Nawashauri CCM tukubali matokeo tusilazimishe. Tusiue Misingi ya Utaifa kwa tamaa zetu

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Ninawaambia CCM tujijenge kisaikolojia kua hii nchi ni ya vyama vingi, huu mfumo imeruhusiwa na upo kikatiba. Kwahiyo ni lazima tukubali kuna mahali ni lazima tugawane kura za Urais na wapinzani, ni lazima tugawane majimbo na wapinzani, ni lazima tugawane halmashauri na upinzani.

Lazima ifike mahali tuelewe kuna majimbo katika nchi hii hata tuwapelekee wananchi wa maeneo husika maziwa na Asali bado watachagua Wapinzani tu, hii imekua Jadi yao tusilazimishe.

Kuna watu wachache wenye kauli za kijinga na za hovyo hovyo eti Upinzani mwaka huu haupati jimbo hata moja, huu ni ujinga. Nani kuambia kua upinzani utapoteza majimbo yake wakati umeshaile jamii hiyo katika hali ya upinzani. Kuna maeneo hata upeleke kitu gani kwao, watakuambia wao CCM "NO"

Tusiue kuvinja misingi ya utulivu wa nchi yetu kwa kulazimisha nazi kuanga kwenye Mwembe, tusilazimishe Uji kua maziwa. Vinginevyo tunataka kupora ushindi wa walioshinda kwa sababu ya tamaa za hovyo hovyo za madaraka na kupandikiza chuki.

Watu wanakubaia kua hawaitakii CCM kwakua kimekua Chama cha Ukimbizi tangu Uhuru, mifumo yake inaongozwa na kanuni zile zile za kila siku hakuna mabadiliko. Kuu yao ni kuona chama kingine kuliunda dola wapate ladha yake kwa mifumo mipya huenda nchi ikapata maendeleo.

Watu hawa huwezi kuwalazimisha wasichague CCM vinginevyo unataka mambo mengine.

Tukubali kua kuna majimbo yatabaki Upinzani na mengine yatarudi CCM kwa haki na kuna majimbo pia yataondoka CCM kwenda Upinzani. Hii ni character au nature ambayo inajitegemea yenyewe huwezi kuizuia.
 
Back
Top Bottom