Nawasifu sana marais wetu kwa kutujengea miundombinu

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,137
33,200
Kila rais kwa awamu yake alijenga miundombinu ni jukumu lake kujenga miundombinu,hakuna rais duniani atakyeingia madarakani asijenge miundombinu,ukiona Rais wa hivyo huyo hatufai,kwa hiyo sio ajabu kwa Rais kujenga miundombinu.hivyo basi kitu pekee kikubwa kwa Rais yeyote kitakachomfanya akumbukwe daima na wananchi wa nchi yeyote kwa matendo yake na kuonekana kama Rais wa kipekee ni kuleta umoja wa kitaifa,kuwaunganisha watu,kuwaletea watu wake furaha,amani na maisha mazuri au maisha bora na mepesi kwa raia wake.

Kujenga miundombinu ni kazi ya serikari yeyote duniani kwa sababu raia wake hulipa kodi.

Kujengewa miundombinu sio hisani kiasi ikifika wakati wa uchaguzi mgombea urais, ubunge au udiwani anawaahidi wapigakura kuwa nitawajengea,barabara,daraja,reli uwanja wa ndege,shule,hospitali,kituo cha polisi n.k ,haya yote yapo kwenye mipango yamaendeleo ya Serikali.

Narudia tena nawapongeza maraisi wetu kwa kutujengea miundombinu na kutuletea maendeleo kupitia viwanda ,kilimo ,bishara,na mishahara bora.

Rais bora ni yule anayewajali wananchi wake kwa :-

kuwapa mishahara mizuri wafanyakazi itakayowawezesha kukidhi mahitaji yao kwa mwezi mzima.

Kuweka mazingira mazuri na rafiki kwa wafanyabiashara kufikia hatua ya kutamani kulipa kodi kwa furaha na amani.

kuweka mazingira mazuri kwa wakulima kwenye shughuli zao za kilimo ili wapate bei rafiki kwa mazao yao.

Anayewaletea amani,furaha na utulivu,kurahisisha maisha au kuondoa ugumu wa maisha.

kujenga miundombinu ni kazi ya mtawala yeyeote kwa mifano tu:
Nawapongeza sana Nyerere,Mwinyi,Mkapa,Kikwete na Magufuli.

Nyerere alijenga
Tazara,Mabarabara,madaraja,UDSM,viwanda kama UFI Urafiki,etc unaweza kuongezea nadahni huyu alijenga viyu vingi zaidi ya yeyote.

Mwinyi alijenga
Barabara,madaraja,madaraja,unaweza kuongezea

Mkapa alijenga
Mabarabara,madaraja (daraja la mkapa la kwenda kusini)uwanja mzuri kabisa wa taifa,muhimbili kitengo cha MOI,unaweza kuongezea

Kikwete alijenga,
Mabarabara,madaraja,(daraja kigamboni),hospitali ya moyo watu hawaendi kupasuliwa mioyo yao nje,njia za mwedno kasi kwa dar,unaweza kuongezea.

Magufuli anajenga
mabarabara,madaraja,anarudishashirika la ndege lililokuwepo wakati wa Nyerere baada aliyeliunda baada ya kuvunjika EAC.Unaweza kuongezea.

Hata hivyo kila rais amekua akiendeleza miradi ya ujenzi ama iliyoachwa na mtangulizi wake,ama ilikuwepo kwenye mipango ya maendeleo ya Taifa.

Narudia tena asanteni marais wetu kwa kutujengea miundombinu,hii ni kazi ya serikali asanteni sana
 
Back
Top Bottom