Nawatakia Heri Katika Mfungo Mtukufu wa Kwaresma. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawatakia Heri Katika Mfungo Mtukufu wa Kwaresma.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Ng'wanangwa, Mar 9, 2011.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Tushiriki kikamilifu kukumbuka Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo Aliye hai.

  Tuwape stahiki zao wale wahitaji.

  Tuwe wapole. Wanyeyekevu. Wasikivu na Wavumilivu.

  Tutimize nadhiri zetu kwa Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi.

  Tumuombee Taifa Takatifu wa Mungu Israel. Aendelee kuwa Taifa Kubwa akikingwa na vijitaifa vidogovidogo visivyokuwa na ubavu wa kumfanya kitu. Avishikishe adabu (kwa Mkono wa Mungu kila vitakapoleta za kuleta).

  Ooh Jerusalem!!

  Tumsifu Yesu Kristo.
   
 2. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hayo ndio maisha yangu ya kila siku, wala si kwa ajili ya kwaresma tu!!
   
 3. R

  Rugemeleza Verified User

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mataifa yote ni ya Mungu. Na watoto wa Mungu ni wale wote wenye mioyo safi, hutenda mema, na kutii amri zake. Hawadhulumu wenzao au kuomba kupatilizwa kwa wale waliowadhulumu.
   
 4. m

  mcheshi JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 769
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Amani ya Kristo itawale mioyo yenu iwalinde na kuwaongoza!
   
 5. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wapendwa hebu tuwekane sawa katika haya:

  1. hakuna kitu hapa duniani kinachoitwa "mfungo mtukufu".
  2. mimi ninajua kwa hakika kuwa mtukufu ni mmoja tu, ndiye Mungu. sifa na utukufu wote humwelekezea yeye.
  2. hakuna na wala halijapata kuwepao hapa duniani "taifa tukufu"
  3. mataifa yote ni yake Bwana na watu wote tangu kuumbwa kwa ulimwengu hadi leo ni kondoo wa maliisho yake na kwa nyakati zote, kila aliyeliitia jina la Bwana aliokolewa bila kujali alitoka taifa gani.
  4. Mungu mwenyezi na mwingi wa rehema na neema hajawahi wakati wowote kuhitaji nadhiri kutoka kwa wanadamu. yeye anasema "ndio" yenu na iwe "ndio" na "sio" yenu na iwe "sio"
  5. kila lililo tunda la roho ni wajibu wa mkristo yoyote wa kweli siku zote za maisha yake na hangoji ujio wa mfungo wa kwaresma

  Mungu akubariki mpendwa kwa kututakia heri

  Glory to God
   
 6. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160

  Milele Amina!!!!!

  Si kufunga kwa nje tu na kiroho zaidi
   
 7. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa DA, nakubaliana nawe 100% kuwa kufunga kwetu kuwe kiroho zaidi na si kwa nje tu. ubarikiwe sana.

  tatizo la wengi wetu tunazingatia zaidi kufunga kwa nje kuliko kiroho. ukishadeclare openly kwamba tunaanza mfungo tarehe XX na tunamaliza mfungo wetu tarehe XX tayari imeishakuwa ni "kufunga kwa nje" kufunga kwa ndani mtu huwezi jua lini mtu kafunga ama kafungua. tukiijua kweli, tutakuwa huru hakika

  stay blessed

  Glory to God
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,254
  Trophy Points: 280
Loading...