Nawatetea Serikali, TCRA, Polisi na mitandao ya simu kuhusu utapeli wa "Tafadhali tuma kwa namba hii"

Rwazi1

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,019
2,000
Nitangulize samahani kwa wadau watakaodhani natetea uhalifu (ubaya) wa namna yoyote. Lakini wema na ubaya havijawai kuachana kama mwanga na giza. Ifikie hatua waibiwaji tujitathmini.

Ubaya ukikwaza wengi mtu timamu huangalia wapi tatizo linaanzia.

Hili la wizi wa mtandaon kama "tafadhari tuma humu" naomba lawama zote nizielekeza kwa wahanga wenyewe.

Huwezi kudai haki kama hutimizi wajibu. Unatumaje pesa kwa sms ya namba usiyoijua bila hata kuhakiki na mhuska!

Kwa haraka haraka Watanzania bado sana tuna uzembe uliopitiliza. Mengine tunaipa serkali mizigo ya ovyo kabsa. Hata nchi jirani zenye watu makini hawana kiwango hiki cha ujinga na ushamba wa dunia ya mitandao.

Kuna mtu anaibiwa kizembe hadi unataman umzabe kibao kama bonus. Serkali ni kama inajitaid kulea na kulinda watoto walemavu wa kutafakar katika kila tambo.

Nashauri kuanzia chekechea watoto wapewe masomo ya kutafakar na kuchaj akili. hili ni pamoja na kuwapa nguvu ya kuhoji na kujihoji. Haki na Wajibu. Kodi na Rushwa. Watu ni waoga hadi dhidi yao wenyewe.

Mbinu hubadilika, bora kuongeza nguvu kwenye ufaham kuliko kutafuta wahalifu kwa kila mbinu mpya inayoibuka na kwa gharama kubwa. Serkali na taasisi zake tuipunguzie mzigo wa kufukuza upepo wakat kuna wizi halisi wa kimtandao kama wa hackers.

Kifupi tu watu wengi wanaibiwa mtandaoni kwa sababu za uzembe, kutojari, ushamba na ulimbuken. Yan KUTOWAJIBIKA!
 
Rwazi1

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,019
2,000
We Mirembe panakufaa
jikite kwenye hoja usijitoe fahamu. unamtumiaje mtu pesa kisa umeona sms ya tuma humu kama hauna walakin wa kufikiri na kutafakari? tujengeane fikra ya kibenk kuwa chukulia kila mteja amekuja kukuibia ili kuwepo umakin zaidi. hata mtandaon hivy hivyo kila kitu fikiria mara 3. ndo maana wanaonunua online huangalia kwanza reviews za kampun kama si ya kitapeli. jifunze kuwajibika sio kulalama tu utadhan serkali inakaa kwenye ubongo wako ili ifikirie kwa niaba.
 
CalvinPower

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
1,552
2,000
Sasa kama unawatetea kwali lazima uje ufungue uzi? Watetee kivyako sio lazima uje ufungue uzi ili kupata maoni yetu. Wewe ungesema tu unakusanya maoni then uangalie yapoje na sio kusema nawatetea, watetee tu kivyako.
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
18,002
2,000
Kwa haraka haraka Watanzania bado sana tuna uzembe uliopitiliza. Mengine tunaipa serkali mizigo ya ovyo kabsa. Hata nchi jirani zenye watu makini hawana kiwango hiki cha ujinga na ushamba wa dunia ya mitandao.

Kuna mtu anaibiwa kizembe hadi unataman umzabe kibao kama bonus. Serkali ni kama inajitaid kulea na kulinda watoto walemavu wa kutafakar katika kila tambo.
Basi serikali ikae pembeni iwaache raia wake waendelee kuliwa maana yote ni ujinga wao
 
jkipaji

JF-Expert Member
Sep 22, 2019
2,008
2,000
Basi serikali ikae pembeni iwaache raia wake waendelee kuliwa maana yote ni ujinga wao
Ulinzi wa Mtu, unaanza na Mtu mwenyewe! Usitegemee Serekali ikulinde wakati wwe mwenyewe huwezi kujilinda hata kwa kuvuka barabara,unataka mpaka traffic aje akuvushe barabara!!
 
Noti bandia

JF-Expert Member
May 3, 2020
820
1,000
Anachokisema mtoa mada nakubaliana naye kabisa, kunautapeli mwingine niwakijinga sana mpaka huwa najiuliza hivi hao matapeli huwa wanatumia dawa ama!.

Kunandugu yangu alitapeliwa kijinga sana, eti katumiwa meseji inayoonyesha amepokea laki nne na nusu wakati anawaza afanye nini akapigiwa simu na huyo tapeli kumbembeleza amrudishie hiyo pesa kwani kakosea kutumia akamtumia yeye.

Ndugu yangu anaridhia kurudisha pesa ila tapeli anamuingiza king kuwa ni vyema aende kwa wakala amuombe wakala ndio amtumie pesa then yeye ataitoa hiyo pesa kwa wakala. Tena anampa na bonus kuwa usitume laki nne na nusu Bali tuma laki nne hiyo hamsini ni yako kama shukrani.

Ok kaenda kwa wakala uzuri wanajuana, wakala kwa sababu wanajuana hakudai pesa mbele Bali akaweka pesa kama ndugu yangu alivyomwambia. Wakala wakati anadai pesa ndugu yangu anamwambia ipo kwenye simu itabidi niitoe kwako then anampa na Mkasa ulivyokuwa.

Hapo tayari alishatapeliwa. Hivi kweli hata kabla ya kwenda kwa wakala mtu hujiulizi maswali kidogo.
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
18,002
2,000
Ulinzi wa Mtu, unaanza na Mtu mwenyewe! Usitegemee Serekali ikulinde wakati wwe mwenyewe huwezi kujilinda hata kwa kuvuka barabara,unataka mpaka traffic aje akuvushe barabara!!
Huko barabarani ni wewe sijazungumzia huko
 
Brightfame

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
1,207
2,000
Nitangulize samahani kwa wadau watakaodhani natetea uhalifu (ubaya) wa namna yoyote. Lakini wema na ubaya havijawai kuachana kama mwanga na giza. Ifikie hatua waibiwaji tujitathmini.

Ubaya ukikwaza wengi mtu timamu huangalia wapi tatizo linaanzia.

Hili la wizi wa mtandaon kama "tafadhari tuma humu" naomba lawama zote nizielekeza kwa wahanga wenyewe.

Huwezi kudai haki kama hutimizi wajibu. Unatumaje pesa kwa sms ya namba usiyoijua bila hata kuhakiki na mhuska!

Kwa haraka haraka Watanzania bado sana tuna uzembe uliopitiliza. Mengine tunaipa serkali mizigo ya ovyo kabsa. Hata nchi jirani zenye watu makini hawana kiwango hiki cha ujinga na ushamba wa dunia ya mitandao.

Kuna mtu anaibiwa kizembe hadi unataman umzabe kibao kama bonus. Serkali ni kama inajitaid kulea na kulinda watoto walemavu wa kutafakar katika kila tambo.

Nashauri kuanzia chekechea watoto wapewe masomo ya kutafakar na kuchaj akili. hili ni pamoja na kuwapa nguvu ya kuhoji na kujihoji. Haki na Wajibu. Kodi na Rushwa. Watu ni waoga hadi dhidi yao wenyewe.

Mbinu hubadilika, bora kuongeza nguvu kwenye ufaham kuliko kutafuta wahalifu kwa kila mbinu mpya inayoibuka na kwa gharama kubwa. Serkali na taasisi zake tuipunguzie mzigo wa kufukuza upepo wakat kuna wizi halisi wa kimtandao kama wa hackers.

Kifupi tu watu wengi wanaibiwa mtandaoni kwa sababu za uzembe, kutojari, ushamba na ulimbuken. Yan KUTOWAJIBIKA!
Sawa, endelea kutetea vibaka wenzio !!
 
pmwasyoke

JF-Expert Member
May 27, 2010
4,109
2,000
Mleta uzi yupo sahihi kuelimisha juu ya kujihami dhidi ya matapeli wa jinsi tajwa, lakini haikuwa lazima kuzitetea taasisi alizozitaja.
 
Ti Go

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
674
500
kwahiyo hao wezi wapo sahihi??
Tatizo la wamiliki wa mitandao ukiwapa ushahidi wa namba za hao matapeli, hawazifungi. Hao matapeli wanajuaje kuwa hela imeingia? Unapoingiziwa hela ndiyo msg za kitapeli zinaanza! Kuna connection ya matapli na wafanyakazi wa mitandao!
 
Rodwell mTZ

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
700
1,000
Makampuni ya simu,yaani Vida,Tigo,Airtel na wengineo wabuni programu waiingize kwenye system zao ambayo itakuwa inafuta ujumbe wowote ulioandikwa "usitumie kwa namba hii .........tuma kwa namba hii........"
Au programu kama hiyo mnasubiri nayo mtengenezewe na mataifa yaliyoendelea? yaani mnakuwa kama makondakta wanaokaribisha wezi kwenye daladala wanazozihudumia,tafakarini mchukue hatua.
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
55,272
2,000
Maelezo haya nimeyaelewa;

"Nashauri kuanzia chekechea watoto wapewe masomo ya kutafakar na kuchaj akili. hili ni pamoja na kuwapa nguvu ya kuhoji na kujihoji. Haki na Wajibu. Kodi na Rushwa. Watu ni waoga hadi dhidi yao wenyewe"
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom