Nawashauri Secret Service wa Marekani kuja Tanzania

mzalendo iq1

JF-Expert Member
Mar 10, 2020
1,258
1,541
Kama kawaida yangu huwa napenda kuleta nyuzi za kizalendo na sio za kisiasa.

Kutokana na suala la ulinzi wa watu wote muhimu duniani kuwa mkali na makini, basi walinzi wa baadhi ya mataifa ya Wazungu inabidi waje kujifundisha kitu katika kuwalinda viongozi wao wa nchi.

Kama tunavyofahamu Rais katika nchi anatakiwa apewe ulinzi wa hali ya juu, tena ikibidi hata walinzi wawe tayari kufa kwa ajili yake. Lakini nashangaa walinzi wa Marais wengi nchi za nje kuweka hatarini maisha ya Marais wao katika janga hili la Corona kwa uzembe wa kutochukua hatua sahihi.

Nawapongeza usalama wa taifa wa Tanzania kwa kuona umuhimu wa rais wetu na kuamua kumpeleka sehemu salama ambayo wao wanahisi itakuwa nzuri na rais kwa kumlinda Rais.

Pia, mkumbuke hata dini zimefundisha kuwalinda viongozi wenu, ndiyo maana hata Yesu alifichwa ila akasalitiwa na Yuda; hata Muhammad pia alikimbilia kujificha pangoni.

Ukitaka kujua ni kiasi gani Rais analindwa kwa hali na mali, angalia Putin alivyoingia kwenye mkutano mwezi wa tatu. Yaani walimvalisha kama vile anaenda mwezini.

Kiukweli kwenye hili swala usalama wa taifa wa Tanzania mmetisha sana. Marekan kila siku inatangaza kuwa Trump anatakiwa apimwe Corona huoni kama hio ni aibu kwa ulinzi wake?

Yaani rais maisha yake yanakua hatarini na hawachukui hatua yoyote. Kweli Marekani ni wakushindwa ujuzi na Usalama wa Tanzania?

Pia papa mwenyewe baada ya mlipuko wa Corona kulipuka itali alifungiwa ndani wiki 3 na hakuna aliyeruhusiwa kuonana naye.
 
Kwa hiyo kupelekwa Chato nayo ni sehemu ya ulinzi wa hali ya juu au sijakuelewa?
 
Putin mwenyewe Yuko mafichon

Screenshot_20200512-225415.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom