Nawatafuta Joseph (Mtoto wa Pili Athanas) na Patric (Mtoto wa Wanjila Zakharia) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawatafuta Joseph (Mtoto wa Pili Athanas) na Patric (Mtoto wa Wanjila Zakharia)

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mbinile, Nov 3, 2008.

 1. M

  Mbinile New Member

  #1
  Nov 3, 2008
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninawatafuta

  1.Patric ambaye mama yake ni Wanjila Zakaria. Patric alizaliwa Dodoma mwaka 1973 maeneo ya Msalato. Mama yake Patric ni mgogo. Baba yake Patric ni Mnyiha kwa jina ni Lemson Jonas Shale Mgalla

  Baba yake Patric alikuwa ni mwanajeshi katika kambi ya Mafunzo ya JKT (Msalato). Baba yake Patric alikuwa maarufu kwa jina la Sokomoko

  Baba yake Patric aliondoka Dodoma baada ya kupata ajali mbaya sana ya gari huko Dodoma. Hivyo tangu apate ajali hiyo hajawahi kuonana na mwanae Patric.

  Yeyote anayefahamu habari za Patric tafadhali awasiliane nami kwa tel. No. 0784-978072

  2. Joseph ambaye mama yake ni Pili Athanas. Joseph alizaliwa mwaka 1973 huko Dodoma. Mama yeke Joseph ni Muha. Baba yake Joseph ni Lemson Jonas Shale Mgallah

  Joseph na mama yake waliondoka Dodoma mwaka 1973 na kuelekea Kigoma kwa matembezi. Bahati mbaya Baba yao hakuweza tena kuonana nao. Kwani Baba yao alipata ajali mbaya sana. Baba yake anaamini Joseph na mama yake hawajui yaliyomkuta.

  Tafadhali kama kuna mtu yoyote anajua taarifa ya ndugu zangu hao anijulishe kwa tel. 0784978072

  ASANTENI
   
 2. Ngorunde

  Ngorunde JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2008
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 1,122
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa kupotezana na wapendwa wako kwa kipindi chote hicho. Ila ndg Mbinile kwa vile umebandika tangazo lako hadharani, ni lazima tulichambue ili na wengine tujifunze kutokana na yaliyopita. Inaonyesha mheshimiwa Mbinile (kama wewe ndiye) ulikuwa na uhusiona usiokuwa mzuri na wake zako....! Kwa nini nasema hivyo; Mosi. Haiwezekani katika mazingira ya kawaida kwa wazazi wote wawili ambao kwa bahati nzuri Mungu aliwajalia watoto mwaka mmoja, watoweke jumla pasi na mmoja wao kukutafute hata kupitia pale Msalato..!! Ajabu na kweli! Pili. Kwa bandiko lako tu hapo juu, pamoja na kwamba imepita miaka takriban 35 inaonyesha bado una chuki na wake zako/wazazi wenzio kwani hujawaulizia kama wako hai au wameshatangulia mbele za haki, kama kuna mwenye taarifa nao..! hiyo ni ajabu nyingine.
  Anyways nikutakie kila la kheri kwa yeyote mwenye taarifa nao atakujuza. Ila hili limenipa fundisho kubwa sana kuwa karibu na Mamsapu wangu maana hujafa hujaumbika.

  Kweli JF shule.
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hapa kaja kutafuta msaada si kuja kuwa offended kwa makosa ya zamani.
  Kama ni makosa bila shaka anajajutia ndio sababu kaona awatafute. Sasa mbaya gani?
  Kila la heri ndugu. Nakuombea upate hao ndugu zako.
  Nani anawafahamu? Jamani amsaidie!
   
 4. Ngorunde

  Ngorunde JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2008
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 1,122
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  MF nisome vizuri hapo juu, sijasema kwamba kuna ubaya kuja kutafuta wapendwa wake, Ila nimesema kwa makosa yake ya zamani wengi tumejifunza. Mimi nikiwa mmoja wapo. Na nimeamua kuyaainisha makosa hayo ili wengi tujifunze. nina imani hata yeye atakuwa amepata kitu katika maelezo yangu, pamoja na wewe kumsemea kwamba amejutia aliyoyafanya zamani. Nirudie tena kusema NINAKUTAKIA KILA LA KHERI NDUGU YETU KATIKA KUWATAFUTA WAPENDWA WAKO na sisi ndugu zako tumejifunza jambo.
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160


  ...Mwanzo mzuri ndugu Mbinile, natumai JF itawafikia ndugu zako hao na kufanikisha a happier reunion, labda pia na mzee wenu!

  Kwa wale wadadisi, mkumbuke; there are always three sides of a story;

  1.Their Story; Pilli Athanas & Wanjila Zakaria.

  2.His Story; Lemson Mgalla.

  3.The truth.

  ...which means, only by 'learning' Lemson Mgalla story, Pilli Athanas story and Wanjila Zakaria story we might know the TRUTH.

  Kila la kheri ndugu Mbinile katika safari ya kuwatafuta Ndugu zako.
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Nov 30, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Sishangai ndugu huyu kutoonana wala kutowatafutwa wanawe na wakeze kwa miaka yote hiyo yapata thelathini tano; inawezekana kutokana na ajalai mbaya aliyopta huenda alipata ulemavu uliomfadhaisha na huenda kukosa faraja na amanio moyoni kwa muda mrefu. Kwa wakati huu inawezakana amepata mtu wa kumfariji na ndipo ameanza kukumbukia ya zamani.

  Hata hivyo, mie ninamfahamu ndugu yangu wa damu kabisa ambaye naye alitengana na mke wake kimchezomchezo tu mwaka 1975 kwa sababu jamaa alikuwa anaoa mke wa tatu!!!!!!! Mkewe huyo hakufurahia kitendo cha mmewe kuoa wake wengi huku akiwa na watoto wapato sita wakati ule, hivyo akondoka kwenda kwao na watoto wake watatu. Tangu wakati huo huyu ndugu yangu hakuwahi kuchukua effort yoyote ya kujua watoto na mama yao wako wapi hadi pale alipokuwa mgonjwa sana mwanzoni mwa mwaka huu akawa anahitaji msaada hospital ndipo alipoanza kumtafuta mtoto mmja ambaye wakati huu ana kazi nzuri sana serikalini. Kwa bahati mbaya sana mtoto yule amemkana huyu baba yake wa damu!!!
   
Loading...