Nawashangaa sana watu wanaoniona mimi ni mtu mwenye akili. Sijui wameona nini kwangu?

Ipo hivi, kuna ofisi moja kubwa sana hapa mujini nilianza kufanya nayo kazi takribani miaka minne hivi iliyopita mpaka sasa.

Wakati huo nikiwa bwana mdogo, ila sasa sijui ilikuwa kuwaje hawa wafanyakazi wenzangu kadri mda ulivozidi kwenda, walikuwa wananichukulia wa tofauti sana, mchapa kazi na mwenye akili sana.

Hata bosi wangu amekuwa akiniambia niandae report za strategy.. ama akiandaa pia report yeyote ananiambia nipitie mimi kama ina make sense.

Ki ukweli kabisa, japo sijawahi kuwaonesha reaction tofauti.. ila huwa nawashangaa sana hawa watu wanavoniona nna akili na mchapa kazi.

Ukweli kuhusu mimi, mimi ni mtu mvivu sana halafu pia nna uwezo wa kuwadanganya watu na kucheza na mawazo yao.. Hicho ndo nlichojaliwa tu... Hawajui yote nnayoyafanya kazini ni maigizo.. Na wao wameingia kingi wananiona mimi kama Einstein..

Nawaonea huruma sana, najua hawatewaza kuijui hii siri milele.. Maana hata watu nliosama nao chuo, nao nimefanikiwa kucheza na akili zao kwa mtindo huo huo..

Wananiona mimi ni mtu mwenye akili sana.. Kila siku lazima wadau wanipigie simu kuniomba ushauri.. Na mimi huwapatia kama vile wachungaji waongo waongo wanavocheza na akili za kondoo wao.

Nimefanikiwa kufika mahali kazini, nikitoa suggestion lazima ifatwe hakuna mwenye ubavu wa kuipinga hadharani. Nimewajengea picha ya kuogopwa na ni ngumu sana wao kujinasua. Unabishana na Genius??

Hayo ndo maisha yangu waungwana.. Huwa najiuliza sana kwanini watu wanakuwa wajinga kuniamini kiasi hicho..

Mimi deep down ni mvivu, sina jipya, sina akili nyingi kihivo... I am just a Conman... Lakini mbona sigunduliki??
Umewahi kuusikiliza wimbo unaitwa "me, myself and I"?.......
katika kila mtu kuna watu tofauti ndani yake... huyo unayemjua wewe ndani yako sio yule anayejulikana na jamii hiyo ya kazini kwako toka kwako..... Jamii ipo sahihi kabisa kukupa hiyo "definition" kuhusu wewe na wewe pia upo sahihi kujipa hiyo "definition" kuhusu wewe... its normal, ni kawaida kabisaa...
 
Back
Top Bottom