Nawashauri viongozi wasituhadae kwenye suala la gharama za mitandao

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,603
29,742
Amani iwe kwenu.

b961e85e9623fc1552b162a58ff82925.png


Mamlaka za Serikali zimeonesha kusuasua kuisajili kampuni ya Elon Musk ( StarLink) ili kutoa huduma ya mawasiliano nchini.

Tuliosoma Cuba tunaelewa sababu za kusuasua huku. Mojawapo ya sababu hizo ni uwepo wa muungano usio wa kawaida kati ya makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano na wasimamizi wa sera ( mwenye akili afahamu) pamoja na watendaji wakuu wa sekta hiyo.

Haya yamejitokeza baada ya wakubwa hao kwa nyakati tofauti wamesimama kutetea upandaji holela wa gharama za motandao. Walienda mbali zaidi kwa kuwaambia Watanzania kuwa gharama bado zipo chini mno.

Kauli hizo ambazo zimekuwa zikitolewa zilikuwa zinajibu malalamiko ya Watanzania dhidi ya upandaji holela wa gharams za bando usiozingatia hali halisi ya vipato.

Kinachoumiza saikolojia za viongozi wetu ni aibu watakayokutana nayo ya unafuu mkubwa wa gharama za StarLink.
Pia uhakika wa connectivity unatishia ustawi wa makampuni yaliyopo sasa smbayo zaidi ya kuwaumiza watumiaji wake latika bei, bali pia kuzimwa kwa signals mara kwa mara hali inayolelekea kukosa uwiano wa kiwango cha bando zilizolipiwa na zinazotumika.


Unafuu wa mtandao wa StarLink ni jibu dhidi ya kauli za viongozi kuhusu unafuu walioutangaza wa gharama kubwa za mitandao nchini.


Tuwaombee
 
Kauli ya kila mbuzi ale kwa urefu wake .......
Chama chote kikawa chama cha mambuzi....
Mbuzi akiwa anakula hana urafiki na mbuzi wenzake....
 
Back
Top Bottom