Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Mara zote mgomo wa madaktari ni jambo la mwisho kabisa katika jamii; ni ishara ya mambo kuwa mabaya na ushahidi wa kushindwa kwa sera za walioko madarakani. Kuanzia mwaka 2006 wakati ule mgomo wa kwanza kuikumba serikali ya JK wengi wetu tulitarajia kuwa wangeonesha ubunifu na uthubutu wa kutatua matatizo yanayokabili sekta ya afya nchini. Hata hivyo, miaka zaidi ya sita baadaye madai yale yale, yenye kuhusu mambo yale yale yakielekezwa kwa viongozi wale wale yamekuwa yakitolewa na karibu mara zote majibu yamekuwa yale yale "tukae mezani tuzungumze".
Kilele cha haya ni mazungumzo ambayo wengine kwa kweli tuliyabeza kwa sababu hayakufikia makubaliano ya jumla. Naamini wakati huu serikali ni lazima ioneshe kuwa inaweza kutatua matatizo na madaktari waoneshe msimamo kuwa wanachogombania ni maslahi makubwa zaidi - nafuu kwa wagonjwa. Binafsi, naunag mkono mgomo huu endapo hatima yake itafikia kwenye kufanya mabadiliko makubwa ya sekta ya afya ambayo itaonekana kumjali mgonjwa na yenye kuhakikisha huduma ya kisasa, nafuu inapatikana kwa urahisi na kwa uhakika kwa watu wote.
Nikijua uzito wa mgomo huu na matokeo yake kwajamii nashindwa kujizuia bila kuunga mkono nikiamini kuwa viongozi hawana uwezo wa kutatua matatizo haya hadi yabane kweli kweli kama tulivyoona mgomo wa mwisho. Madaktari wakikaa tena chini kunywa soda Ikulu watakuwa wamepoteza uhalali wao; mazungumzo yoyote sasa ni lazima yafikie kukubaliwa kwa madai namabadilikombalimbali tena kwa maandishi na yaonekane kwenye bajeti ya afya.
Hatuwezi kuwa kwenye mgomo wa sekta hii kila baada ya miezi sita!!! Suluhisho la kudumu liwe tokeo kuu la mgomo huu.
I support the doctors!