Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,193
- 25,504
Nawaandikia wapinzani, yaani vyama vyote vya upinzani hapa Tanzania vikiongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Nawasihi kuwa wasithubutu kususia uchaguzi wowote utakaosimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC). Hata kama hayatatokea ya Rais Maduro wa Venezuela ya kukataza waliosusa kushiriki tena, nasema kwa uwazi na uthabiti kuwa kususia uchaguzi ni kujimaliza kabisa. Hatupendi iwe hivyo!
Dunia nzima, hakuna mahali ambapo vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi na uchaguzi husika kutofanyika. Inafahamika kuwa ni kazi pevu, dunia nzima, vyama vya upinzani kupambana uchaguzini na hata siasani na chama tawala. Sababu kuu ni mbili. Mosi, chama tawala ndicho kinachounda Serikali. Hivyo, vyombo vya dola 'huwa karibu' na mtawala.
Pili, chama tawala hakipangi wala kupenda kutoka madarakani. Hufanya kila njia ya kisiasa kubakia madarakani. Siasa, ingawa mimi si mwanasiasa, ni pamoja na mbinu, ubunifu na kuthubutu. Siasa ni mapambano ya kupambania kuongoza Serikali. Harakati zake, tangu zianze hamsini kweusi, hazijawahi kuisha. Harakati za kisiasa za kimapambano hazisusiwi. Huendelezwa.
Wapinzani wapambane kadiri ya uwanja na nafasi iliyopo. Kama mikutano imekatazwa, tumieni media kufikisha ujumbe wenu. Wananchi wakielewa mnachokisimamia watawasaidia kusimamia hoja zenu. Mabadiliko yote ya kisheria na kimfumo yatakuwa rahisi kupatikana. Hakuna ubishi mkubwa kuwa mfumo mzima wa uchaguzi wa Tanzania, ikiwemo Tume ya Uchaguzi, una dosari.
Kwa mfano, uchaguzi ngazi ya Majimbo na Kata kusimamiwa na wateule wa Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama tawala ni dosari kubwa. Ushindi kwa wapinzani, katika mazingira hayo, ni kama ngamia kupenya kwenye tundu ya sindano. Wapinzani husambaratishwa hata kwa mapingamizi na vigisu za kuchelewa kurejeshwa kwa fomu za wagombea.Hatahivyo, wapinzani hushinda.
Hakika, kuna hoja za kidemokrasia za kuzifanyia kazi katika kufanya siasa na wakati wa uchaguzi. Lakini, kususia si njia sahihi. Njia itakiwayo ni kuendeleza mapambano uchaguzini huku changamoto zikibebwa na kuelezwa kila uchao kwa namna mbalimbali. Hatimaye, mambo yatakuwa na nafuu. Lakini, kwa nchi nyingi za dunia hii, upinzani haukuwahi kucheza fair game na chama tawala. Ingawa wapo wapinzani walioibuka washindi.