Nawauliza TANESCO mbezi beach mnajua maana ya emergency kweli?

bigKilaza

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
356
211
Jirani yangu kapata tatizo leo siku ya tatu hana umeme. Kaenda kutoa taarifa ya tatizo la mita waliomfungia haifanyi kazi hivyo kusababisha kukosa umeme siku ya tatu leo. Wale jamaa wa emergency walimwambia baada ya masaa 24 watakuja kwenye tukio toka saa aliyotolea taarifa sasa uliza hayo masaa 24 + 24 +24 + ? Ukiwapigia wanakwambia wapo njiani. Jamani badirikeni mkishindwa kufanya kazi muache sio mpo kusubiria kutumbulia. Meneja watu wako wanakuangusha.
 
Kati ya watu waomuangusha mheshimiwa Rais ni pamoja na Tanesco,wapo slow sana katika suala zima la utatuzi wa matatizo ya wananchi.Yani tatizo dogo kama hili linamfanya mtu alale giza zaidi ya siku 3 da hii ni hatari sana aisee
 
Zamani wakati wa mamita ya kuzunguka ,yangu ilisimama ghafla, nikatoa taarifa mara tatu kwa nyakati tofauti ,hawakuwahi kuja. Kwa mwaka mzima niliendelea kula mema ya nchi mpaka nilipofungiwa mita ya luku
Kwa kweli utendaji wao unakera
 
Back
Top Bottom