Nawakumbusha tu, mipaka mingi imefungwa,tusiitie kiberiti nchi yetu

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
4,722
2,000
Amani iwe nanyi,

Nafuatilia mienendo ya wanasiasa, wasimamizi wa siasa na wananchi katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu, naona kama kuna hali ya kuchoshwa na amani iliyopo sasa. Vitendo vingi vinaashiria pande hizi haziko tayari kutenda haki au kuona haki inadhulumiwa.

Nikiwa kama mtanzania mpenda amani, na mwenye vitu vingi vya kupoteza, naomba niwakumbushe kwamba kwa sasa sisi watanzania hatukubaliki kwa sababu hatuku- handle issue ya corona kwa namna jamii ya kimataifa ilivyotaka. Mipaka mingi ni kama imefungwa na hakuna regular commercial airlines. Tukiitia kiberiti nchi yetu sasa tutakua wageni wa nani?

Aidha, ni jambo ambalo halikubaliki kuiweka nchi yetu rehani kwa mambo ambayo hayana umuhimu au yenye viashiria vya uroho wa madaraka. Maslahi mapana ya nchi yetu yatamalaki. Mwenye haki apewe na aliyenyimwa haki aitafute haki yake kwa njia ya amani.

Eventualities za machafuko ni nyingi na hakuna anayejua for certain fate yake itakuaje. Narudia kukumbusha huu si wakati sahihi sana wakuitia kiberiti nchi yetu
 

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
7,899
2,000
MUNGU YUPO NA ANAENDELEA VIZURI NA KAZI
Screenshot_20200909-071320.jpg
 

mtanganjia

JF-Expert Member
May 19, 2018
1,182
2,000
Wewe kwaiyo na sisi rokudown ili tukubalike kama nchi zingine
au wewe kiongozi ulikua una ushauri gani
 

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
4,722
2,000
Siyo wakati sahihi wa kuitia nchi kiberiti haya twambie wakati gani sahihi tuitie kiberiti?
Nchi hii imekauka sana kiberiti kinaitamani .
Wakati ambapo jamii ya kimataifa iko active na inaweza kuingilia na kutoa humanitarian aids, tujifunze post elections violance za Kenya na genocide ya Rwanda utapata picha
 

maiyanga1

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
933
1,000
Waliopo madarani wameshika kibiriti, majani yamenyauka, hawana Cha kupoteza, wameshajilimbikizia vya kutosha nje ya nchi kupitia miradi isiyopitia bungeni, na kupitishia fedha kwa mmasai kwa geresha ya kununua madini.
 

Ugobha

JF-Expert Member
Jul 18, 2020
342
1,000
Wakati ambapo jamii ya kimataifa iko active na inaweza kuingilia na kutoa humanitarian aids, tujifunze post elections violance za Kenya na genocide ya Rwanda utapata picha
Hii nchi ilipofika haiwez kupokonywa urais kwa ushindi wa vikaratasi,
hili nakwambia kwa faida yako wewe mwenye vingi vya kupoteza hamisha mapema au uza mali zako uwape maskini.
 

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
4,722
2,000
Hii nchi ilipofika haiwez kupokonywa urais kwa ushindi wa vikaratasi,
hili nakwambia kwa faida yako wewe mwenye vingi vya kupoteza hamisha mapema au uza mali zako uwape maskini.
Phrase "vitu vingi vya kupoteza" isitafsiriwe kipekee kuwa ni mali tu, zakuhamishika au la, ni pamoja na ndugu jamaa na marafiki, wake na michepuko,pamoja na bata na shangwe.
 

pumzihaiuzwi

JF-Expert Member
Mar 27, 2015
2,919
2,000
Bwana asipo ulinda mji walindao wakesha bure amani na wapa amani nawaachia, heri hao wanaopenda amani na kuchukia maovu, tafakuri nyumba hii ipo juu ya mchanga au msingi imara?, mtu hawezi kutoa chakula cha wanae cha akiba na kuwalisha mbwa, ole wao wale wanaopenda visasi na machafuko, Mungu ibariki Tanzania ,Mungu ibariki Africa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom