Nawaza Tu huu Mwaka Mmoja na Miezi 7 Tu!

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Najiuliza JPM ana mwaka Mmoja na Miezi Saba tangu aanze kazi ya urais baada ya baadhi ya Watanzania kumchagua
Kwa upande wangu huu mwaka Mmoja na Miezi 7 ya jamaa kuongoza nchi naona kasababisha tu life liwe gumu ,na kuhusu kufukuza watumishi wenye vyeti feki na hewa naona hakuna impact yoyote hadi sasa Kwa sababu wafanyakazi hawajaongezewa salary,hakuna ajira za maana zilizowanufaisha Watanzania wengi zaidi ya kuajiri walimu 3000 na Mia kadhaa wa sayansi bado hapa naona hakuna jipya alilofanya
Katoa wafanyakazi hewa,katumbua watumishi wenye vyeti feki,kabana matumizi but still mambo ovyo mtaa wapiga Kura wake wanalia ukata
Mwaka Mmoja na Miezi 7 ya jamaa hatuangalii Bunge live,no freedom of speech ukikosoa kidogo unakamatwa eti mchochezi
Sera ya viwanda naona bado ni ngonjera tu na porojo sijasikia au kuona angalau ramani ya kiwanda cha kutengeneza tooth pick
Suala la madini limeibuliwa na watu wakashangilia na kuanza kulazimisha maandamano ya kupongeza wakati bado matunda ya ufuatiliaji wa hizo rasilimali hatujayaona mnapongeza nini sasa
Mwaka Mmoja na Miezi 7 naona ni kukamata wapinzani tu na kuwatupa lupango na kuona ni maadui wa utawala na maendeleo ya nchi sielewi !!
Mwaka Mmoja na Miezi 7 naona wanafunzi wa vyuo vikuu wanalialia Tu kukosa mkopo
Ajira hakuna pesa hakuna
Tuache unafiki na kujipendekeza safari bado ndefu tusubiri angalau nusu ya safari halafu tuangalie tulikotoka
Sijaona cha kupongeza wala kuandamana ndani ya mwaka mmoja huu na Miezi 7.
OVA
 
wengine wanaandamana kumpongeza wewe unalalamikaaa ? watakushangaa ila watanzania ni wanafki dunia nzima
 
Comrade Sigara Kali
Nakubaliana nawe baadhi ya vipengele.
Uongozi ni kazi ngumu sana hasa huku Afrika.
Ukikiuka misingi yake....hakika miaka inakimbia sana...
 
Back
Top Bottom