Nawakumbusha kuweka matumaini kwenye humanity zaidi, haya mataifa yanakuja na kutoweka, siyo mamlaka za kudumu za kiutawala

CreativityCode

Senior Member
Aug 8, 2020
118
1,000
Shalom,

Wengi mnaweza msinielewe, hasa wale nationalists, lakini napenda kuwakumbusha tu kuwa kabla ya 1950 Afrika hakukuwa na mataifa ya Tanzania, Rwanda, Uganda, Kenya n.k

Lakini pia kabla ya July 4, 1776 hakukuwa na taifa la Marekani, Canada kama taifa halikuwepo kabla ya July 1, 1867 n.k

Dola la Rumi liko wapi? kuna mtu alifikiria litatoweka? Ottoman Empire je?

Kwa ufupi utaifa siyo dhana ya kudumu. Je, umewahi kujiuliza kama Tanzania itakuwepo baada ya miaka 100 ijayo?

Sina maana ya kuikana asili yangu lakini nadhani ni vema tukafikiria kwa mapana zaidi kuhusu ubinadamu ama humanity kuliko dhana ya utaifa ambayo kwa uhakika ni ya kufikirika zaidi yaani imaginary entity.

NI VEMA KUWAPENDA WATU WOTE DUNIANI NA KUISHI KAMA RAIA WA DUNIA NA SIYO WA TAIFA MAHSUSI.

WEEKEND NJEMA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom