Nawakumbusha tu al shabaab 700, nchunga alishinda kwa kura 1,437 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawakumbusha tu al shabaab 700, nchunga alishinda kwa kura 1,437

Discussion in 'Sports' started by nngu007, May 22, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=3][/h][​IMG]

  ETI wanachama 700 wa Yanga walikutana Jumapili makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kufikia uamuzi wa kumngÂ’oa madarakani Mwenyekiti, Wakili Lloyd Bahargu Nchunga.
  Mapinduzi haya yaliongozwa na Mzee Ibrahim Akilimali, ambaye kihistoria nilishasema siku nyingi ni mzee kinara wa migogoro na mvuruga amani klabuni.


  Kweli, Nchunga ameshindwa kuongoza Yanga na sababu kubwa ni uelewa wake mdogo katika masuala ya michezo na kukosa ushirikiano kutoka kwa Wajumbe wenzake wa Kamati ya Utendaji na wadau wengine wa klabu, wakiwemo hao wanaojiita wazee.

  Lakini ukirejea uchaguzi uliomuweka madarakani Nchunga Jumapili ya Mei 18, mwaka 2010, alishinda Uenyekiti baada ya kupata kura 1,437, akiwaangusha wapinzani wake wanne, Francis Kifukwe aliyepata kura 370, Mbaraka Igangula aliyepata kura 305, Abeid Falcon aliyepata kura 301 na Edgar Chibura aliyeambulia kura 65 katika kura 2,220 zilizopigwa, wakati kura 23 kati ya hizo ziliharibika.


  Kura 370 za Kifukwe na 305 za Igangula kwa pamoja wakichanganya, bado hawawezi kufikia kura za Nchunga- ina maana alishinda kwa kishindo. Inakuwa rahisi kuhisi watu hawa 700 waliokutana Jumapili ni wale wale 700 waliomnyima kura Nchunga PTA Mei 18, 2010.


  Sitaki kuzama ndani sana- kwa sababu nimeshapitisha sera ya kutoandika habari za migogoro- lakini kwa pamoja na wasomaji wangu napenda tujadili, kiongozi aliyeshinda kwa kura 1,437 anaweza kungÂ’olewa madarakani na watu 700?


  Tena watu ambao hakuna aliyewahakiki kama kweli ni 700 na hakuna aliyehakikisha kama kweli ni wanachama wa Yanga? Tujadili.


  [​IMG]
  LLOYD NCHUNGA


  [​IMG]


  MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI YA YANGA, RIDHIWAN KIKWETE AKITANGAZA MATOKEO MEI 19, 2010, KULIA NI MFADHILI WA KLABU HIYO, YUSUF MANJI

  [​IMG]


  MAKAMU MWENYEKITI, DAVIS MOSHA AKITOA SHUKURANI KWA WANACHAMA

  [​IMG]


  SARAH RAMADHAN ALIYESHINDA UJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI

  [​IMG]


  ALLY MAYAI TEMBELE ALIYESHINDA UJUMBE

  [​IMG]


  CHARLES MUGONDO ALIYESHINDA UJUMBE

  [​IMG]


  THEOFRID RUTASHOBORWA (SASA MAREHEMU) ALIYESHINDA UJUMBE

  [​IMG]


  SALIM RUPIA ALIYESHINDA UJUMBE

  [​IMG]


  MZEE YUSSUF ALIYESHINDA UJUMBE


  [​IMG]


  MOHAMMED BHINDA ALIYESHINDA UJUMBE
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Huyu Mzee Ibrahim Akilimali kiongozi wa Al-Shaabab ndio kinara wa Miogomvi yote Yanga; Hana pesa lakini anailetea Timu

  Matatizo kila Mara na wakati kwanini Wazee ndio wanotulea Matatizo kwenye Klabu zetu za Simba na Yanga?

  Hizo katiba lazima zibadilishwe tuwe na Wakurugenzi, Marais kama Clabu za Uingereza - Wanachama Wapo wanasikilizwa

  Lakini hawana Nguvu ya Kuivuruga Vuruga Timu kiasi hicho na Hawana Pesa za hata kuwalipia Chakula
   
 3. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mtoa mada hapo kwenye RED ndo panapotuhusu wana'Yanga,na huo ndo msingi mkuu wa mgogoro huu ndani ya Club ya Yanga,ni kweli katiba haikufuatwa katika mkutano ule uliojaribu kumpindua Bwana Nchunga lkn hata Nchunga mwenyewe pia hafuati katiba kwa kung'ang'ania madaraka ilhali anaona kabisa kuwa kazi imeshamshinda na waliokuwa wasaidizi wake wote wamepiga chini,hivi yeye Nchunga anajisikiaje akiingalia hali iliyoko katika Club kwa sasa hivi? Pia napenda kumkumbusha mleta mada kuwa kwenye uchaguzi uliomuweka bwana Nchunga madarakani bwana Kifukwe alisha'withdraws jina lake dakika chache kabla ya kura kupigwa baada ya kuona zengwe la wazi lililokuwa likiendeshwa na huyo bwana mkubwa aliyevaa koti la draft ndogondogo na huo ndo msingi mkuu wa kupata kura chache kwani ilibidi baadhi ya kura zilizokuwa ziwe upande wake ziangukie kwa Nchunga aliyekuwa anapigiwa chapuo na huyo bwana mkubwa niliyemtaja hapa juu.
  Kwa mtazamo wangu bwana Nchunga hana washauri wazuri,nasema hivyo ksbb yeye pamoja na washauri wake walitakiwa wapime athari za kung'ang'ania kwake madaraka kwa team na kuchukua maamuzi,kama kina Mayayi,Rupia,Mzee Yusuph na wengineo wamepima na kuchuka maamuzi why not him,kwanini ang'ang'anie pale,pana nini? embu tutafakarini pamoja jamani.
   
Loading...