Nawashangaa Viongozi wa CCM kila linapotajwa kosa au tuhuma na nchi washirika wa maendeleo mnakimbilia kusema vita ya kiuchumi. Jibuni hoja kwa hoja

Jelavic

Senior Member
Dec 28, 2016
170
500
Yan nashangaa sana leo balozi wa ubelgiji anasema habari zinazo sambaa sio za kweli, Ndio nakubaliana nae sio za kweli lkn kuhusu hoja iliyopelekea ile habari kutokea ni yakweli au sio ya kweli.

Je, ni kweli mmebeba mapesa ya watu kwa jina la CORONA na hamjazitumia kwa lengo husika.
Je, ni kweli mliwakatalia WHO kutoa takwim na hali ya corona nchini.

Hizi ndio hoja inabidi zijibiwe kwanza kisha ndio tuangalie mambo mengine.

Hii nchi ikikosa msaada sio sabab eti vyama pinzani vimeshinikiza, wazungu sio wajinga kiasi hicho mpka wasikilize kila wanacho ambiwa kama hakina ukweli.

Jibu hoja sio kukimbilia kusema sentensi za jumla jumla ooh sijui hii ni vita ya kiuchumi, sijui mabeberu

Na kama nchi hii itapitia kipindi kigumu kimataifa basi sabab ni nyinyi CCM.

Nyinyi ndio mnawakilisha wananchi kwenye uongozi, tukifeli ni sabab nyinyi mmetufelisha.
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Hivyo ndio Vichaka vyao walivyo chagua kujifichia ,ukitaka kumuua Mbwa basi mpe Sifa mbaya itakuwa simple na msaada utapata kutoka pembeni.

Muda utaamua juu ya Uongo na Ukweli halisi ,Kitanzi kitakapo fika Shingoni wata toka walipo na Ukweli nnacho sikitika watakao umia zaidi ni Raia masikini .
 
mukaruka mzee

JF-Expert Member
Jan 22, 2020
915
500
Ni majuha tu, EU, US wanashida gani na uchumi wa TZ? Tunavyowauzia siyo essential to their survival. Wanaweza wakaishi bila kunywa kahawa, chai, (na nini tena?)
Naweza kusema kwa uhakika kabisa BILA KUJING'ATA ULIMI kuwa this can be the shallowest bandiko humu JF kwa 2020! Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu haingii akilini mtu kusema kuwa hizo nchi tajwa hazina shida na uchumi wa TZ! Kweli? Hata wao wakisoma hili bandiko watakushangaa. Wanahitaji malighafi karibu zote kutoka nchi zetu, ikiwemo TZ.

Wanahitaji madini yote, wanahitaji pamba yote, wanahitaji chochote atakachofikiria mtu makini humu JF. Nadhani mara ya mwisho ulipokwenda Ulaya au US au UK hukutembea na kuona how dependent they are on our raw materials and ALL CHEAP GOODS from our countries including TZ. Kama hawahitaji kitu, sasa wanahitaji nini - UTAWALA BORA NA HAKI ZA BINADAMU - for what kama siyo kutengeneza njia rahisi za kuiba malighafi zetu!?
 
Zamazangu

JF-Expert Member
May 16, 2015
669
500
Mimi ni mkufunzi Jana nikiwa darasani nagawa mitihani kwa vijana wangu niliponaliza mmoja Kati ya wale ambao hawakufanya nikamuuliza "Ulikuwa wapi siku ya mtihani"?
Kwa mshangao mkubwa akajibu kwa kujiamini SIKUWEPO!!
Darasa lote walimwangalia kwa kumhurumia wakijua fika hakujibu jibu sahihi.
Tatizo la kujibu swala tofauti na maudhui ya jibu sahihi imejengeka na kuanza kuwa tabia ya kawaida
Kwenye kada ya elimu na mafunzo tujaribu kuondoa OMBWE hili ambalo huharibu taswira yetu ndani na nje ya nchi
Unajiuliza je huyu mtu kashindwa kujibu jibu sahihi au ametawaliwa na UNAFIKI
Mungu ibariki Tanzania
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
26,171
2,000
Naweza kusema kwa uhakika kabisa BILA KUJING'ATA ULIMI kuwa this can be the shallowest bandiko humu JF kwa 2020! Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu haingii akilini mtu kusema kuwa hizo nchi tajwa hazina shida na uchumi wa TZ! Kweli? Hata wao wakisoma hili bandiko watakushangaa. Wanahitaji malighafi karibu zote kutoka nchi zetu, ikiwemo TZ. Wanahitaji madini yote, wanahitaji pamba yote, wanahitaji chochote atakachofikiria mtu makini humu JF. Nadhani mara ya mwisho ulipokwenda Ulaya au US au UK hukutembea na kuona how dependent they are on our raw materials and ALL CHEAP GOODS from our countries including TZ. Kama hawahitaji kitu, sasa wanahitaji nini - UTAWALA BORA NA HAKI ZA BINADAMU - for what kama siyo kutengeneza njia rahisi za kuiba malighafi zetu!?
Wewe ndiye mwaka huu umeweka argument so shallow kuwa umekuwa mshindi wa shallow argument mwaka huu. Say specifically kutoka Tanzania kuwa wakikikosa, viwanda vyao vinafungwa, mention specifically ni viwanda aina gani vitafungwa kwa vile TZ wamekataa kutoa mali ghafi zao.
 
Ryaro wa Ryaro1233

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
353
1,000
Mimi ni mkufunzi Jana nikiwa darasani nagawa mitihani kwa vijana wangu niliponaliza mmoja Kati ya wale ambao hawakufanya nikamuuliza "Ulikuwa wapi siku ya mtihani"?
Kwa mshangao mkubwa akajibu kwa kujiamini SIKUWEPO!!
Darasa lote walimwangalia kwa kumhurumia wakijua fika hakujibu jibu sahihi.
Tatizo la kujibu swala tofauti na maudhui ya jibu sahihi imejengeka na kuanza kuwa tabia ya kawaida
Kwenye kada ya elimu na mafunzo tujaribu kuondoa OMBWE hili ambalo huharibu taswira yetu ndani na nje ya nchi
Unajiuliza je huyu mtu kashindwa kujibu jibu sahihi au ametawaliwa na UNAFIKI
Mungu ibariki Tanzania
Jibu ni Unafiki na Kutaka Kuwafurahisha Waliomteua.. Kila Mmoja amelianaglia Bunge lile "EU", Anachokanusha Hata Hakieleweki.
 
Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
5,842

Upumbavu pumbavu tuuu, mistari mirefu hakuna points
 
KAPONGO

JF-Expert Member
May 29, 2009
1,560
2,000
Naweza kusema kwa uhakika kabisa BILA KUJING'ATA ULIMI kuwa this can be the shallowest bandiko humu JF kwa 2020! Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu haingii akilini mtu kusema kuwa hizo nchi tajwa hazina shida na uchumi wa TZ! Kweli? ...
Ni watu makini tu watakaoulewa ukweli huo. Wengine wenye akili za kushikiwa wataendelea tu na mapambio ya kudhani kuwa maendeleo yao binafsi yanategemea huruma, maelekezo na msaada wa wazungu. Watapata taabu sana!.
 
mukaruka mzee

JF-Expert Member
Jan 22, 2020
915
500
Wewe ndiye mwaka huu umeweka argument so shallow kuwa umekuwa mshindi wa shallow argument mwaka huu. Say specifically kutoka Tanzania kuwa wakikikosa, viwanda vyao vinafungwa, mention specifically ni viwanda aina gani vitafungwa kwa vile TZ wamekataa kutoa mali ghafi zao.
Nenda kaulize hiyo orodha sehemu moja inaitwa Economic Processing Zones (EPZ). Kwani nikikwambia mimi itakuwa ni ubishi usio na mwisho ila huko utaipata FRESH!
 
Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
10,514
2,000
Yan nashangaa sana leo balozi wa ubelgiji anasema habari zinazo sambaa sio za kweli, Ndio nakubaliana nae sio za kweli lkn kuhusu hoja iliyopelekea ile habari kutokea ni yakweli au sio ya kweli.

Je, ni kweli mmebeba mapesa ya watu kwa jina la CORONA na hamjazitumia kwa lengo husika.
Je, ni kweli mliwakatalia WHO kutoa takwim na hali ya corona nchini.

Hizi ndio hoja inabidi zijibiwe kwanza kisha ndio tuangalie mambo mengine.

Hii nchi ikikosa msaada sio sabab eti vyama pinzani vimeshinikiza, wazungu sio wajinga kiasi hicho mpka wasikilize kila wanacho ambiwa kama hakina ukweli.

Jibu hoja sio kukimbilia kusema sentensi za jumla jumla ooh sijui hii ni vita ya kiuchumi, sijui mabeberu

Na kama nchi hii itapitia kipindi kigumu kimataifa basi sabab ni nyinyi CCM.

Nyinyi ndio mnawakilisha wananchi kwenye uongozi, tukifeli ni sabab nyinyi mmetufelisha.
Hahahaaaa

Mataga bana/....

Utasikia "VITA YA KIUCHUMI".....

As if Tanzania ipo kwenye big leagues za kiuchumi wanagombea soko mahali..kumbe tupo matakoni humu hatuna chochote tunachoweza uza popote dunia hii....

"VITA VYA KIUCHUMI" my ass!!
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,667
2,000
Naweza kusema kwa uhakika kabisa BILA KUJING'ATA ULIMI kuwa this can be the shallowest bandiko humu JF kwa 2020! Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu haingii akilini mtu kusema kuwa hizo nchi tajwa hazina shida na uchumi wa TZ! Kweli? Hata wao wakisoma hili bandiko watakushangaa. Wanahitaji malighafi karibu zote kutoka nchi zetu, ikiwemo TZ. Wanahitaji madini yote, wanahitaji pamba yote, wanahitaji chochote atakachofikiria mtu makini humu JF. Nadhani mara ya mwisho ulipokwenda Ulaya au US au UK hukutembea na kuona how dependent they are on our raw materials and ALL CHEAP GOODS from our countries including TZ. Kama hawahitaji kitu, sasa wanahitaji nini - UTAWALA BORA NA HAKI ZA BINADAMU - for what kama siyo kutengeneza njia rahisi za kuiba malighafi zetu!?
Mbona mnapenda mno kuwatukana wenzenu? Hivi kuna mali ghafi ipi ambayo Ulaya haiwezi kupata kwengine kuliko Tanzania? Nadhani hauelewi kuwa sehemu kubwa ya Ulaya imetoka katika uchumi wa viwanda. Viwanda vya nguo viko Bangladesh, Cambodia n.k. kahawa inayopendwa na wengi ni ya Ethiopia na Columbia, chai ni kutoka Kenya na India, maua ni kutoka Kenya na Ethiopia, machungwa kutoka Spain na Misri, ndizi zinatoka Latin America, gas wanatoa Urusi na Qatar, korosho wananunua kutoka Vietnam na India ambao nao wananunua kutoka kwetu, msumbiji na Afrika Magharibi. Madini yapi ambayo tunazalisha yanachangia katika uchumi wao? Almasi wanatoa Botswana, dhahabu inazalishwa zaidi na Ghana na Afrika Kusini kuliko sisi. Msijidanganye, mpaka sasa ni sisi ndio tunaowategemea zaidi kuliko wao wanavyotutegemea. Au unadhani hizo ndege tumenunua ili sisi twende tukatalii Ulaya na sio wao waje kwetu kutalii?

Amanda...
 
CHARLES2016

Member
Mar 22, 2016
92
125
Jibu ni Unafiki na Kutaka Kuwafurahisha Waliomteua.. Kila Mmoja amelianaglia Bunge lile "EU", Anachokanusha Hata Hakieleweki.
Ile ilikuwa ni kamati ya bunge la EU inayodeal na nchi za Atrika, kwa hiyo ni sehemu ndogo mno ya bunge la EU lenye wabumge takribani 700, kamati hiyo ina wajumbe 70 unaweza kuona wajumbe waliochangia Jana hawafiki hata 10 na yale yalikuwa ni mawazo ya wajumbe hao ambao pia hawakufikia consesus. Kwa hiyo maamuzi ya kusitishwa misaada kwa Tanzania hayawezi kufanywa na kamati peke yake tena yenye uwakilishi mdogo kiasi hicho.
 
mukaruka mzee

JF-Expert Member
Jan 22, 2020
915
500
Mbona mnapenda mno kuwatukana wenzenu? Hivi kuna mali ghafi ipi ambayo Ulaya haiwezi kupata kwengine kuliko Tanzania? Nadhani hauelewi kuwa sehemu kubwa ya Ulaya imetoka katika uchumi wa viwanda. Viwanda vya nguo viko Bangladesh, Cambodia n.k. Kahawa inayopendwa na wengi ni ya Ethiopia na Columbia, chai ni kutoka Kenya na India, maua ni kutoka Kenya na Ethiopia, machungwa kutoka Spain na Misri, ndizi zinatoka Latin America, gas wanatoa Urusi na Qatar, korosho wananunua kutoka Vietnam na India ambao nao Wana wananunua kutoka kwetu, msumbiji na Afrika Magharibi. Madini yapi ambayo tunazalisha yanachangia katika uchumi wao? Almasi wanatoa Botswana, Dhahabu inazalishwa zaidi na Ghana na Afrika Kusini kuliko sisi. Msijidanganye, mpaka sasa ni sisi ndio tunaowategemea zaidi kuliko wao wanavyotutegemea. Au unadhani hizo ndege tumenunua ili sisi twende tukatalii Ulaya na so wao waje kwetu kutalii?

Amanda...
Kwa kweli siwezi kubishana on this eti we are not exporting anything huko Ulaya!? Sasa wanatutakia nini kama nchi au wanawataka akina Lissu!?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom