Nawashukuru wajumbe wa CCM jimbo la Nkenge kubwaga Assumputa na Kamala

Black Mirror

JF-Expert Member
Oct 17, 2019
833
1,041
Salaam wana JF,

Poleni kwa msiba wa Mh Mkapa, mbali ya kwamba CCM imeendeleza kuimarisha ufukara kwa Watanzania, lakini kwa Jimbo la Nkenge(Missenyi) nawapongeza sana tena sana wajumbe wa CCM kwa kazi kubwa mlioifanya ya kuwabwaga chini hawa vigogo yaani Dr Deodorus Kamala Buberwa na Huyu mama Asumputa Nshunju Mshama, hawa wote wamekuwa wabunge wa jimbo la Nkenge kwa vipindi tofauti lakini ukweli ni kwamba hakuna la maana lolote walilo lifanya, aidha obovu wao ulitegemeana.

Asumputa kwa miaka mitano ya nyuma alipokuwa Mbunge hakufanya jambo lolote la kuwatetea wana Nkenge, yeye aliishia kugawa mipira ya miguu, jezi kwa vijana pia na kanga kofia na visenti kidogo kwenye vikoba kwa akina mama, akaenda zake bungeni kula bata. Muda ulipoisha akapigwa chini na Dr Kamala, huyu ndiye hakufanya chochote na hakuweza hata kumfikia Asumputa walau kugawa jezi alishindwa.

Kamala ni mbunge pekee ambaye baada ya kuchaguliwa alianza kuwatukana wananchi wake kila walipojaribu kumueleza changamoto zao alisema wazi kuwa yeye hakupewa kura bali pesa yake ndiyo ilimpa kura. Alitoa majibu ya kejeli sana, mfno huko kwao kiziba waliwahi kumueleza juu ya uwepo wa kundi la ngedere kwenye mashamba yao aliwajibu hivi...."...ngedere wangekuwa wanaliwa wasingekuwepo..." lakini alisahau wananchi wa Nkenge wanapaswa kutetewa na kupiganiwa juu ya masula ya maji, umeme, barabara, hospitali, masoko na miradi mbalimbali.

Nawashukuru tena kwa kuwapiga chini hawa watu. Mh Kyombo mbunge mteule najua kwenye kamati kuu bado unaweza kuinuka kidedea, kama utaweza kuingia Bungeni hebu jaribu kwanza kurekebisha taswira ya Halmashauri ya Missenyi, ingia vijijini huko watu hawana maji, umeme, barabara nk.
 
Ni kweli hakuna mbunge wa kuleta hayo, lakini kazi ya mbunge ni pamoja na kuwasemea au kufikisha kero za wananchi huko serikalini hawa walishindwa pia. Alafu mtanzania yeyote anaye jitambua , kwa uchaguzi uliofanyika 2015 na uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka jana 2019, ni dhahiri hakuna Mtanzania anaweza kuiondoa CCM madarakani kwa box la kura, hapa watu wataishi kulaumiana tu lakini huo ndo ukweli.
 
Hivi Dodorous Kamala alikuja baada au kabla ya Asumpta?
Kamala alikuwa mbunge wa Nkenge alafu baadae akapigwa chini na Asumputa, Rais Kikwete akampeleka kuwa balozi nadhani nchini Ubeligiji kama sijakosea, Asumputa akawa mbunge hadi 2015, Baadae Kamala akarudi kuwa Mbunge tena 2015 hadi 2020, na kipindi hicho Asumputa amekuwa ni Mkuu wa wilaya .2020 Kamala akarudisha jina na Asumputa akarudisha jina , Mungu si mwemye upendeleo wote wakabwagwa chini maana hawana msaada wowote kwa wana Nkenge
 
Ooh nilikua silijui hili maana mara mwisho kuwasiliana na Kamala ilikua 2009 akiwa minister baada ya hapo nikasikiaga ameqngushwa 2010 kumbe alirudi.

Kqgera muache kuwaendekeza hao CCM hawana maana.
 
Ni kweli hawa jamaa wa CCM hawana maana kabisa, wamezidi kuchochea umaskini kwa Watanzania, lawama hizi pia ziende kwa POLISI na TAKUKURU
 
Huyu DK hata sikuhisi kama alirudi kuwa mbunge, bora ametoswa ila yote kwa yote niwape hongera kwa kumtosa Asumpta Mshama
 
Huyu Flolent Kyombo mteule mpya hapo Nkenge sina mashaka na utendaji kazi wake,ni zaidi ya jembe,naamini atalisaidia sana hilo jimbo kimaendeleo,kwani aliyoyafanya huko Wilaya ya Mvomero alipokuwa Mkurugenzi kila mtumishi wa pale anajua,brother yule kwa kweli anajielewa sana,Mwenyezi Mungu amjalie ktk safari yake ya kisiasa
 
Binafsi simfahamu vizuri huyu ndugu Kyombo, ila kwa utendaji wa Asumputa na Kamala bora CCM wangeweka hata kipande cha mti mkavu kingepigiwa kura lakini siyo hawa makupe, hawana la maana walilowasaidia wana Nkenge. Huyu Kamala ndo alikuwa anasaini pesa za bure huko mjengoni hana lolote na naomba apotee kabisa kwenye uwanja wa siasa japo najua anautajiri wa kutupwa. Huyu Kyombo asiige mienendo ya hawa naamini wana-Nkenge watampa ushirikiano mzuri.
 
Huyu DK hata sikuhisi kama alirudi kuwa mbunge, bora ametoswa ila yote kwa yote niwape hongera kwa kumtosa Asumpta Mshama
Alikuwa na tamaa ya Fisi amekuwa mbunge wa Nkenge kwa miaka kibao lakini hakuna lolote ambalo wananchi wanaweza kujivunia kwakwe.
 
Binafsi simfahamu vizuri huyu ndugu Kyombo, ila kwa utendaji wa Asumputa na Kamala bora CCM wangeweka hata kipande cha mti mkavu kingepigiwa kura lakini siyo hawa makupe, hawana la maana walilowasaidia wana Nkenge. Huyu Kamala ndo alikuwa anasaini pesa za bure huko mjengoni hana lolote na naomba apotee kabisa kwenye uwanja wa siasa japo najua anautajiri wa kutupwa. Huyu Kyombo asiige mienendo ya hawa naamini wana-Nkenge watampa ushirikiano mzuri.

Hyu brother pale Mvomero kaacha alama kubwa sana,hakuna mfanyakazi anayemwongelea vibaya,kwa kweli aliibadilisha sana ile Wilaya hasa kimapato na kiutendaji kiasi cha kwamba watu waliposikia anasepa anakwenda kutangaza nia kwao walibaki kusikitika tu,lakini mwisho wa siku kila mtu alimtakia kheri tu huko aliopopachagua,naamini huko atafanya vizuri zaidi kwa kuwa ni kitu anachokipenda zaidi,halafu ni mzuri mno kwa kujenga hoja,ukitaka kubishana nae kwa hoja ujipange,yupo vizuri sana,naamini hata akiwa Bungeni au kwenye Mabaraza yao ya Halmashauri atafanya vizuri pia
 
Mm nampenda kamala bora angekuja huku Bukoba mjini tungempa kura, nyie waziba wezi wezi na ubinafsi umewajaa.
 
Salaam wana JF,

Poleni kwa msiba wa Mh Mkapa, mbali ya kwamba CCM imeendeleza kuimarisha ufukara kwa Watanzania, lakini kwa Jimbo la Nkenge(Missenyi) nawapongeza sana tena sana wajumbe wa CCM kwa kazi kubwa mlioifanya ya kuwabwaga chini hawa vigogo yaani Dr Deodorus Kamala Buberwa na Huyu mama Asumputa Nshunju Mshama, hawa wote wamekuwa wabunge wa jimbo la Nkenge kwa vipindi tofauti lakini ukweli ni kwamba hakuna la maana lolote walilo lifanya, aidha obovu wao ulitegemeana.

Asumputa kwa miaka mitano ya nyuma alipokuwa Mbunge hakufanya jambo lolote la kuwatetea wana Nkenge, yeye aliishia kugawa mipira ya miguu, jezi kwa vijana pia na kanga kofia na visenti kidogo kwenye vikoba kwa akina mama, akaenda zake bungeni kula bata. Muda ulipoisha akapigwa chini na Dr Kamala, huyu ndiye hakufanya chochote na hakuweza hata kumfikia Asumputa walau kugawa jezi alishindwa.

Kamala ni mbunge pekee ambaye baada ya kuchaguliwa alianza kuwatukana wananchi wake kila walipojaribu kumueleza changamoto zao alisema wazi kuwa yeye hakupewa kura bali pesa yake ndiyo ilimpa kura. Alitoa majibu ya kejeli sana, mfno huko kwao kiziba waliwahi kumueleza juu ya uwepo wa kundi la ngedere kwenye mashamba yao aliwajibu hivi...."...ngedere wangekuwa wanaliwa wasingekuwepo..." lakini alisahau wananchi wa Nkenge wanapaswa kutetewa na kupiganiwa juu ya masula ya maji, umeme, barabara, hospitali, masoko na miradi mbalimbali.

Nawashukuru tena kwa kuwapiga chini hawa watu. Mh Kyombo mbunge mteule najua kwenye kamati kuu bado unaweza kuinuka kidedea, kama utaweza kuingia Bungeni hebu jaribu kwanza kurekebisha taswira ya Halmashauri ya Missenyi, ingia vijijini huko watu hawana maji, umeme, barabara nk.
Wewe utakuwa ni Riz king, umebadilisha id unajitekenya na kucheka mwenyewe.
Jitihada za wajumbe wa kura za maoni zimehamia mtandaoni, inawezekana wewe pia ukawa ni mgombea.
Tuliza mzuka, kama we ni msafi jina lako litarudi, usi panic kwenye teuzi hakuna figisu this time around mkuu.
 
Hujielewi mkuu( sorry for that) kwahiyo kutoa hisia , mawazo na furaha yangu unadhani mimi ni mwanasiasa. Usikariri sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom