Mromboo
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 2,927
- 6,465
Hivi Karibuni kuna Tangazo linapita kwenye TVs zetu likionyesha binti wa chuo na kijana wachuo kama sijakosea wakienda hosipitalini kupata ushauri namna ya kujikinga na mimba wakiwa bado shuleni.
Mbaya zaidi binti anatoka huku akijiproud kuwa kapata mwarubaini wa kumaliza masomo bila kupata mimba.
Wanaonekana kuwa wako na pills za kupanga uzazi wakati bado ni vijana wadogo na wako masomoni. Tangazo linaonekana kuruhusu wanafunzi kufanya ngono mashuleni bila tahadhari ya virusi vya UKIMWI kuzingatiwa.
Kwenu wizara husika, hili tangazo linatufundisha nini kwamaadili ya Tanzania?
Kwamba mmesharuhusu wanafunzi kujamiana shuleni tena bila kificho huku wakitumia dawa za uzazi wa mpango ilhali hata ndoa hawana?
Mmeamua kuharibu kabisa maadili ya watoto wetu walioko mashuleni maana tangazo hili liko wazi kabisa na linaruka mpaka mida ya mchana?
Naomba sana wizara tajwa hapo juu mkae mapema sana na msitishe hili tangazo.
Tena mtoe mwongozo kwamba wanafunzi shuleni wanatakiwa kusoma na sio kujihusisha na ngono holela ambazo nje ya mimba za utotoni zitasababisha kuenea kwa virusi vya UKIMWI.
Inaumiza sana