Nawahabarisha mambo kadhaa...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Wapendwa wana JF na Wasikilizaji wa KLH News,

Napenda kutumia nafasi hii kuwapa taarifa za mambo mbalimbali ambayo nimekuwa nikiyafanya na ambayo yana maslahi na wadau wengi hapa. Mambo haya ni yale ambayo aidha yamejadiliwa humu au nimewahi kuwapasha habari zake.

a. Suala la vijana Ukraine:

Suala la wanafunzi waliokwama Ukraine limefikia hatima yake, ingawa ni hatima ambayo mimi binafsi na wazazi wengi wa vijana hawakuitarajia. Tarehe 15 Septemba kundi la mwisho la wanafunzi waliokuwa Ukraine liliwasili nyumbani baada ya kuingia mkopo wa tiketi na deni lao "kushughulikiwa" na serikali. Kati ya wanafunzi wote 29 wachache walikwisha acha masomo, wengine walijirudisha wenyewe baada ya serikali kugoma kabisa na kundi hilo la mwisho ambalo hatimaye lilipatiwa tiketi na kuondoka Ukraine.

Ni mmoja tu ambaye hakuweza kuondoka kutokana na uzito wa ushiriki wake katika suala hili zima na hisia kuwa kwa vyovyote vile kurudi kwake Tanzania ingekuwa ni kushindwa kwa jitihada zote za kuhakikisha anaendelea na masomo. Huyo mwanafunzi mmoja kwa msaada wa wadau wa hapa JF tumeweza kuhakikisha amehama toka Chuo Kikuu alichokuwapo na kwenda chuo kingine ambapo familia yake wameahidi kujitahidi kumwendeleza na masomo kama tungewapa tafu kwa mwaka huu.

Tulifanya hivyo na ninashukuru wale ambao tuliwasiliana chemba na ambao waliitikia wito wangu.

Nashukuru kwa namna pekee serikali kwa ushirikiano walioonesha hasa baada ya kuamua kufanya mazungumzo ya chini kwa chini ambayo yaliwezesha vijana hawa kurudi nyumbani na zaidi ya yote kupewa nafasi nyingine ya kuendelea na masomo. Ingawa bado tuna issue ya wanafunzi wachache ambao tunaendelea kushughulikia ni matumaini yangu kuwa serikali hatimaye itaamua kuwasamehe deni la tiketi ambalo walitakiwa kulipia ndani ya miezi sita.

Mke wa Bob
Kwa wale wanaokumbuka mapema mwaka huu nilijitahidi kumuunganisha binti wa Kizambia ambaye alikuwa ameolewa na Mtanzania na waka wanaishi Angola. Mapema mwaka huu kijana huyo Bob alifariki dunia akitanguliwa na mtoto wake wa miaka kama mitano hivi.

Alipofariki mkewe alikuwa haijui familia ya marehemu na walikuwa wamepanga kwenda Handeni baadaye mwaka huu. Hivyo kijana huyo alizikwa Angola pasipo taarifa kwa wazazi wake au ndugu yeyote Tanzania. Ndipo jambo hilo likanifikia na kwa kutumia contactz zangu tukaweza kupeleka habari za msiba nyumbani kwa Marehemu na nikaweza kuwaunganisha mke wa marehemu na wazazi kwa njia ya simu na hatimaye kuwezesha mpango wa binti huyo kwenda kuwatembelea huko Handeni katikati ya mwaka huu.

Kwa hili namshukuru sana Mbunge wa Handeni Dr. Abdalah Kigoda kwa ushirikiano wote alionipa, na milele moyo wangu umejaa shukrani.

Ujumbe kwa Watanzania
Mapema mwaka huu pia kutokana na mjadala wa "Kuanguka kwa CCM, Unabii Utatimia" lilitolewa wazo la kuandika ujumbe ambao ungeweza kuelekezwa kwa Watanzania wote na ambao utakuwa na nguvu zaidi kuliko Makala ile ya awali. Ujumbe huo umekamilika na uko kwenye uhariri na utatolewa kabla tu ya kuanza kwa mkutano mkuu wa CCM.

Tovuti ya KLH News
Kama mnakumbuka katika mada ya "KLH Kufungwa" nilielezea ugumu unaonipata katika kufanikisha majukumu mbalimbali niliyojitwika ya kuwaletea maoni na habari na katika kutimiza dhana ya "hoja hujibiwa kwa hoja" na ya kuwa kwenye KLH News hapendwi mtu, hapendelewi mtu na haogopwi mtu.

Mwitiko wa wadau hapa umenitia moyo sana, wale ambao walitoa ahadi wachache wameshazitimiza na daima nawashukuru na wengine ambao ahadi zao bado ziko njiani ila kutokana na sababu mbalimbali wameshindwa kufanya hivyo hadi hivi sasa. Kwa wao natanguliza shukrani na pamoja nao navuta subira. Naomba watakaoweza kutimiza ahadi hizo wawasiliane nami kabla ya Novemba 10, 2007 kabla hatujafanya beta testing.

Nimeshapata wataalamu wa mambo haya ya kompyuta ambao kuanzia jana (tarehe 8 Oktoba) wameanza rasmi kufanyia kazi tovuti hiyo ambayo itakapokuwa tayari (matarajio ni wiki ya kwanza ya Novemba) itakuwa ni tovuti bora kabisa ya habari na maoni ya mambo mbalimbali kuliko tovuti nyingine yoyote ya Watanzania.

Lengo ni kuinua ubora wa tovuti za habari na kuziweka kwenye kiwango cha kimataifa. Matunda ya awali nimeanza kuyaona na ndugu zangu, I am impressed (and I don't get impressed easily).

Ninawashukuru
Nawashukuru wale wote ambao hadi hivi sasa wamewezesha kunipa taarifa, mawazo, maoni, ukosoaji na kusahihisha kila nilipopotoka. Natumaini tutaendelea hivyo tunavyoelekea mwisho wa mwaka. Muda ni mfupi lakini safari ni ndefu. Peke yangu siwezi na sitoweza licha ya kujitahidi sana, lakini kwa msaada wenu mambo mengi yanakuwa mepesi kufanyika.

Mniunge mkono na mimi nawaahidi sitawaangusha katika kila nifanyalo. Siwaahidi kutokosea, nawaahidi kuwa nikikosoea sitajificha au kuficha makosa yangu! Na nawaahidi siwezi kuanguka bila kusimama tena! Kwani kusimama nitasimama!

Hotuba ya Nyerere Mei Mosi

Katika kukumbuka miaka nane tangu Baba wa Taifa atutoke, Kuanzia kesho Jumatano (Oktoba 10) nitaanza kuwaletea sehemu ya hotuba ya Rais Nyerere aliyoitoa kwenye sherehe za Mei Mosi 1995 ambayo imebakia kama alama ya Nyakati. Kwa wale mlioangalia kipindi cha Jenerali on Monday mtakumbuka kuwa hata Prof. Beregu alinukuu toka kwenye hotuba hiyo.

NI hotuba ambayo kwa hakika ilionesha ni upeo na umahiri wa Mwalimu katika kujenga hoja. Kwa kadiri ninavyoisikiliza ndivyo kwa namna fulani naamini kuwa hotuba hii inaanza kunijenga kifikra kama zilivyofanya barua ya MLK na hotuba ya Mandela kizimbani. Natumaini mtachukua muda kusikiliza.

Na katika sehemu ya kumbukumbu hiyo natarajia kuwa na onesho maalum siku ya Jumapili kupitia bongoradio.com na natumaini kuwa na ugeni mkubwa kwenye show hiyo tunapoangalia nyuma na kumkumbuka Mwalimu. Nitawapa muda na jina la mgeni/Wageni pindi mambo yakitengemaa..

Ndugu yenu na Mtanzania mwenzenu,

M. M. M.
 
Wapendwa wana JF na Wasikilizaji wa KLH News,

Napenda kutumia nafasi hii kuwapa taarifa za mambo mbalimbali ambayo nimekuwa nikiyafanya na ambayo yana maslahi na wadau wengi hapa. Mambo haya ni yale ambayo aidha yamejadiliwa humu au nimewahi kuwapasha habari zake.

a. Suala la vijana Ukraine:

Suala la wanafunzi waliokwama Ukraine limefikia hatima yake, ingawa ni hatima ambayo mimi binafsi na wazazi wengi wa vijana hawakuitarajia. Tarehe 15 Septemba kundi la mwisho la wanafunzi waliokuwa Ukraine liliwasili nyumbani baada ya kuingia mkopo wa tiketi na deni lao "kushughulikiwa" na serikali. Kati ya wanafunzi wote 29 wachache walikwisha acha masomo, wengine walijirudisha wenyewe baada ya serikali kugoma kabisa na kundi hilo la mwisho ambalo hatimaye lilipatiwa tiketi na kuondoka Ukraine. Ni mmoja tu ambaye hakuweza kuondoka kutokana na uzito wa ushiriki wake katika suala hili zima na hisia kuwa kwa vyovyote vile kurudi kwake Tanzania ingekuwa ni kushindwa kwa jitihada zote za kuhakikisha anaendelea na masomo. Huyo mwanafunzi mmoja kwa msaada wa wadau wa hapa JF tumeweza kuhakikisha amehama toka Chuo Kikuu alichokuwapo na kwenda chuo kingine ambapo familia yake wameahidi kujitahidi kumwendeleza na masomo kama tungewapa tafu kwa mwaka huu.

Tulifanya hivyo na ninashukuru wale ambao tuliwasiliana chemba na ambao waliitikia wito wangu.

Nashukuru kwa namna pekee serikali kwa ushirikiano walioonesha hasa baada ya kuamua kufanya mazungumzo ya chini kwa chini ambayo yaliwezesha vijana hawa kurudi nyumbani na zaidi ya yote kupewa nafasi nyingine ya kuendelea na masomo. Ingawa bado tuna issue ya wanafunzi wachache ambao tunaendelea kushughulikia ni matumaini yangu kuwa serikali hatimaye itaamua kuwasamehe deni la tiketi ambalo walitakiwa kulipia ndani ya miezi sita.

Mke wa Bob
Kwa wale wanaokumbuka mapema mwaka huu nilijitahidi kumuunganisha binti wa Kizambia ambaye alikuwa ameolewa na Mtanzania na waka wanaishi Angola. Mapema mwaka huu kijana huyo Bob alifariki dunia akitanguliwa na mtoto wake wa miaka kama mitano hivi. Alipofariki mkewe alikuwa haijui familia ya marehemu na walikuwa wamepanga kwenda Handeni baadaye mwaka huu. Hivyo kijana huyo alizikwa Angola pasipo taarifa kwa wazazi wake au ndugu yeyote Tanzania. Ndipo jambo hilo likanifikia na kwa kutumia contactz zangu tukaweza kupeleka habari za msiba nyumbani kwa Marehemu na nikaweza kuwaunganisha mke wa marehemu na wazazi kwa njia ya simu na hatimaye kuwezesha mpango wa binti huyo kwenda kuwatembelea huko Handeni katikati ya mwaka huu. Kwa hili namshukuru sana Mbunge wa Handeni Dr. Abdalah Kigoda kwa ushirikiano wote alionipa, na milele moyo wangu umejaa shukrani.

Ujumbe kwa Watanzania
Mapema mwaka huu pia kutokana na mjadala wa "Kuanguka kwa CCM, Unabii Utatimia" lilitolewa wazo la kuandika ujumbe ambao ungeweza kuelekezwa kwa Watanzania wote na ambao utakuwa na nguvu zaidi kuliko Makala ile ya awali. Ujumbe huo umekamilika na uko kwenye uhariri na utatolewa kabla tu ya kuanza kwa mkutano mkuu wa CCM.

Tovuti ya KLH News
Kama mnakumbuka katika mada ya "KLH Kufungwa" nilielezea ugumu unaonipata katika kufanikisha majukumu mbalimbali niliyojitwika ya kuwaletea maoni na habari na katika kutimiza dhana ya "hoja hujibiwa kwa hoja" na ya kuwa kwenye KLH News hapendwi mtu, hapendelewi mtu na haogopwi mtu. Mwitiko wa wadau hapa umenitia moyo sana, wale ambao walitoa ahadi wachache wameshazitimiza na daima nawashukuru na wengine ambao ahadi zao bado ziko njiani ila kutokana na sababu mbalimbali wameshindwa kufanya hivyo hadi hivi sasa. Kwa wao natanguliza shukrani na pamoja nao navuta subira. Naomba watakaoweza kutimiza ahadi hizo wawasiliane nami kabla ya Novemba 10, 2007 kabla hatujafanya beta testing.

Nimeshapata wataalamu wa mambo haya ya kompyuta ambao kuanzia jana (tarehe 8 Oktoba) wameanza rasmi kufanyia kazi tovuti hiyo ambayo itakapokuwa tayari (matarajio ni wiki ya kwanza ya Novemba) itakuwa ni tovuti bora kabisa ya habari na maoni ya mambo mbalimbali kuliko tovuti nyingine yoyote ya Watanzania. Lengo ni kuinua ubora wa tovuti za habari na kuziweka kwenye kiwango cha kimataifa. Matunda ya awali nimeanza kuyaona na ndugu zangu, I am impressed (and I don't get impressed easily).

Ninawashukuru
Nawashukuru wale wote ambao hadi hivi sasa wamewezesha kunipa taarifa, mawazo, maoni, ukosoaji na kusahihisha kila nilipopotoka. Natumaini tutaendelea hivyo tunavyoelekea mwisho wa mwaka. Muda ni mfupi lakini safari ni ndefu. Peke yangu siwezi na sitoweza licha ya kujitahidi sana, lakini kwa msaada wenu mambo mengi yanakuwa mepesi kufanyika. Mniunge mkono na mimi nawaahidi sitawaangusha katika kila nifanyalo. Siwaahidi kutokosea, nawaahidi kuwa nikikosoea sitajificha au kuficha makosa yangu! Na nawaahidi siwezi kuanguka bila kusimama tena! Kwani kusimama nitasimama!

Hotuba ya Nyerere Mei Mosi

Katika kukumbuka miaka nane tangu Baba wa Taifa atutoke, Kuanzia kesho Jumatano (Oktoba 10) nitaanza kuwaletea sehemu ya hotuba ya Rais Nyerere aliyoitoa kwenye sherehe za Mei Mosi 1995 ambayo imebakia kama alama ya Nyakati. Kwa wale mlioangalia kipindi cha Jenerali on Monday mtakumbuka kuwa hata Prof. Beregu alinukuu toka kwenye hotuba hiyo. NI hotuba ambayo kwa hakika ilionesha ni upeo na umahiri wa Mwalimu katika kujenga hoja. Kwa kadiri ninavyoisikiliza ndivyo kwa namna fulani naamini kuwa hotuba hii inaanza kunijenga kifikra kama zilivyofanya barua ya MLK na hotuba ya Mandela kizimbani. Natumaini mtachukua muda kusikiliza.

Good job Mwanakijiji,

MUNGU awe nawe kwa kazi nzuri unayofanya kwa niaba ya nchi yako.

MUNGU awabariki pia wale walio na wanaochangia kufanikisha kazi hii.

Thanks very much!
 
Mimi pia nampongeza M.M Mwanakijiji kwa "kujipongeza" kwa kazi murua...........ungesubiri mwisho wa mwaka ndio ingekuwa "magoli" zaidi,hata hivyo chukua tano!!!!!!!!1.
 
Yournameismine, lengo si kujipongeza kwani I don't NEED to do that....Nyani Ngabu alianzisha mada ya "Updates" na kuna mambo ambayo nilitaka niwaupdate watu wanaofuatilia mambo mbalimbali na kuna mambo ambayo yanapaswa kujulikana na mara nyingi najaribu kuleta taarifa ya mambo ninayofanya angalau kila baada ya miezi mitatu. Safari hii nimeamua kuanzishia mada na ni matumaini yangu kuwa ma MoDs wataiunganisha hii na ile ya Nyani baada ya kesho au watakapoona inafaa.

Pia nilitaka kutoa shukrani hadharani kwa wale wote waliosaidia, kwani mtu asiye na shukrani hastahili zawadi, na watu wengi hapa wamekuwa zawadi kwangu na kwa Watanzania wengine kupitia mimi na nimeona ni vyema kushukuru sasa kwani nikipanga kusubiri mwisho wa mwaka inabidi nikubaliane na mbinguni kwanza!
 
Pole zao wanafunzi. Hopefully they can pick up where they left off.
Good going mkuu.
 
Mk/jiji,

I didn't know that you are doing all these, pengine kwa sababu ya ugeni wangu. it is fantastic and well done.

many thanks
 
well done mwana kijiji, sisi tupo pamoja nawe tuombe uzima tu maana under the sun everything is possible may God bless u and add you more where you loose
 
thanks mwanakijiji for your effort, naomba usilegeze kamba uzi ni ule ule mpaka kieleweke. sisi tunachoomba ni uzima tu maana under the sun nothing is impossible.
 
Yournameismine, lengo si kujipongeza kwani I don't NEED to do that....Nyani Ngabu alianzisha mada ya "Updates" na kuna mambo ambayo nilitaka niwaupdate watu wanaofuatilia mambo mbalimbali na kuna mambo ambayo yanapaswa kujulikana na mara nyingi najaribu kuleta taarifa ya mambo ninayofanya angalau kila baada ya miezi mitatu. Safari hii nimeamua kuanzishia mada na ni matumaini yangu kuwa ma MoDs wataiunganisha hii na ile ya Nyani baada ya kesho au watakapoona inafaa.

Pia nilitaka kutoa shukrani hadharani kwa wale wote waliosaidia, kwani mtu asiye na shukrani hastahili zawadi, na watu wengi hapa wamekuwa zawadi kwangu na kwa Watanzania wengine kupitia mimi na nimeona ni vyema kushukuru sasa kwani nikipanga kusubiri mwisho wa mwaka inabidi nikubaliane na mbinguni kwanza!

MMKJJ,
LOL........ile kitu ilikuwa designed ku-trigger response kama hiyo yako hapo juu kwenye quotes, anyway...thanx again kwa yote, kwani you just make my day!!!!!!!!!!
 
mmkjj....

vp kuhusu MUAFAKA KATI YA CUF na CCM,hali ya mheshimiwa MUDHIHIR MUDHIHIR,kesi ya braza dito na MAHALU na KUCHIMBWA MAFUTA ZNZ.
 
MM Mwanakijiji,
juhudi zako zinatupa matumaini makubwa sana,michango yako inafika
hadi vijijini,watu wanapenda makala zako,nasi mashabiki wa KLH tupo
tunakuunga mkono.BIG UP MAN,GOD BLESS YOU.
 
Wapendwa wana JF na Wasikilizaji wa KLH News,

Napenda kutumia nafasi hii kuwapa taarifa za mambo mbalimbali ambayo nimekuwa nikiyafanya na ambayo yana maslahi na wadau wengi hapa. Mambo haya ni yale ambayo aidha yamejadiliwa humu au nimewahi kuwapasha habari zake.

a. Suala la vijana Ukraine:

Suala la wanafunzi waliokwama Ukraine limefikia hatima yake, ingawa ni hatima ambayo mimi binafsi na wazazi wengi wa vijana hawakuitarajia. Tarehe 15 Septemba kundi la mwisho la wanafunzi waliokuwa Ukraine liliwasili nyumbani baada ya kuingia mkopo wa tiketi na deni lao "kushughulikiwa" na serikali. Kati ya wanafunzi wote 29 wachache walikwisha acha masomo, wengine walijirudisha wenyewe baada ya serikali kugoma kabisa na kundi hilo la mwisho ambalo hatimaye lilipatiwa tiketi na kuondoka Ukraine. Ni mmoja tu ambaye hakuweza kuondoka kutokana na uzito wa ushiriki wake katika suala hili zima na hisia kuwa kwa vyovyote vile kurudi kwake Tanzania ingekuwa ni kushindwa kwa jitihada zote za kuhakikisha anaendelea na masomo. Huyo mwanafunzi mmoja kwa msaada wa wadau wa hapa JF tumeweza kuhakikisha amehama toka Chuo Kikuu alichokuwapo na kwenda chuo kingine ambapo familia yake wameahidi kujitahidi kumwendeleza na masomo kama tungewapa tafu kwa mwaka huu.

Tulifanya hivyo na ninashukuru wale ambao tuliwasiliana chemba na ambao waliitikia wito wangu.

Nashukuru kwa namna pekee serikali kwa ushirikiano walioonesha hasa baada ya kuamua kufanya mazungumzo ya chini kwa chini ambayo yaliwezesha vijana hawa kurudi nyumbani na zaidi ya yote kupewa nafasi nyingine ya kuendelea na masomo. Ingawa bado tuna issue ya wanafunzi wachache ambao tunaendelea kushughulikia ni matumaini yangu kuwa serikali hatimaye itaamua kuwasamehe deni la tiketi ambalo walitakiwa kulipia ndani ya miezi sita.

Mke wa Bob
Kwa wale wanaokumbuka mapema mwaka huu nilijitahidi kumuunganisha binti wa Kizambia ambaye alikuwa ameolewa na Mtanzania na waka wanaishi Angola. Mapema mwaka huu kijana huyo Bob alifariki dunia akitanguliwa na mtoto wake wa miaka kama mitano hivi. Alipofariki mkewe alikuwa haijui familia ya marehemu na walikuwa wamepanga kwenda Handeni baadaye mwaka huu. Hivyo kijana huyo alizikwa Angola pasipo taarifa kwa wazazi wake au ndugu yeyote Tanzania. Ndipo jambo hilo likanifikia na kwa kutumia contactz zangu tukaweza kupeleka habari za msiba nyumbani kwa Marehemu na nikaweza kuwaunganisha mke wa marehemu na wazazi kwa njia ya simu na hatimaye kuwezesha mpango wa binti huyo kwenda kuwatembelea huko Handeni katikati ya mwaka huu. Kwa hili namshukuru sana Mbunge wa Handeni Dr. Abdalah Kigoda kwa ushirikiano wote alionipa, na milele moyo wangu umejaa shukrani.

Ujumbe kwa Watanzania
Mapema mwaka huu pia kutokana na mjadala wa "Kuanguka kwa CCM, Unabii Utatimia" lilitolewa wazo la kuandika ujumbe ambao ungeweza kuelekezwa kwa Watanzania wote na ambao utakuwa na nguvu zaidi kuliko Makala ile ya awali. Ujumbe huo umekamilika na uko kwenye uhariri na utatolewa kabla tu ya kuanza kwa mkutano mkuu wa CCM.

Tovuti ya KLH News
Kama mnakumbuka katika mada ya "KLH Kufungwa" nilielezea ugumu unaonipata katika kufanikisha majukumu mbalimbali niliyojitwika ya kuwaletea maoni na habari na katika kutimiza dhana ya "hoja hujibiwa kwa hoja" na ya kuwa kwenye KLH News hapendwi mtu, hapendelewi mtu na haogopwi mtu. Mwitiko wa wadau hapa umenitia moyo sana, wale ambao walitoa ahadi wachache wameshazitimiza na daima nawashukuru na wengine ambao ahadi zao bado ziko njiani ila kutokana na sababu mbalimbali wameshindwa kufanya hivyo hadi hivi sasa. Kwa wao natanguliza shukrani na pamoja nao navuta subira. Naomba watakaoweza kutimiza ahadi hizo wawasiliane nami kabla ya Novemba 10, 2007 kabla hatujafanya beta testing.

Nimeshapata wataalamu wa mambo haya ya kompyuta ambao kuanzia jana (tarehe 8 Oktoba) wameanza rasmi kufanyia kazi tovuti hiyo ambayo itakapokuwa tayari (matarajio ni wiki ya kwanza ya Novemba) itakuwa ni tovuti bora kabisa ya habari na maoni ya mambo mbalimbali kuliko tovuti nyingine yoyote ya Watanzania. Lengo ni kuinua ubora wa tovuti za habari na kuziweka kwenye kiwango cha kimataifa. Matunda ya awali nimeanza kuyaona na ndugu zangu, I am impressed (and I don't get impressed easily).

Ninawashukuru
Nawashukuru wale wote ambao hadi hivi sasa wamewezesha kunipa taarifa, mawazo, maoni, ukosoaji na kusahihisha kila nilipopotoka. Natumaini tutaendelea hivyo tunavyoelekea mwisho wa mwaka. Muda ni mfupi lakini safari ni ndefu. Peke yangu siwezi na sitoweza licha ya kujitahidi sana, lakini kwa msaada wenu mambo mengi yanakuwa mepesi kufanyika. Mniunge mkono na mimi nawaahidi sitawaangusha katika kila nifanyalo. Siwaahidi kutokosea, nawaahidi kuwa nikikosoea sitajificha au kuficha makosa yangu! Na nawaahidi siwezi kuanguka bila kusimama tena! Kwani kusimama nitasimama!

Hotuba ya Nyerere Mei Mosi

Katika kukumbuka miaka nane tangu Baba wa Taifa atutoke, Kuanzia kesho Jumatano (Oktoba 10) nitaanza kuwaletea sehemu ya hotuba ya Rais Nyerere aliyoitoa kwenye sherehe za Mei Mosi 1995 ambayo imebakia kama alama ya Nyakati. Kwa wale mlioangalia kipindi cha Jenerali on Monday mtakumbuka kuwa hata Prof. Beregu alinukuu toka kwenye hotuba hiyo. NI hotuba ambayo kwa hakika ilionesha ni upeo na umahiri wa Mwalimu katika kujenga hoja. Kwa kadiri ninavyoisikiliza ndivyo kwa namna fulani naamini kuwa hotuba hii inaanza kunijenga kifikra kama zilivyofanya barua ya MLK na hotuba ya Mandela kizimbani. Natumaini mtachukua muda kusikiliza.

Na katika sehemu ya kumbukumbu hiyo natarajia kuwa na onesho maalum siku ya Jumapili kupitia bongoradio.com na natumaini kuwa na ugeni mkubwa kwenye show hiyo tunapoangalia nyuma na kumkumbuka Mwalimu. Nitawapa muda na jina la mgeni/Wageni pindi mambo yakitengemaa..

Ndugu yenu na Mtanzania mwenzenu,

M. M. M.

Kazi nzuri sana Mkjj.Ndio mapambano ya kifikra hayo mkuu.Mungu akuzidishie nguvu zaidi.
Mimi bado nina wasi wasi na kuhusu hao wanafunzi kuendelea na masomo.Je mkuu wamepewa ahadi ya kuendelea na masomo katika vyuo vetu vya nyumbani? Na je sina hakika lakini nauliza hakuna ambao kozi zao hazipo katika vyuo vya nyumbani? na kama hakuna je sirikili ahadi gani wamewapa hawa?

Pia kuna suala la kuhamisha credit,najua kuna wengine walikuwa miaka ya mbele.Je kwa Tanzania kuhamisha credit sidhani kama wanakubali.Hawa kama wakitimiziwa "ahadi" ya kuendelea na masomo wataanza upya tena?
Ni hayo kwa muda huu!
 
Mtu, hilo la wanafunzi nitawapa update zaidi baadaye ila kwa wakati huu waliporudi tu juhudi ilikuwa ni kuhakikisha wanaendelea na masomo kwenye vyuo vya nyumbani, tatizo ni masharti yamebadilika na muda wa kuandikisha ulikuwa unapita kwa kasi..
 
Mzeee mwenzangu MMJ,

Heshima mbele mkuuu, ninaomba kukuliza kuwa mtu akitaka kukutumia hela kidogo katika kukusaidia hiii shughuli inakuwaje mkuu, maana kazi yako ni nzito na hukuhitaji kuifanya,

kwa hiyo ustaarabu ni pmaoja na kukuuunga mkono kwa hali na mali, naomba nifahamishe mkuuu, ili tuweze kujipiga piga kidogo,

Salute!
 
Wapendwa wana JF na Wasikilizaji wa KLH News,

Napenda kutumia nafasi hii kuwapa taarifa za mambo mbalimbali ambayo nimekuwa nikiyafanya na ambayo yana maslahi na wadau wengi hapa. Mambo haya ni yale ambayo aidha yamejadiliwa humu au nimewahi kuwapasha habari zake.

a. Suala la vijana Ukraine:

Suala la wanafunzi waliokwama Ukraine limefikia hatima yake, ingawa ni hatima ambayo mimi binafsi na wazazi wengi wa vijana hawakuitarajia. Tarehe 15 Septemba kundi la mwisho la wanafunzi waliokuwa Ukraine liliwasili nyumbani baada ya kuingia mkopo wa tiketi na deni lao "kushughulikiwa" na serikali. Kati ya wanafunzi wote 29 wachache walikwisha acha masomo, wengine walijirudisha wenyewe baada ya serikali kugoma kabisa na kundi hilo la mwisho ambalo hatimaye lilipatiwa tiketi na kuondoka Ukraine. Ni mmoja tu ambaye hakuweza kuondoka kutokana na uzito wa ushiriki wake katika suala hili zima na hisia kuwa kwa vyovyote vile kurudi kwake Tanzania ingekuwa ni kushindwa kwa jitihada zote za kuhakikisha anaendelea na masomo. Huyo mwanafunzi mmoja kwa msaada wa wadau wa hapa JF tumeweza kuhakikisha amehama toka Chuo Kikuu alichokuwapo na kwenda chuo kingine ambapo familia yake wameahidi kujitahidi kumwendeleza na masomo kama tungewapa tafu kwa mwaka huu.

Tulifanya hivyo na ninashukuru wale ambao tuliwasiliana chemba na ambao waliitikia wito wangu.

Nashukuru kwa namna pekee serikali kwa ushirikiano walioonesha hasa baada ya kuamua kufanya mazungumzo ya chini kwa chini ambayo yaliwezesha vijana hawa kurudi nyumbani na zaidi ya yote kupewa nafasi nyingine ya kuendelea na masomo. Ingawa bado tuna issue ya wanafunzi wachache ambao tunaendelea kushughulikia ni matumaini yangu kuwa serikali hatimaye itaamua kuwasamehe deni la tiketi ambalo walitakiwa kulipia ndani ya miezi sita.

Mke wa Bob
Kwa wale wanaokumbuka mapema mwaka huu nilijitahidi kumuunganisha binti wa Kizambia ambaye alikuwa ameolewa na Mtanzania na waka wanaishi Angola. Mapema mwaka huu kijana huyo Bob alifariki dunia akitanguliwa na mtoto wake wa miaka kama mitano hivi. Alipofariki mkewe alikuwa haijui familia ya marehemu na walikuwa wamepanga kwenda Handeni baadaye mwaka huu. Hivyo kijana huyo alizikwa Angola pasipo taarifa kwa wazazi wake au ndugu yeyote Tanzania. Ndipo jambo hilo likanifikia na kwa kutumia contactz zangu tukaweza kupeleka habari za msiba nyumbani kwa Marehemu na nikaweza kuwaunganisha mke wa marehemu na wazazi kwa njia ya simu na hatimaye kuwezesha mpango wa binti huyo kwenda kuwatembelea huko Handeni katikati ya mwaka huu. Kwa hili namshukuru sana Mbunge wa Handeni Dr. Abdalah Kigoda kwa ushirikiano wote alionipa, na milele moyo wangu umejaa shukrani.

Ujumbe kwa Watanzania
Mapema mwaka huu pia kutokana na mjadala wa "Kuanguka kwa CCM, Unabii Utatimia" lilitolewa wazo la kuandika ujumbe ambao ungeweza kuelekezwa kwa Watanzania wote na ambao utakuwa na nguvu zaidi kuliko Makala ile ya awali. Ujumbe huo umekamilika na uko kwenye uhariri na utatolewa kabla tu ya kuanza kwa mkutano mkuu wa CCM.

Tovuti ya KLH News
Kama mnakumbuka katika mada ya "KLH Kufungwa" nilielezea ugumu unaonipata katika kufanikisha majukumu mbalimbali niliyojitwika ya kuwaletea maoni na habari na katika kutimiza dhana ya "hoja hujibiwa kwa hoja" na ya kuwa kwenye KLH News hapendwi mtu, hapendelewi mtu na haogopwi mtu. Mwitiko wa wadau hapa umenitia moyo sana, wale ambao walitoa ahadi wachache wameshazitimiza na daima nawashukuru na wengine ambao ahadi zao bado ziko njiani ila kutokana na sababu mbalimbali wameshindwa kufanya hivyo hadi hivi sasa. Kwa wao natanguliza shukrani na pamoja nao navuta subira. Naomba watakaoweza kutimiza ahadi hizo wawasiliane nami kabla ya Novemba 10, 2007 kabla hatujafanya beta testing.

Nimeshapata wataalamu wa mambo haya ya kompyuta ambao kuanzia jana (tarehe 8 Oktoba) wameanza rasmi kufanyia kazi tovuti hiyo ambayo itakapokuwa tayari (matarajio ni wiki ya kwanza ya Novemba) itakuwa ni tovuti bora kabisa ya habari na maoni ya mambo mbalimbali kuliko tovuti nyingine yoyote ya Watanzania. Lengo ni kuinua ubora wa tovuti za habari na kuziweka kwenye kiwango cha kimataifa. Matunda ya awali nimeanza kuyaona na ndugu zangu, I am impressed (and I don't get impressed easily).

Ninawashukuru
Nawashukuru wale wote ambao hadi hivi sasa wamewezesha kunipa taarifa, mawazo, maoni, ukosoaji na kusahihisha kila nilipopotoka. Natumaini tutaendelea hivyo tunavyoelekea mwisho wa mwaka. Muda ni mfupi lakini safari ni ndefu. Peke yangu siwezi na sitoweza licha ya kujitahidi sana, lakini kwa msaada wenu mambo mengi yanakuwa mepesi kufanyika. Mniunge mkono na mimi nawaahidi sitawaangusha katika kila nifanyalo. Siwaahidi kutokosea, nawaahidi kuwa nikikosoea sitajificha au kuficha makosa yangu! Na nawaahidi siwezi kuanguka bila kusimama tena! Kwani kusimama nitasimama!

Hotuba ya Nyerere Mei Mosi

Katika kukumbuka miaka nane tangu Baba wa Taifa atutoke, Kuanzia kesho Jumatano (Oktoba 10) nitaanza kuwaletea sehemu ya hotuba ya Rais Nyerere aliyoitoa kwenye sherehe za Mei Mosi 1995 ambayo imebakia kama alama ya Nyakati. Kwa wale mlioangalia kipindi cha Jenerali on Monday mtakumbuka kuwa hata Prof. Beregu alinukuu toka kwenye hotuba hiyo. NI hotuba ambayo kwa hakika ilionesha ni upeo na umahiri wa Mwalimu katika kujenga hoja. Kwa kadiri ninavyoisikiliza ndivyo kwa namna fulani naamini kuwa hotuba hii inaanza kunijenga kifikra kama zilivyofanya barua ya MLK na hotuba ya Mandela kizimbani. Natumaini mtachukua muda kusikiliza.

Na katika sehemu ya kumbukumbu hiyo natarajia kuwa na onesho maalum siku ya Jumapili kupitia bongoradio.com na natumaini kuwa na ugeni mkubwa kwenye show hiyo tunapoangalia nyuma na kumkumbuka Mwalimu. Nitawapa muda na jina la mgeni/Wageni pindi mambo yakitengemaa..

Ndugu yenu na Mtanzania mwenzenu,

M. M. M.

Kisha mwenye hotuba ya baba wa Taifa aliyoitoa Dodoma nadhani ni hotuba ya mwisho kabisa katika kipindi chake cha uhai kulihutubia taifa ilikuwa inahusu utunzaji wa mazingira pale ambapo aliahinisha mambo mbali mbali yanayochangia kuharibu mazingira na athari zake akaelezea kwamba itafika wakati visiwa vinaweza kumezwa na maji ya bahari kutokana na kuyeyuka kwa barafu katika poles yaani north pole na south pole ambako kuna barafu zilizogandana akaelezea pia kutatokea vimbunga. Yote haya tumeweza kuyashuhudia kwani ingawa tulijifunza katika geography kuhusu tsunami tumeona vitu hivi. Kuhusu CCM kuja kusambaratika dalili tayari zinajionyesha wazi lakini waliopo madarakani watasema huyo ni nyoka anajichuna ngozi tu. Tujaribu kufuata maadili na miiko ya uongozi tutaweza kunusurika, Mwl anasema kwa mfano kwamba huko UK kuna waziri aliwahi kupatikana na kashfa ya kutembea na changudoa ikabidi ajiuzulu uwaziri kwa sababu hiyo, kashfa am,bayo hapa Bongo ni utamaduni wa viongozi wetu kutenda makosa hayo. Hatutavumilia kuona uozo huu lazima aliyoyasema Mwalimu yatimie. Nyerere ni Nabii.
 
Back
Top Bottom