Uta Uta
JF-Expert Member
- Feb 2, 2016
- 3,739
- 8,736
Watumiaji wengi wa vyombo vya usafiri huwa hawapendi kuzingatia kanuni za usalama barabarani. Wengi wao hujifanya wana haraka kuliko wenzao. Na hii imepelekea kusababisha ajali nyingi barabarani hasa mijini. Ila nipende kutoa pongezi zangu za pekee kwa wanawake, hawa wanajitahidi sana kutii sheria, sehemu ya kusimama (zebra crossing) utawakuta wamesimama wanasubiri watembea kwa miguu wapite. Na mara chache sana kumkuta mwanamke ametanua barabara. Kama madereva wote wangefuata kanuni kama wanawake, tungepunguza ajali nyingi na kila mtumiaji wa barabara angeitumia kwa uhuru hasa watembea kwa miguu. Tifuate sheria, tuthamini maisha ya wenzetu nao pia wana haki ya kutumia barabara. Hongereni sana wanawake kwa hili*