Nawamegea tu: CUF na UKAWA kwa ujumla, piganieni demokrasia ndani CUF

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Leo sitaji wala kumnyoshea kidole kama ngole yeyote kwa tafrani iliyotokea kwenye mkutano wa CUF pale Ubungo Plaza. Nawasihi na kuwapa moyo wanaCUF na wanaUKAWA kwa ujumla kuipigania demokrasia chamani CUF.

Kifanyike chochote halali uchaguzi ufanyike CUF. Kukwama kwa CUF ni kukwama kwa UKAWA na upinzani kwa ujumla. CUF ikipata doa lisilo na dua,wapinzani wote watachafuka. Wapinzani mlio kwenye UKAWA,CUF is now your burden. Hamna nafasi ya kuikwepa. Wahini kabla mambo hayajawa mengi.

Walio nyuma ya mkwamo wa CUF watapambana zaidi. Watapambana kwakuwa wana lengo. Wana lengo la kuweka pengo. Watapambana hadi kieleweke na wacheke. Waliowekwa mbele mnawajua. Walio nyuma ya hilo mtawajua. Leo nimewamegea tu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Huyu prof amuulize Lyatonga alipita uvunguni mwa meza Tanga kunusuru maisha yake
 
Umeongea ukweli mtupu, kinachofanywa hapa na CCM katika juhudi zao za kuidhoofisha CUF ni kuua ndege wawili kwa jiwe moja na hivyo wakiweza kuidhoofisha CUF watakuwa pia wameidhoofisha UKAWA. UKAWA isikae kimya kuhusu hizi juhudi kubwa za CCM ili kuleta mtafaruku mkubwa ndani ya CUF.
 
hiyo mambo yote ni ccm ndio wanaopika na kusuka njama kamwe hawatafanikiwa kwa kuwa
CUF wanaongozwa na katiba.

swissme
 
Lengo la kukivuruga CUF ina malengo mawili moja ni kupunguza nguvu ya upinzani na suala la znz,

nimewaona wale wafuasi waliohojiwa leo itv wanaonyesha lengo lao siyo kudai lipumba kurudi ila ni kukiua chama cha CUF kwa kukigawa cuf bara na CUF znz ikitokea hilo cuf inapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa na kufutwa rasmi,

na kikifutwa suala la madai ya seif kupokonywa ushindi litakuwa limekufa kwa hiyo znz itaanza kupokea misaada kama kawaida, ndiyo maana serikali ya Magufuli imediriki kuwanunua wajumbe karibu nusu wa CUF ili walifanikishe hilo kwa kumtumia lipumba
 
Swala la Lipumba limeshafungwa kwa kura 467 dhidi ya kura 14 hamna mjadala tena.
Maandalizi ya kuita mkutano wa uchaguzi yanafanyika now.
 
Back
Top Bottom