Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,300
- 33,915
Kwa Mbinyo wanaopewa wapinzani wa CCM na wale wana CCM wanaotaka kuwa na mawazo huru na yaliyo tofauti na viongozi wao, nimewaza ikitokea siku Jamiiforums isiwe hivi ilivyo ama isiwepo kabisa, siasa zetu za Tanzania zitakuwaje!
Nawaza nguvu ya Jukwaa hili kwa siasa za nchi yetu iwe kwa vyama vya upinzani ama kwa CCM, itakuwaje lisipokuwepo. Hapa JF ndipo wanasiasa wanapoambiwa bila ya kuhurumiwa wala kuonewa aibu na ama na wafuasi wao waliojificha nyuma ya majina bandia ama na wapinzani wao kuhusu udhaifu wao na ujinga walio nao.
Unaposikia wanasiasa wanahanikiza kwamba mitandao ya kijamii ni hatari kwa "amani na utulivu" wa nchi yetu, ujue hapo inatajwa JF kwa jina la uficho. Kuna watu leo hii kwa jinsi wanavyoichukia JF wakipewa nafasi ya kuchagua kati ya kuishi na mwanawe na JF ama kuishi bila mwanawe na bila ya JF atachagua kuishi bila mwanawe na kuishi bila ya JF pia.Ataona ni bora mwanawe afe ili na JF nayo ife. Lakini baada ya hapo siasa zetu zitakuwaje?
Kwa mbali kinasikika kishindo cha zimwi lenge minyonyoro na kufuli la shaba likiinyemelea JF. Kuna kauli kama kuashiria "Bora JF isiwepo tupumzike na makelele yao". Lakini bila Jf siasa zetu Tanzania zitakuwaje?