Navutiwa sana na wanawake wanaojua mapishi

Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
14,007
13,799
Wakuu.

Poleni na mihangaiko na corona pia...Mola atusaidie kuvuka hili jaribu.

Mimi napenda sana mapishi.Na home wanalijua hilo. Napenda sana kula vitu vizuri.
Navutiwa sana na mwanamke anayepafahamu vyema jikoni. Kiufupi ugonjwa wangu ndo upo hapo. Vitu vingine huwa kwa mwanamke huwa sivipi kipaumbele.

Kuna mmoja nilifanikiwa kumpata kipindi cha nyuma. Kiukweli alikuwa anajua kupika vyakula vingi sana kwa ustadi mkubwa. Nilichofanya ni kumuachia kiasi cha pesa na baadaye nikitoka mizunguko nakuta mambo mazuri. Kipindi hicho nilizoea kula restaurant ila niliacha. Kuna wakati nilikutana na majina ya vyakula nisivyovifahamu na nikirudi home namuambia anafanya mpango kwan alivifahamu.

Unfortunately, alinitoka. Kilichofanya nimkumbuke ni baada ya leo kukutana na chakula nisichokifahamu Sanitizer tea. Niwe mkweli sijawahi tumia hiki kitu. Nimepiga kinachonihusu nikaondoka.

Ila yote kwa yote navutiwa sana na wanawake wanaojua mapishi.Uzuri wa mwanamke mimi naujulia jikoni.Pale anapopika huwa namwangalia then najaji mzuri au wakawaida.

BTW nimerudi migahawani tena. Ila nitatokako soon.
 
Tatizo bana sisi wanaume tunaojua kupika tunapata tabu sana kwakweli. Unajua mtu ukishakua unapenda kula vitu vizuri na unajua chakula kizuri kinapikwaje, halafu urudi nyumbani ukute li mchuzi linakutolea macho, manyanya mazima mazima yanaelea, layer ya mafuta juu aaarghh.


Mtu unapambana kutafuta hela, unakuja home umeleta sato wazuri, au maini, au ile nyama pendwa siitaji kwa heshima ya huu mwezi, halafu mtu anakuja anaharibu limboga linakuaje sijui.. yaani hata moyo wa kuleta vitu home unaisha. Sometimes unatamani uwaambie hebu kaeni kushoto niwaonyeshe lakini ndio ivyo tena muda huo haupo..😪😥😥
 
Back
Top Bottom