Naweza kupata hati ya kusafiria kwenye banda la Uhamiaji katika maonyesho ya sabasaba?

nyamalagala

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
743
1,000
Natumai wanajukwaa mnaendelea na majukumu ya kujitafutia riziki.

Naomba mwenye kufahamu kama naweza kupata hati ya kusafiria katika maonesho ya sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya maonyesho katika banda la maonyesho la idara ya Uhamiaji.

Nategemea kuhudhuria kongamano la kimasomo la CHAWAKAMA litakalofanyika nje ya Tanzania. Kutokana na ratiba ya kukaa huku DSM inaelekea kuisha sasa nilitaka nikamilishe taratibu zote niipate hati hiyo mapema.

Naomba kujua kama nikienda kesho kwenye banda lao ninaweza kupatiwa. Ikumbukwe kuwa nimeshajaza fomu ya maombi na nimeshapata Baraka zote na mahakama lakini tatizo kwangu ni muda wa kwenda ofisini kwao kwani niko kwenye UE na nilitaka niitumie siku ya tarehe 7/7 kujongea huko.

Naomba kama kuna mwenye kujua hili anisaidie.

Natanguliza shukrani.
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
36,418
2,000
Ngoja waje,

Mimi nilienda jumapili iliyopita nilikuwa na lengo hilo lakini sikufanikiwa kulipata hilo banda la uhamiaji, nikijaribu kuzurura sehemu zote.

Muda bado upo kama lipo tutajuzwa
 

nyamalagala

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
743
1,000
Ngoja waje,

Mimi nilienda jumapili iliyopita nilikuwa na lengo hilo lakini sikufanikiwa kulipata hilo banda la uhamiaji, nikijaribu kuzurura sehemu zote.

Muda bado upo kama lipo tutajuzwa
Nawasubiri sana kwa hamu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom