Nawalaumu wanaume wanaotelekeza watoto, japokuwa wadada mmezidi kutubambikia watoto

Manzile

JF-Expert Member
Apr 23, 2020
227
1,000
Habari ya mwaka mpya wakuu.

Mwaka 2013 nilienda field mgodi wa Bulyanhulu huko kakora uliokuwa unamilikiwa na Accacia, kwenye kivuko pale Busisi nikakutana na dada mmoja mrembo sana. Tukiwa tunasubiri kivuko kianze safari nikasogea karibu naye nikaanzisha mazungumzo na yeye yaliyopelekea kukaa siti moja baada ya kivuko kuanza safari.

Yule Binti wa Kisukuma, naye alikuwa anaenda field hospital ya Mkoa wa Geita, alikuwa bado mwanafunzi katika fani mojawapo ya afya. Ni mrembo haswa, anavutia machoni kumtazama, Ni miongoni mwa wasichana warembo sana. Yeye alishukia Geita mimi nikaendelea na safari na kwa bahati nzuri tukawa tumebadilishana mawasiliano, na baada ya miezi kadhaa tukawa wapenzi.. Kiukweli huyu dada nilimpenda sana ni mwanamke ambaye niliweza kumfanyia kila kitu alichokuwa akiniambia.

Mwaka uliofuata mimi nilihitimu chuo huku nikiwa najishugulisha zaidi na miradi ya familia. Siku moja mzee wangu aliniita baada ya chakula cha jioni akaniambia maneno ambayo alipenda kunieleza siku zote lakini kwa siku ile yalikuwa na uzito na alikuwa serious kuliko siku zingine mbele ya ndugu wengine wa kifamilia waliokuwepo.

Kimsingi, mzee wangu alikuwa ananikumbusha matamanio yake kwangu kwa vile mimi ndio mtoto wa pekee wa kiume kwake. Alitaka kuona mimi kijana wake niko katika mahusiano ya kueleweka au nioe kwa vile tayari alishaniwezesha kichumi na kunipa majukumu ya kusimamia miradi ya kifamilia pamoja na mambo mengine alitaka kuona naanzisha familia nikiwa bado kijana. Hapa ndipo wazo la kuoa likanijia, na mtu wa kuoa alikuwa ni huyu binti wa kisukuma.

Nikamueleza dhamira yangu ya kumuoa yeye, akasema nimsubiri amalize chuo kwangu haikuwa tatizo, nikasubiri huku mapenzi yetu yakiendelea na hapa akawa na mawasiliano na wazazi wangu kama mke wangu mtarajiwa, lakini mimi sikubahatika kuwa na mawasiliano na watu wa kwao mara kadhaa aliniambia nisubiri kwanza amalize, kwa vile yeye ni mtoto wa kike na bado alikuwa chini ya himaya ya mzazi wake nilimuelewa.

Kipindi anamaliza chuo, mimi sikuwepo hapa nchini na cha kushangaza simu zake zikawa hazipatikani na nilipowauliza wazazi wangu labda kama anawapigia wakasema hata wao hawampati, niliporejea nilimtafuta nikampata, nilipomuelezea kuwa sasa ni mda muafaka wa kuishi kama mke na mume akakasema yeye anaona ni vema nimsubiri apate kazi lakini tuendelee kuwa wapenzi. Ushawishi wangu wote kwake ukagonga mwamba na hayo ndiyo yalikuwa majibu yake ya mwisho.

Kuna siku nilikuwa na safari ya Mwanza nikamtaarifu lakini cha ajabu nafika Mwanza simu zake zote hazipatikani akaja kunitfuta baada ya wiki nimeshaondoka kwa kutumia namba ya rafiki yake, kwa vile alikuwa mwanamke niliyempenda sana sikuwa na maneno mengi kwake zaidi ya kumwambia nitakuwa na safari nyingine ya huko siku chache zijazo.

Nilivorudi tena akawa hapatikani, nilikuwa na namba ya rafiki yake aliyonitafuta nayo kipindi cha nyuma, nikamtafuta ili anijuze nini kimempata huyu mpendwa wa moyo wangu naye hakuwa na mawasiliano naye kama wiki hivi. Nikamuomba nionane nae akanikatalia, siku 3 nahangaika kumshawishi tukutane na lengo langu ilikuwa kumuuliza kuhusu rafiki yake ambaye ni mpenzi wangu ana matatizo gani. Baada ya kunikubali kuonana nae akakataa kuzungumza chochote juu yake.

Mwaka ukapinduka, tukaingia 2015 Rais ni magufuli bado anasubiri ajira ili nimuoe, mimi nikaona isiwe shida nikaanza kumchombeza rafiki yake akawa hanielewi kabisa alidhani nia yangu ni kuwachanganya yeye na rafiki yake kwenye kapu moja la mapenzi. Lakini kama ilivo hakuna mkate mgumu mbele ya chai.. Akalainika na nikaoa baada ya miezi kadhaa. huyu nilioa bila kumjua radha yake yaani siku naona ndio navua chupi hapa mpaka leo najishangaa ni nini kilitokea, nikakata mawasiliano na msukuma wangu.

Alikuja kujua kwamba nimeoa rafiki yake wa karibu baada ya mwaka kupita, alianzisha vurugu isiyoumiza mpaka kwa wazazi wangu , Baadae ilibidi atulie maana hakukuwa na namna mwaka 2018 alinitafuta akidai anataka kuonana na mimi, amemisi mahaba yangu. Kwa mapenzi niliyokuwa nayo kwa huyu mwanamke sikuwa na jinsi nikapanga safari nikaaga kwangu nikamtumia nauli tukakutana Kampala, hii ilikuwa mwezi wa pili 2018 na hapa ndo Sekeseke lilipoanza

Baada ya wiki mbili tangu tulipoachana Kampala, akadai kwamba ana mimba yangu binafsi sikukataa nikawa nahudumia kwa vile ukiachana na mambo mengine nilikuwa na mapenzi ya dhati kwake. Mwezi wa saba mwanzoni ananipigia simu kajifungua, hapa nikaanza kuona maluweluwe, nikamuuliza kama mtoto ni njiti, akasema hapana.

Nikamuambia palepale huyo mtoto sio wangu. Akaniwakia kama mwewe kwamba natelekeza mtoto na maneno mengi ya kashfa. Japo nilihudumia mimba lakini kwa hapa wakuu nimenyoosha mikono, Dunia hii wapi ambapo watoto wanazaliwa kwa mimba ya Miezi mitano kasoro?.

Sasa kaanzisha Twimbili lingine lisiloumiza anawapigia wazazi wangu kuwaambia nimetelekeza mtoto.

Jana nimekuta ujumbe What'sApp akidai anataka kuishi na mimi na yuko tayari kuwa mke wa pili, anataka nimjengee nyumba na gari kwa ajili ya mtoto. alivoona sijibu akaendelea kama nitaendelea kumtelekeza mtoto ataenda kwenye sheria ili niwajibike huko.

Nikiri kwamba huyu ni mwanamke niliyekuwa nampenda na nilikuwa na Dhamira ya kweli kwake na yeye akatumia uzuri wake kama ngao na kibaya mpaka sasa hajapata ajira na mimi tayari niko kwenye ndoa na rafiki yake wa karibu na tuna watoto wawili. Ningeweza kufanya chochote juu yake lakini kwa hili la mtoto naona kama nabambikiwa.

Inawezekana mtoto kuzaliwa akiwa na miezi mitano kasoro dunia hii wakuu?
 

Manzile

JF-Expert Member
Apr 23, 2020
227
1,000
Asikuumize kichwa huyo malaya, naona kiuchumi upo vizuri muite mkapime DNA baada ya hapo piga block usimchekee kabisa huyo mwanamke naona ni muuaji na usipokua makini atakuharibia familia yako uliyo nayo sasa...
Hili ndilo la msingi japo anakwepa sana
 

MPOKEA KODI

Member
Apr 1, 2020
78
125
Asikuumize kichwa huyo malaya, naona kiuchumi upo vizuri muite mkapime DNA baada ya hapo piga block usimchekee kabisa huyo mwanamke naona ni muuaji na usipokua makini atakuharibia familia yako uliyo nayo sasa...
Usisahau kumwambia anapo kwenda kupima DNA aende kupimia nje ya nchi...
 

Ing'ang'a

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
1,758
2,000
Kaka Umezingua mwenyewe ujue
Toka alivyozingua basi ungemkaushia mazima
Umemlea mwenyewe alivojirudi ukamgonga.

Yule mdada anajua unampenda na yeye ni mrembo
Hvo anajua kila atakachofanya wewe unafata
Wee una pesa Bhana Afu mapenzi yataanzaje kukutesa
Switch off mapenzi yasiyoeleweka

Una hela Afu unageuka Marioo ??!!
Lia Lia .
Umeona sasa anaenda kwenye Dawati na utaitwa japo ikifika wakati timbeni hospital Uelekeo kwenye DNA ndo jawabu.
Demu Ana njaa , mwaka wa Sita bila bila NO Ajira Baba hatari.

KAZA.
 

Manzile

JF-Expert Member
Apr 23, 2020
227
1,000
Kaka Umezingua mwenyewe ujue
Toka alivozingua basi ungemkaushia mazima
Umemlea mwenyewe alivojirudi ukamgonga.

Yule mdada anajua unampenda na yeye ni mrembo
Hvo anajua kila atakachofanya wewe unafata
Wee una pesa Bhana Afu mapenzi yataanzaje kukutesa
Switch off mapenzi yasiyoeleweka

Una hela Afu unageuka Marioo ??!!
Lia Lia .
Umeona sasa anaenda kwenye Dawati na utaitwa japo ikifika wakati timbeni hospital Uelekeo kwenye DNA ndo jawabu.
Demu Ana njaa , mwaka wa Sita bila bila NO Ajira Baba hatari.

KAZA.
Nafsi yangu ilimpenda sana huyu mwanamke.
 

Yna2

JF-Expert Member
Aug 18, 2018
22,236
2,000
Kama ungejua mtoto ni wako ungeweza fanya chochote juu yake.. hata kwa kumuoa mke wa pili kama alivyotaka??🙄
 

Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
10,152
2,000
Mwambie muende kupima DNA. Huyo mtoto si wako mwambie aende kwenye Sheria halafu huko waombe wawaamuru muende dna ndo muendelee na shauri lenu. Atakimbia
 

Shamkware

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
1,164
2,000
Mkatae kabisa huyo mtoto sio damu yako unaibiwa saana kama atabisha si kapime nae DNA tu laki tatu haiwezi kukushinda mkuu wanawake kama hao sio wa kumdekeza kihivyo brother..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom