Nawauliza watawala, hivi sisi wananchi mnatuonaje? Mnatuchukuliaje?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Mnatuambia, tunawasikiliza. Tunawaheshimu. Tunafuata mnachoagiza. Tunawatii bila shuruti. Tunawapenda bila kuwaponda. Tunawaombea bila umbea hadi mnabarikiwa. Tunawaunga mkono kwa yenu maono. Tunawajali kuliko asali na kuwathamini kwa kuwaamini.

Tunakubali mkitukataza bila kukwaza (mf. katazo la mikutano ya hadhara mbele ya hadhira yenye 'hasira' ya vyama vya siasa). Tunawashangilia bila kulia hata kama 'mnatupanga' (mf. wapokeaji wageni uwanja wa ndege wa JKN na Wazee wa Dar). Tuko nanyi kuanzia kule hadi sasa.

Lakini, nyinyi mnatuchukuliaje sisi wananchi wenu? Mnatuonaje? Tukiwashauri, mnatuona jeuri na kiburi. Tukiwakosoa, mnatuona tunakosea na mnataka kimya. Tukiwaongezea mawazo mnatuona hamnazo kuliko mwanzo. Tukichangia hoja, mnatuona vihoja vya haja kama sarawili isiyo na mkaja.

I wapi haki yetu ya kuwarekebisha na kuwashauri chamani na Serikalini? I wapi haki yetu ya kusema kwa uhuru mahali penye nuru na nyingi duru? I wapi haki ya kidemokrasia kuhutubia mamia na ukweli kuwaambia? I wapi nafasi yetu ya kujinafasi bila wasiwasi wa uasi kama watanzania?

Tunachowapa, mtupe. Tukiheshimu, mtuheshimu. Tukiwasikiliza, mtusikilize. Tukiwatii, mtupende kama tende wakati huu wa mfungo. Msituchukulie 'poa'. Ni kwakuwa tu nafasi za kiuongozi ni chache. Wote hatuwezi kuwa nyinyi. Hii ni nchi yetu sote.Tafadhali msituone hamnazo!

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Mnatuambia, tunawasikiliza. Tunawaheshimu. Tunafuata mnachoagiza. Tunawatii bila shuruti. Tunawapenda bila kuwaponda. Tunawaombea bila umbea hadi mnabarikiwa. Tunawaunga mkono kwa yenu maono. Tunawajali kuliko asali na kuwathamini kwa kuwaamini.

Tunakubali mkitukataza bila kukwaza (mf. katazo la mikutano ya hadhara mbele ya hadhira yenye 'hasira' ya vyama vya siasa). Tunawashangilia bila kulia hata kama 'mnatupanga' (mf. wapokeaji wageni uwanja wa ndege wa JKN na Wazee wa Dar). Tuko nanyi kuanzia kule hadi sasa.

Lakini, nyinyi mnatuchukuliaje sisi wananchi wenu? Mnatuonaje? Tukiwashauri, mnatuona jeuri na kiburi. Tukiwakosoa, mnatuona tunakosea na mnataka kimya. Tukiwaongezea mawazo mnatuona hamnazo kuliko mwanzo. Tukichangia hoja, mnatuona vihoja vya haja kama sarawili isiyo na mkaja.

I wapi haki yetu ya kuwarekebisha na kuwashauri chamani na Serikalini? I wapi haki yetu ya kusema kwa uhuru mahali penye nuru na nyingi duru? I wapi haki ya kidemokrasia kuhutubia mamia na ukweli kuwaambia? I wapi nafasi yetu ya kujinafasi bila wasiwasi wa uasi kama watanzania?

Tunachowapa, mtupe. Tukiheshimu, mtuheshimu. Tukiwasikiliza, mtusikilize. Tukiwatii, mtupende kama tende wakati huu wa mfungo. msituchukulie 'poa'. Ni kwakuwa tu nafasi za kiuongozi ni chache. Wote hatuwezi kuwa nyinyi. Tafadhali msituone hamnazo!

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

MADARAKA yanalevya,mtakuja kushtuka akishamaliza muda wake
 
Vipi tena Mkuu wamekufanya nini huko Lumumba? Mimi nilidhani hiki kilio ni cha wapinzani peke yao!
 
Heshima ingekuwepo kama kura zetu tunazitumia vizur,lakin wa Tz ni wapumbavu tutavunjiwa heshima na viongizi kwani nauhakika wa madaraka kila uchaguzi
 
Back
Top Bottom