Naweza kuunganisha king'amuzi kimoja TV tofauti?

mwenye shamba

JF-Expert Member
May 31, 2015
962
1,604
Habari wapendwa,

Napenda kujua namna ya kutumia dishi na king'amuzi kimoja ili kisambaze channel katika tv tofauti.
Nataka kila chumba kiweze kupata channel lakini ninadish moja.

Kwa anayefahamu naomba anielekeze namna ya kufanya hatua kwa hatua.

Asante.
 
Vipi inawezekana kutumia dish LA startimes kwenye king'amuzi cha azam?
Ndio inawezekana..mimi ninaking'amuzi cha Azam na dishi lake..sasa dishi liliyumba kama mara mbili ivi fundi akanambia ili nisahau maswala yakuyumba yumba nitafute kadish kastar times hako ukiweka umeweka japo toka anirekebishie kwamara yamwisho halijayumba tena konami nikapotezea kutafuta tena dish la startimes
 
Asante sana kaka
 
Inawezekana kwa namna mbili:

1. Kama una dish moja na king'amuzi kimoja, basi utahitaji kifaa chenye 1 input ya HDMI, na 2 outputs. Kwa maana utachomeka hicho kifaa kwenye king'amuzi chako, alaf kwenye zile 2 outputs utachomeka 2 HDMI cables ambazo zote zitaenda kwenye Tv mbili tofautu.

Ubaya wa hii ni kwamba, tv zote zitaonesha channel moja, maana king'amuzi ni kimoja.

2. Unakuwa na dish moja, ila ving'amuzi vinakuwa zaidi ( mfano viwili au vitatu). Hapa utahitaji T-connector. Let say unaving'amuzi viwili. Ule waya unaotoka kwenye dish mpaka ndani, ukifika ndani connect kwenye port moja ya ile T-connector, alaf katika zile port 2 zinazobaki, unaunganisha tena waya zingine kama ule uliotoka kwenye dish, alaf kila waya unaupeleka kwenye king'amuzi. Hapa kila tv utaona channel unayotaka.

Njia hii ya pili unaweza kuitumia kwa pia kuunganisha nyaya toka madishi tofauti, alaf ndani ya nyumba ukaingia waya mmoja tu ambao utaweza kuutumia kwenye ving'amuzi vyote.
 
Habari wapendwa,
Napenda kujua namna ya kutumia dishi na king'amuzi kimoja ili kisambaze channel katika tv tofauti.
Nataka kila chumba kiweze kupata channel lakini ninadish moja.
Kwa anayefahamu naomba anielekeze namna ya kufanya hatua kwa hatua.
Asante I.
Kutumia dishi 1 na kingamuzi kimoja kwa TV 2 tofauti, basi unahitaji kutumia output tofauti kwa kila tv kutoka kwenye kingamuzi. Kwa mfano: utatumia HDMI kwaajili ya TV ya kwanza halafu utatumia AV kwaajili ya TV ya pili . Lakini mtakuwa mnaangalia chaneli moja wote kwa wakati mmoja.

Kutumia DISHI 1 na Dikoda 2 kwa TV 2,
Ukitumia T-connector /splitter mtakuwa pia mnaangalia channel moja kwa wakati mmoja kwasababu LNBF ni moja.

Kutumia DISHI 1 na Dikoda 2 kwa TV 2,
Ukitumia TWIN LNBF, kila mmoja atakuwa anatumia TV kwa uhuru wake, Kila mtu anaweza kuangalia channel anayotaka wakati wowote. Hii ni sawa na kila mtu kuwa na dish lake.

Wataalamu watakupa mbinu zingine....
 
Kwa hiyo ving'amzi vyote vitalipiwa?
 
Inawezekana moja tumia Av na nyingine tumia hdmi kama ni machogo tafuta connecter one in two. Ila channel utabadilisha kwa sourge yaani kwa dicoda
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom