Nawakubali mawaziri wa Muungano Kutoka Zanzibar

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
- Vua Nahodha
- Hussein Mwinyi
- Saada Mkuya

Mnatoa hoja kwa utulivu na mna-stick to the point!

Asanteni kwa Kutuwakilisha waZanzibar - Kasheshe Kutoka Bububu
 
Husein Mwinyi ni Mzanzibar, anawezaje kuwa waziri kwenye wizara ambayo haihusiani na mambo ya Zanzibar kwenye JMT? Hivi kuna Mtanganyika anaweza kwenda kuwa Waziri wa Afya Zanzibar?
 
Ndugu hatuna serikali ya Tanganyika. Mzanzibar yeyote anaweza kuwa kwenye taasisi yoyote ya JMT!
 
Huu ni udhaifu mkubwa wa katiba yetu kama sisi hatuwezi kuhudumu SMZ. Kwa nn wao waruhusiwe huku bara?
 
Hawa Wazanzibar waliojichimbia huku Tanganyika ni ngumu kuwarudisha huko Visiwani. Maana miaka siyo mingi hivyo Visiwa vitajaa watu, hasa ukizingatia Wapemba wanvyozaa haraka haraka.
 
Husein Mwinyi ni Mzanzibar, anawezaje kuwa waziri kwenye wizara ambayo haihusiani na mambo ya Zanzibar kwenye JMT? Hivi kuna Mtanganyika anaweza kwenda kuwa Waziri wa Afya Zanzibar?
mkuu unashangaa hilo? Mbona zanzibar inaitawala tanganyika kisiri?
 
Hawa Wazanzibar waliojichimbia huku Tanganyika ni ngumu kuwarudisha huko Visiwani. Maana miaka siyo mingi hivyo Visiwa vitajaa watu, hasa ukizingatia Wapemba wanvyozaa haraka haraka.
Jamani visiwa vyetu pemba na unguja vyaweza zama majini miaka 200+ ijayo sasa mnategemea wajukuu wetu waishi wapi?
 
Binafsi naunga mkono, tatizo linaanza huku bara, mawaziri ni ufisadi na majivuno kwa kwenda mbele! Kina kawamba,ghasia, pinda na wengineo, ni porojo na propaganda kwa kwenda mbele, ufanisi ni sifuri!
 
Tanganyika ndio yenye kuitawala ZANZIBAR tena sio kisiri kila mtu anajua hilo.
 
Husein Mwinyi ni Mzanzibar, anawezaje kuwa waziri kwenye wizara ambayo haihusiani na mambo ya Zanzibar kwenye JMT? Hivi kuna Mtanganyika anaweza kwenda kuwa Waziri wa Afya Zanzibar?

kwao mkuranga
 
Huu ni udhaifu mkubwa wa katiba yetu kama sisi hatuwezi kuhudumu SMZ. Kwa nn wao waruhusiwe huku bara?

Mbona hufahamu swahiba? Hakuna serikali ya BARA wala TANGANYIKA, tatizo nini sasa? Serikali ilokuwepo ni ya Jamhuri ya muungano wa tanzania, hii ni serikali yetu sote kwa pamoja, kisha sisi tukaweka serikali yetu, si unajua mke akiolewa tena jina lake ndo basi la mume linabaki, sema ndo ivo mume ----- tu.
 
Mpende msipende mawaziri wa Muungano wa asili ya Unguja na Pemba a.k.a Zanzibar ni wachapa kazi... hawana kashfa... sio mzigo.... Kudos Mwinyi, Nahodha, Saada, Mbarawa, Samia mnatuwakilisha vizuri... Waonyesheni inawezekana kuwa waziri bila kuwa mlafi!!! indeed our next VP wa JMT ni .... ni Mh. Nahodha!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom