Naweza kufungua kiwanda kidogo cha unga wa sembe bila kibali kutoka TBS na TFDA?

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
4,467
10,993
Wakubwa zangu nina wazo la kuanzisha kiwanda kidogo cha unga wa sembe ila kitu ambacho mpaka sasa kinanipa changamoto ni juu ya hawa watu TBS na TFDA.

Je, naweza fanya uzalishaji bila kibali toka kwao?

Na kama kibali ni lazima utaratibu uko vipi na gharama zake kwa wajasiriamali wadogo.

Pia lazima wote wawili wahusike au unaweza thibitishwa na mmoja ukaendelea na kazi.

NB: Nimesoma michango mingi sana kuhusu hii biashara nimejifunza vitu vingi sana ila kwa hao jamaa nilikosa taarifa sahihi. Msaada kwa wazoefu.

El perdedo
 
Ni kosa kufanya biashara bila kuwa na kibali kutoka:

1. Regulatory Authorities
2. Kujisali na kupata TIN na kuleta makadirio yako ya biashara kwa Kaisari
 
Wakubwa zangu nina wazo la kuanzisha kiwanda kidogo cha unga wa sembe ila kitu ambacho mpaka sasa kinanipa changamoto ni juu ya hawa watu TBS na TFDA.

Je,naweza fanya uzalishaji bila kibali toka kwao?

Na kama kibali ni lazima utaratibu uko vipi na gharama zake kwa wajasiriamali wadogo.

Pia lazima wote wawili wahusike au unaweza thibitishwa na mmoja ukaendelea na kazi.

NB:Nimesoma michango mingi sana kuhusu hii biashara nimejifunza vitu vingi sana ila kwa hao jamaa nilikosa taarifa sahihi.Msaada kwa wazoefu .

El perdedo
Usiite kiwanda utajicomplicate mpaka ushindwe.

Anzisha mashine ya kusaga, paki unga uza.

Utahitaji:

Vibali utahitaji Fire, Leseni ya biashara na Brela kwa kuanzia.

Hao TBS, TMDA weka pembeni kwanza.
 
Serikali ya Samia ni wakati muafaka sasa kuirudisha TFDA maana TBS imeshindwa kusimamia masuala mazima ya ukaguzi na udhibiti wa ubora wa chakula na vipodozi nchini.

Hivyo kuhatarisha afya za watanzania.

#MaendeleoHayanaChama
 
Maafisa Afya kwenye Halmashauri hawawezi kazi mpaka usubirie TBS ambao Wana ofisi kwenye Kanda?

Punguza siasa a chukiiii 'Toxic' ili kichwa kipate Logic.
 
Back
Top Bottom