hivyo ametuma msg (very urgent)lakini kupitia email ya wife, mwombe akutumie password yake ili uweze soma hiyo msg. Huo ndo ushauri wangu.
 
Pole mkuu, hope umeshapata solution tayari na labda zile arobaini hazijatimia bado.
ila kama utasave/umesave hili zali kuwa makini next time!
 
Pole ndugu green29, ila kwa ushauri wangu jaribu yafuatayo; mwambie wife kuna jamaa yako ulimpa email yako na yake(wife) hivyo ametuma msg (very urgent)lakini kupitia email ya wife, mwombe akutumie password yake ili uweze soma hiyo msg. Huo ndo ushauri wangu.

kjon, mbona unamdanganya mwenzio, hapo hakuna cha email ilienda kushoto au kulia. Chamsingi kwa Green29 ni kumuomba mkewe msamaha na kuachana na tabia ya nyumba ndogo. Ithink mke wa green29 ni mzuri thats why aliamua kufunga nae ndoa. Na wewe kama unatabia hiyo please acha na hii ni kwenu wanaJumboforum wote wa kiume (mlio-oa) acheni tabia ya kuwa na vimada, Mungu hapendi
 
'ALWAYS LIES HAVE SHORT LEGS' BORA UMEPELEKA MESAGE BADALA YA VIRUSI. HUO NI UUUNGWANA KWELI?? KUMDANGANYA MKEO KUWA UKO KIGOMA KUMBE UKO ZANZIBAR EEEEHH NI UUUNGWANA HUO? WACHA TABIA HIYO CHAFU. NI FUNDISHO KUWA DONT DO IT? HAPA USITEMEE HURUMA. NDIYO NYIE MNAOSAMBAZA VIRUSI KWA KUTOKIUWA WAAMINIFU. JAMANI HAMKOMI NA TABIA CHAFU. HATA HUONI AIBU UNALETA UFYONZO HUO HAPA ARE u SERIOUS?? WACHA UFISADI WA MAPENZI MHESHIMIWA. KAUNGAME NA UKOME NA TABIA HIYO. I AM SORY KAMA NIMEKUWA MKALI KIASI HICHO.
 
inawezekana kama wife hajaifungua
fanya hivi

1.Mwambie kompyuta yako ina virus, kila mtu kwenye id mesenger yako kapata same mesege, hizo mesege zinajituma zenyewe, na uwezi format system

2.Jaribu kumwabia wife kuwa ID yako iko hacked,sasa unamuomba kutumia email yake kuwataarifu yahoo, hivyo muombe akupe password akikupa tuu kosa la jinai.

3.Kama nyumbani kwako kuna internet, na wife yupo home basi mtege, chomoa cable ya net, then mwambie alog in ukiwa ofisini kesho mchati akishindwa mwambie akutumie email na password ujaribu ofisini kwako kama inafanya kazi.

4.Kama ikishindikana yote hayo badili email id!, Mwambie umepoteza password jana baada ya kuchati nae na hivyo basi umefungua id mpya, kama akikuta meseje yoyote mwambie haijatoka kwako mostyl kwa hackers

Ukishindwa yote hayo basi kubali yaishe
 
Sasa kama ndoa ni changa haya nyumba ndogo ulianza lini?

Vitu vingine hata kusaidia ni ngumu kwa kweli, nadhani hapa ndio unaapply ile methali ya "za mwizi...."
 
Haya majibu ndugu yangu yatakupoteza zaidi na yote yatakuwa muafaka kutemeana na kiwango cha uelewa wa mkeo Bro! Hivi utanieleza nini nikupe password yangu? Hiyo itakuwa tena password. Wewe yako anayo? Unajua tatizo hapa jamaa wana under estimate viwango vya wake zao/za wenzao, kina mama wengi they are very good with technology siku hizi.

Kaka jipange tu na usubiri mtihani wala usiandae majibu maana hujauona. Ikibidi omba msamaha km maswali na ukali wake utamfanya ajilengesha kwa hili kuokoa ndoa yako toa uongo kulingana na lile atakalokuwa kapata au kauliza. Lakini tabia hii pia iwe fundisho. if you have to do what you do then be more careful!!!! Si unajua hata vibaka huwa wanapiga na kuua vibaka wenzao wanapokamatwa? Utauwawa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom