Nawapenda rafiki zangu kuliko ndugu zangu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawapenda rafiki zangu kuliko ndugu zangu.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Husninyo, Dec 22, 2010.

 1. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ndugu wengi ni watu wa lawama, hawana jema jamani. Hawawezi kukufanyia zuri na zuri utakalowafanyia wewe hawana shukrani nalo.
  Wengi ni wasiopenda kuona unafanikiwa hata sijui kwanini.
  Kuwasiliana au kuonana ni hadi kwenye matukio eg msiba au harusi.
  Wale waliofanikiwa huwa ni wenye kujisikia na wale wenye hali za chini hujiona dhaifu.
  Jamani mnafanyaje kukabiliana na ndugu wa aina hizo?
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hongera. Ukipata rafiki wa kweli umepata tunu. Ndugu wengi kwa hakika wana mauzauza. Wana wivu, husuda, ukiwasaida whawaoni kipya kwani wanaona ni haki yao. Ndugu huumizana (rejea Abeli na Kaini; Yusufu na nduguze = wana wa Isaka, nk katika maandiko matakatifu) na kutendeana kila aina ya uovu.
   
 3. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa uyasemayo. Mi nimefika point ambayo nikiwa na inshu inanitatiza ushauri nitauomba kwa rafiki,ndugu nitamjulisha tu juu ya maamuzi yangu kama itabidi sana. Nashukuru Mungu nina rafiki ambao ni yaidi ya ndugu.
   
 4. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hujatueleza ni ndugu wa vipi! Shangazi, mjomba binam, bibi au wakuzaliwa nao? sikatai kuna wanandugu hawafai. Lakini kumbuka ndugu hasa wa damu hata ukilost hawata kutupa lakini ni bahati sana kupata rafiki wa hivyo. Nina uzoefu na marafiki na ndugu walio fanya mambo ya ajabu na mazuri. Tueleze kategori ya ndugu unao maanisha
   
 5. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Haya mambo hayana fomula YEYOTE AWEZA KUTOSA ndugu au rafiki
   
 6. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Let me tell you one thing: Unawependa ndugu zako bali rafiki zako unawafurahia. Mungu ndio anatupenda sisi wanadamu, no matter tunamkosea vipi lakini upendo wake kwetu bad upo. Wengine tunafurahiana tu na si kupendana, unadai unampenda mkeo kwa sababu anakufurahia, anakupikia, anakuliwaza wakati wa huzuni, haya asipoyaonyesha upendo unaisha na unatafuta nyumba ndogo ili uyapate. Upendo hauna kikomo, sie twafurahiana na hatupendani!
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  ndugu wote ukiacha wa kuzaliwa nao tumbo moja.
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mi nafikiri kupenda na kufurahia vinaendana pamoja.
  Hivi unaweza ukakifurahia kitu wakati hukipendi?
  Au unaweza ukakipenda kitu huku haukifurahii?
  Labda unieleweshe zaidi juu ya hilo.
   
 9. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Upendo hauna kikomo
  Furaha na upendo ni vitu tofauti
  Mvuta sigara anapenda kuvuta sigara au anafurahia tendo la kuvuta sigara?
   
 10. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kwa hilo lisikuu mize kichwa hapo nakuunga mkono 61% Unachotakiwa
  1. Ishinao kimjini mjini
  2. Watu wapo busy na kuonana ni kwenye matukia ni sawa
  3. Kama upo Dsm foleni inasababisha watu wasitembeleane/inatia uvivu
  4. '' '' Kupanda daladala kunachosha (kwa asiye na gari)
  5. Acha mtindo wa kutafutiana viwanja jirani na unapoishi Sio lazima wote muishi kimara nk
  6. Unapoishi mbali heshima na upendo vinaongezeka
  7. Ukifuata hayo utapendana na hao ndugu japo kwa hizo 61%
   
 11. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mmmh! Hata sijui. Kama kuna mvutaji humu atatujibu.
   
Loading...