mult_talented_p
Senior Member
- Oct 10, 2016
- 103
- 120
Nawasihi vijana msijitoe muhanga.
Vumilieni mbaki hai.
Ukitamani kuwa kiongozi bora wa baadae, sio kwa kujitoa muhanga. Soma, omba Mungu. Fanya mambo yanayoonekana kwenye jamii. Mimi nina imani, haki itakuja bila kumwaga damu.
Biblia inatuhusia kuwa tuwaombee viongozi walioko juu yetu. Mungu aliwaambia wana wa Izraeli walioko uhamishoni kuwa waiombee amani nchi ile waliyokuwako maana katika amani ya ile nchi, na wao wangekuwa na amani. Nasi tuwaombee viongozi wetu; amani pamoja na, umoja wa nchi yetu.
Duniani kuna siasa za aina Tatu.
Siasa za Mrengo wa Kulia
Siasa za Mrengo wa Kushoto Na,
Siasa za Mrengo wa Kati; zisizofungamana na Mrengo wowote au, zikiwa zimechukua baadhi ya itikadi za Mrengo wa Kulia na baadhi za Mrengo wa Kushoto.
Wakati Mrengo wa Kushoto ukisimamia haki, na uhuru wa kiuchumi na kijamii, Mrengo wa Kulia unasimamia Maslahi ya nchi na ulinzi wa katiba ya nchi, ukiweka mkazo kwenye matakwa ya serikali. Hii ni kwa lugha nyepesi ya kuelewa. Mrengo wa Kati huwa ukichota baadhi ya itikadi kutoka Mirengo yote miwili.
Lakini, wananchi wengi ni mashabiki wa siasa, kama walivyo mashabiki wa soka, bila kujua kiundani sana, wanafungamana na siasa za Mrengo upi. Jambo hili halidhuru lakini ni vizuri kulifahamu.
Siasa inahitaji uvumilivu au kwa kimombo, Political Tolerance.
Siasa haipaswi kutenganisha jamii.
Siasa ni msingi wa utawala wa Nchi.