Nawalilia Seleli, Lembeli, Kimaro nk | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawalilia Seleli, Lembeli, Kimaro nk

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mrekebishaji, Aug 12, 2010.

 1. M

  Mrekebishaji Senior Member

  #1
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 168
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Inapokuja maswala ya kitaifa na si jimbo wala chama,baada ya kura za maoni ndani ya CCM najisikia uchungu sana nikikumbuka yale yaliyowapata SELELII,LEMBELI, KIMARO nk(wenye kupigania haki kama hao).

  Kuna wakati nilizungumzia umuhimu wa kuwa na wabunge wa kitaifa. kwa bahati mbaya, tumezoea mambo yale yale na hivyo sikushangaa nilipopingwa hoja yangu. Nalazimika kurzungumzia jambo hili mara ya pili.

  Hivi mnakumbuka umuhimu wa hao watu katika nchi hii kupitia michango yao bungeni; kwa mfano;

  1. Selelii ndiye aliyesimamia kidedea suala ya Richmondi akisaidiana na wana kamati wenzie. Selelii ndiye aliyesimama kidede kuwaambia mawaziri waangalie maslai ya nchi, na wakumbuke ipo siku nao watakufa, na akawakumbusha kuwa waangalie makaburi wataona ukweli kuwa wale walio katika makaburi nao siku moja walikuwa wazima.

  2. Lembeli na kimaro nao tumewaona katika michango yao, kwa sasa nisitoe mifano hiyo.

  HOJA:
  Katika imempa rais mamlaka ya kuteua wabunge kumi bila kubanwa na mgawanyo wowote ule. Je, ni kwa nini tusipiganie katiba hiyo hiyo iruhusu kuwa na wagombea ubunge kwa jimbo la KITAIFA(yaani wabunge wa kuwakilisha nchi na si jimbo fulani).

  Sababu.
  Kwa mfumo tulionanao, wale wapiganaji wa kupinga ufisadi, unakuta hawana fedha za kutosha kupeleka miradi katika majimbo yao na hivyo wakati fulani kujitkuta hawatoshelezi matakwa ya jimbo fulani wakati wanatoa mchango mkubwa kitaifa.(Si wakati wote kila jimbo litakuwa kama Kyela ambao wanaona fahari kuwa na mbunge mwenye maslai kitaifa zaidi pengine kuliko jimbo tu, na hivyo wakaamua kumpitisha(Dr. Mwakyembe).

  hivyo basi ifike hatua, tukute watu kama selelii, mpendazoe, kimaro, said Nkumba wanagombea jimbo la kitaifa lenye kuwa na pengine nafasi kumi. Na hivyo hata wakiingia bungeni wanamsemea mtanzania halisi bila kujali jimbo moja tu.

  Madhara yake tumeyaona, tubadilike.

  Nimerudia hoja hii, nitarudia tena popote. Mungu akipenda, nikiingia bungeni 2015 nitapeleka hoja binafsi ili tuwe na wabunge wasiobanwa na jimbo wala chama ili wananchi wote ndio wanampima.
   
 2. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Kama wameenguliwa kifisadi basi aje Chadema , nafasi ipo kwa makamanda kama hao.
   
 3. n

  njori Member

  #3
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo wanasiasa waliopevukia uzeeni wanatia aibu ktk nchi hii,unapoamua kuwa mwakilishi wa jimbo fulani hakikisha unatekeleza kwa vitendo mahitaji ya wananchi wako.unapoamua kwenda bungeni na kuingilia bifu za kumkandamiza fulani huku wananchi wako hawana maji safi,barabara zinazofikika,hosp/zahanati lazima wakumwage tu!!!!!!!maana hawatakuuliza bifu ngapi umefanikiwa?
  wanasiasa amkeni,vijana watawapiku kirahisi kama hamutekelezi walichowatuma bungeni
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Jamani vuvuzela letu Seleli hata kama unaona aibu chukua maamuzi magumu hamia upinzani kaendelee kupuliza vuvuzela lako ukitetea nchi tafadhali sana usingoje kiza kikaingia
   
Loading...