Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,939
- 6,849
Wewe bila shaka ni kijana wa juzi na haujui hali ilivyokuwa nchini baada ya vita vya Kagera. Hali ile ilitokana na wenye fedha zao kutaka zifanyike structural reforms katika mambo ya uchumi. Haukuweko wakati tunapigiwa muziki London na kwingineko ili kushinikiza mataifa ya magharibi kutusamaa madeni yaliyotokana na fedha tulizokopa wenyewe. Haukuweko wakati watu wanazungusha kibakuli Dovos kumpa Mkapa ili zimsaidie kununua vyandarua.That is the issue, kama wanaweza kupata kwingine, basi watuache tufanye biashara na wengine ambao kwa standard zao kila kitu kiko sawa. Lakini wanakuja na hoja zao za "haki za binadamu na usawa wa binadamu" kwa viwango na vigezo vyao ambavyo kwao havitumiki ila wanataka vitumike kwetu tu. Tukivikataa, basi nongwa, eti tutawekewa vikwazo vya kiuchumi! Mnadhani ni rahisi namna hiyo? Nchi ngapi zimewekewa hivyo vikwazo au ni mikwara tu ya kutaka tuyumbe, watutoe kwenye RELI wapore utajiri wetu kwa faida yao. Hatuyumbi wala hatutolewi kwenye RELI we are an independent sovereign state na wenye kujua haki na wajibu wetu kwa watu wetu na kwa marafiki zetu wenye adabu na heshima na wanaotutakia mema. Kinyume cha hapo tutapamabana nao tu! Ingawa kwa watu wenye kasumba ya kikoloni, hili ni ajabu kwao/kwenu.
Wewe na wengine mnadhani hii ni mara ya kwanza sisi kujimwambafai na kusema tusiingiliwe kwenye mambo yetu. Mwaka 1999 tulipotaka kununua Radar kutoka BAE tulionywa sana na mabeberu kuwa tunauziwa kitu ambacho hakitufai na kwa bei isiyoendana na uhalisia. Tukawaambia watukome, tukanunua radar. Wote tunajua hatma ya hii hadithi. Mabeberu waliwafuatilia BAE ( kampuni ya kwao) na kugundua kuwa walitupiga sana kwenye ule mradi na kuwataka waturudishie kiasi kikubwa tu cha fedha.
Kuna mwaka tulitaka kumnunulia Rais wetu ndege. Tukaonywa sana lakini Waziri musikaali wa wakati ule akawaambia mabeberu kuwa tuko tayari kula nyasi ili Rais wetu apate ndege ya saiz yake. Wote tunajua mheshimiwa huyo aliishia wapi!
Waliotutangulia walituasa kuhusu umuhimu wa kuchagua vita tunazopigana. Nyingine, kama hii haina tija na hatuna sababu ya kuishupalia.
Amandla...