Nawapongeza Kanali Kinana na Luteni Makamba kwa ukomavu, ustahimilivu na kufuata taratibu. Wakati wa kumtaja aliye nyuma ya Cyprian Musiba ni sasa!

Ana hofu kwa sababu anajua kwa hakika kuwa hakubaliki. Hakubaliki ndo maana ameshaanza kamoeni za urais kabla kipenga hakijapulizwa.
Kuna sehemu wamesema hii yote inasababishwa na mtu huyo anayemtu musiba kuwa na HOFU ,sasa mfalme Wa chato anakuwa na hofu yanini wakati wananchi wanamkubali
 
Na DAB anatumiwa kwa maslahi gani na ya nani?
Hesabu ni ndogo sana hivi nani ambaye untouchable kwa sasa hapa inchini anaweza Fanya lolote aguswi jibu ni Bashite kwaiyo kama musiba analopoka na aguswi ina maana musiba anatumika na kina Bashite, over
 
..unakumbuka kauli ya Mzee Makamba kuwa wapinzani watabatizwa kwa moto?

..sasa mbona haya anayopitia yana ahueni kulinganisha na udhalimu wanaofanyiwa wapinzani?

..Mzee Makamba aache kudeka.

Cc tindo, BAK
Kuna watu wanamlea Musiba, hawajui madhara ya uamuzi wa kumtumia mtu akafanya fitina na ndani ya chama kimoja.

Majibu ya upuuzi wanaoufanya watakuja kuyapata, na bahati mbaya muda huo watakuwa hawana tena akili ya kutafakari maono ya kipumbavu waliyoamua kuwa nayo vichwani mwao.
 
Kuna mtandao fulani umezaliwa ndani ya awamu ya tano, hauna nguvu ndani ya CCM, una nguvu katika mawasiliano binafsi ya nje ya chama.

Ni mtandao mbaya kama ule wa enzi za JK na mzee wa Monduli, kwani siku zote mnapounda kundi ndani ya kundi hamuwezi kuwa na ile roho ya umoja, mtaongozwa na ubinafsi uliojificha.

Lakini iwapo Mungu aliweza kuwafanya watu wa Babeli wakaongea lugha tofauti japokuwa ni wamoja, hatashindwa kuusambaratisha huu mtandao mpya wenye kufurahia kuona mtu fulani akiwa anateseka (sadism).
 
..lakini si afadhali ccm hamtekwi wala kuumizwa?

..Mzee Makamba na Kinana hawajapitia udhalilishaji na ukatili wanaopitia viongozi wa cdm.

..hawajawekwa lockup kiuonevu, hawashtakiwi kwa kesi zisiziokuwa na msingi, hawajaharibiwa mali zao, hawajapigwa mabomu ya machozi, hawajashambuliwa kwa risasi.

..hayo anayofanya Musiba is nothing compared to mambo yanayofanywa na ccm, polisi, mahakama, na bunge, dhidi ya wana Cdm.

..Waswahili walisema, " MKUKI KWA NGURUWE, KWA BINADAMU MCHUNGU."
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom