Naweza kusema haya ni Maamuzi sahihi? Au ni mapenzi ya kweli kwa mpenzi?

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,565
Nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari ITV jana na juzi, nikakutana na habari hii ...

Kuna boat moja ilizama, I think Kenya, juzi; ilikuwa imebeba watu wa kutosha. Ndugu mmoja ambaye alinusurika kwenye hiyo ajali alikuwa na familia yake ya mke na watoto watatu. Alisema yeye alichofanya ni kujiokoa yeye kwanza na halafu akamuokoa na mke wake.
Watoto wake wawili waliokolewa baadaye na watu wengine. Huyo mmoja haikujulikana status yake.

Swali: Ingekuwa wewe kwenye hatari ya tukio hili la kweli ungemuokoa mke/mpenzi au watoto? Unafikiri alifanya maamuzi sahihi? tunaweza kuyaita haya ni mapenzi ya kweli kutoka kwa mume kwenda kwa mke?

Tusaidiane mawazo.

Wenu,

HorsePower
 
Yeyote aliye karibu ndiye ningemuokoa kwanza, pia ningefanya juhudi kuwaokooa wengine waliobaki. Sababu wote ninawapenda watoto na mume.
 
Hatari haina formula
Kuna wengine akiingia mwizi ndani wanapigana
Kuna akina yakhe hapa akiingia mwizi ndani tunazimia hadi anapata kazi ya kukupepea ili umuoneshe pesa ziko wapi.

Kwa alichikifanya ni kizuri maana aliokoa maisha.
 
I was trying to think kipuuzi kabisa, kuwa ukiokoa mke, unaweza kuzaa watoto wengine, ila ukiokoa watoto huwezi kupata mke kama yule ...
na pia baada ya tukio waweza kujikuta umejenga upendo wa kweli ndani ya nyumba ....
 
Sahihi yake sio lazima iwe yangu kwasababu priority zetu hazifanani.

Binafsi ningeokoa mtoto/watoto wangu.
 
hapo ni kumshukuru mungu kwa yote yaliyo tokea sidhani kama jamaa alipenda kuwaacha watoto wafe,na hakuwa na uwezo wa kuwasaidia wote kwa wakati mmoja.
 
ajari wala haikualert kuwa mnaenda kupata ajari.
cha msingi okoa yeyote yule aliye karibu wako ukiona una uwezo wa kufanya ivyoo, ss kama ni mkeo haya , watoto haya , jirani haya.
 
Hatari haina formula
Kuna wengine akiingia mwizi ndani wanapigana
Kuna akina yakhe hapa akiingia mwizi ndani tunazimia hadi anapata kazi ya kukupepea ili umuoneshe pesa ziko wapi.

Kwa alichikifanya ni kizuri maana aliokoa maisha.

Pole sana kama hali ndo hiyo, ngoja nikushauri kidogo. Siku nyingine mwizi akiingia ndani, ukizimia hata kama utasituka vunga tu kwamba bado umezimia, ikifika asubuhi atasepa mwenyewe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom