Mr Antidote
JF-Expert Member
- Jan 11, 2015
- 952
- 1,293
Wakuu habari zenu!
Nimekaa tu hapa baada ya kuvimbilwa maharagwe nikishushia na maji yangu ya kandoro, chini ya kivuli cha mpapai huku nikitafakuri ya mwaka 2016 unaoisha na mambo yake.
Nikiwa napanga nakupangua kwa ajili ya mwaka 2017 ghafla wazo la likanijia.
Moja ya mambo yaliyotikisa mwaka huu ni ukosekanaje wa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu. Ukiachilia mbali ukosekanaji huo wa ajira pia, bodi ya mikopo nao imekujaa juu kudai madeni yao.
Sasa swali vipi hawa heslb wataweza kukusanya pesa yao ikiwa watu wanawao wakopesha wakihitimu ajira hakuna?
Kitu cha kufurahisha zaidi kwamba bado mikopo inaendelea kutolewa japo si kama awali na wakijua kwamba hawa jamaa kuja kupata ajira baada ya kuhitimu ni bahati nasibu.
Mwisho wa kufikiria nikaona hivi kwanini hii bodi ya mikopo isiwakopeshe hawa jamaa hizi pesa kama mtaji wakafanye ujasiliamali badala ya kwenda chuoni miaka 3 au 4.
Hawa wanafunzi wanapokea si chini ya 2mil kwa mwaka ukizidisha mara miaka 3 ni ni mil 6. Kwanini wasitoe elimu ya ujasilia mali kwa kipindi cha mwaka 1 na baada ya kuhitimu wakawapa hao wahitimu angalau mil 5 kila mmoja kwenda kuanza ujasilia mali?
Simaanishi watu wasisome elimu ya juu la hasha bali waweke kiwango fulani kwa ajili ya watu kwenda elimu ya juu ambao baada ya kuhitimu watakua na uwezo wa kuwaajili angalau nusu yao.
Hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira pia itawasaidia hata hawa heslb kupata pesa zao kwa wakati.
Japo changamoto zitakuwepo lakini na amini kwa kiasi itapunguza watu wasio na ajira mtaani.
Mwisho kabisa niwatakie heri ya mwaka mpya wa 2017 na Mungu awatangulie na kuwafungulia yale mnayoyaomba na kuyatamani kwa mwaka ujao.