Cleopatrasat
Member
- Jul 19, 2022
- 11
- 1
Watu wangu wengi wa karibu ni wafanyakazi katika makampuni hapa Dar es salaam lakini wanapenda sana kujihusisha katika kilimo, kutokana na kazi kuwabana na uaminifu mdogo kati ya ndugu au rafiki katika pesa wengi wao wameshindwa kuwekeza kwenye kilimo kuhofia usimamizi wake utakua mdogo sana au kusiwe na usimamizi kabisa na hata utapeli na uaminifu mdogo kutoka kwa wale watakaokuwa wanasimamia.
Hii ikanifanya nichunguze hata kwa watu wengine nje ya wale ninaowafahamu na kugundua hili ni tatizo la watu wengi, hapo nikapata namna nzuri ya kutatua changamoto hii.
Nikaona kuna uwezekano mkubwa kuanzisha kampuni itakayokua inajihusisha na kusimamia masuala ya kilimo ambapo watu watakua wakiwekeza pesa zao kwaajili ya kilimo lakini msimamizi mkuu ni kampuni hiyo nitakayo anzisha, uaminifu wa kutosha, kuajiri wafanyakazi mahiri na wachapakazi ambayo pia itasaidia kutoa ajira kwa vijana wengi, ushirikiano mzuri kati yangu na wawekezaji katika kila hatua ili wawe wakijua kila shughuli inayofanyika na matumizi ya njia zote bora za kilimo kuhakikisha faida ya wale waliowekeza inapatikana ndio vitu vikuu nilivofikiria katika kufanikisha hilo.
Naamini kupitia kampuni hii uwekezaji katika kilimo utaongezeka zaidi kwa sababu watu wengi watapata mahali wanapoamini pesa zao zitakua salama na utendaji kazi ni mzuri, hivyo sekta ya kilimo ikikua zaidi; kutakua hakuna tatizo la chakula nchini, biashara na masoko vitatanuka zaidi na watu wengi watajipatia ajira kwa kujiajiri na kuajiriwa.